Mke wangu askari Polisi bado anawasiliana na mzazi mwenzie ambae pia ni askari Polisi

TOFU

JF-Expert Member
Aug 26, 2012
573
196
Habari zenu wanajamvi wenzangu.

Nimeoa askari polisi miaka miwili iliyopita, japo nilimkuta mwenzangu akiwa na mtoto wa kiume.

Kutokana na maelezo yake Baba wa mtoto wake ni Police tena mwenye cheo kikubwa tu

Walishawai kuishi nae ila alimiacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine na kupelekea kuachana

Ila uko alipooa hakuwai kupata mtoto mwingine

Hivyo basi jamaa uyo amekuwa busy na kumfatilia mtoto kulipa ada na garama za mavazi

Sina wivu ila najaribu kutaka ushauri kwenu nyie wakubwa zangu mlionizidi kwa kila kitu kuhusu haya mahusiano

Vile vile sina tatizo na mke wangu.

Tunaheshimiana Tunapendana lakini mwisho wa siku nahitaji kupata ushauri wa tahadhari ili baadae yasinikute

Naomba kuwasilisha ..
 
Kwa hiyo umeoa single mother?
Wakati mwingine vijana matatizo tunajitakia wenyewe. Wewe umejiunga familia ya mkeo, hujaanzisha familia yako. Hivi uliyafikiria haya kabla hujaoa? Yaani as if hukuyajua haya before.

Shauri yako mwenyewe.
 
Kwa hiyo umeoa single mother?
Wakati mwingine vijana matatizo tunajitakia wenyewe. Wewe umejiunga familia ya mkeo, hujaanzisha familia yako. Hivi uliyafikiria haya kabla hujaoa? Yaani as if hukuyajua haya before.

Shauri yako mwenyewe.
Asante Mkuu kwa Ushauri ...
 
"Alimiacha na kwenda kuoa mwanamke mwingne" Mtoto wa kitanga unalilia mapenzi, move on na ww.
Tatizo mkuu tumeshafunga ndoa na tayari tumejaliwa mtoto wa Kike ...
Hana shida tatizo ni hayo mawasiliano tu mkuu...
Naweza kumpiga marufu
Naweza peleka mtoto kwa Baba ake
Lakini naisi bado naitaji ushairi mzuri na wenye busara ili ndoa yetu isije kupata doa siku za mbeleni maana mimi na mke wangu hatujashindwana kwa chochote kile ..
Tunasikilizana fresh tu
 
Tatizo sio kuwasiliana..swali je wanawasiliana kwa mfumo upi?

Kama ni mawasiliano ya kuhusu mtoto naona Ni Bora mtoto akalelewe na Bibi na mawasiliano yawe baina ya baba mtoto na Bibi mkeo kazi yake iwe kutoa maelezo tu kwa Bibi wa mtoto na isiwe zaidi ya hapo.
 
Tatizo sio kuwasiliana..swali je wanawasiliana kwa mfumo upi?

Kama ni mawasiliano ya kuhusu mtoto naona Ni Bora mtoto akalelewe na Bibi na mawasiliano yawe baina ya baba mtoto na Bibi mkeo kazi yake iwe kutoa maelezo tu kwa Bibi wa mtoto na isiwe zaidi ya hapo.
Ukweli ni kwamba mawasiliano mengi huwa kwa issue ya mtoto tu..
Kama kunamengine kiukweli sijawai kuyaona ..
Huwa nayafumania kwenye simu ya mke wangu maana tunatabia ya kushare simu..
 
Ukweli ni kwamba mawasiliano mengi huwa kwa issue ya mtoto tu..
Kama kunamengine kiukweli sijawai kuyaona ..
Huwa nayafumania kwenye simu ya mke wangu maana tunatabia ya kushare simu..
Ongea nae mwambie hufurahishwi na hayo mawasiliano alafu inaonekana mkeo anafanya kwa mawasiliano ya Siri na mzazi mwenzie Kama ni kweli hafanyi Jambo jema
 
Mpelekeni huyo mtoto akaishi na bibi, taarifa, ada n.k atapeleka kwa bibi.

Mawasiliano yakiendelea fanya kugoogle bei ya gunia la mkaa
[/QUOT

Mweleze ukweli mke wako na kama hupendi huyo Baba wa mtoto aje hapo nyumbani basi mshauriane baba yake amchukue nyie mtakuwa mnaenda kumjulia hali kwa Baba yake.
 
Mweleze ukweli mke wako na kama hupendi huyo Baba wa mtoto aje hapo nyumbani basi mshauriane baba yake amchukue nyie mtakuwa mnaenda kumjulia hali kwa Baba yake.[/QUOTE]
 
Habari zenu wanajamvi wenzangu...
Nimeoa askari polisi miaka miwili iliyopita, japo nilimkuta mwenzangu akiwa na mtoto wa kiume..
Kutokana na maelezo yake Baba wa mtoto wake ni Police tena mwenye cheo kikubwa tu ..
Walishawai kuishi nae ila alimiacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine na kupelekea kuachana ..
Ila uko alipooa hakuwai kupata mtoto mwingine ..
Hivyo basi jamaa uyo amekuwa busy na kumfatilia mtoto kulipa ada na garama za mavazi ...
Sina wivu ila najaribu kutaka ushauri kwenu nyie wakubwa zangu mlionizidi kwa kila kitu kuhusu haya mahusiano ...
Vile vile sina tatizo na mke wangu..
Tunaheshimiana Tunapendana lakini mwisho wa siku nahitaji kupata ushauri wa tahadhari ili baadae yasinikute ...Naomba kuwasilisha ..

Kabla ya kumuoa huyo mwanamke au kabla ya kufunga naye NDOA haukupata muda WA kutafakari kuhusiana NA suala hili unaloomba ushauri??? Unaambiwa fikiri kabla ya kutenda, wewe umefanya kinyume chake. Hivi ni KWA nini Wanaume wengi WA siku hizi wapo namna hii??

Suala LA kuoa au kuolewa ni jambo nyeti sana ktk maisha ya binadamu, hivyo basi, kabla ya MTU yeyote yule hajaamua kuingia kwenye NDOA ni lazima kwanza afanye upembuzi yakinifu wa kina kabisa ili kujiridhisha juu ya utayari wake. NDOA siyo jambo LA kukurupuka, hasa unapoamua kumuoa mwanamke ambaye tayari ana mtoto au watoto aliozaa NA mwanaume mwingine.

Kazi kwako, ,"UKILIKOROGA LAZIMA ULINYWE"

"Kalagabao NA ubwenzi wako !!"
 
"Kutokana na maelezo yake".

Kumbe ni maelezo ya Mkeo.

Kwanini na wewe usifanye Uchunguzi wako ili upate kujua anachosema Mkeo ni cha kweli, au si cha kweli.

Kwa KAULI yako hii "Kutokana na maelezo yake", inaonesha fika ya kuwa wewe mwenyewe nusu unakiamini anachokisema Mkeo, na nusu hukiamini.

Hapa kuna UTATA
 
Back
Top Bottom