Mke wangu ananipiga vijembe sana WhatsApp status

Mke wangu ananipiga vijembe sana WhatsApp status

Wazee kwa vijana
wadada kwa wamama.
Jina la bwana lihimidiwe!

Kwa muda mrefu sana hili jambo huwa linatokea baadae linapotea kisha linajirudia tena!

Huyu wife wangu amekuwa akirusha vijembe sana huku whatsap status! Kwa uchunguzi nimegundua kila ikitokea tumepishana kidogo kauli haipiti dakika unakuta ameweka status whatsup:

Mara "USIZARAU DAFU EMBE TUNDA LA MSIMU", siku yingine utakuta "KIKIWA NDANI CHAKO KIKITOKA SIO CHAKO"

LIMEKUSHINDA LIMAO UNAFATA NDIMU"
"WE NI KONOKONO KAMA KONOKONO WENGINE"
"UKITAKA HALUA KUNDU PANUA"

Hizo baadhi ya vijembe ambavyo moja kwa moja najua vinanihusu mimi ni zaidi ya hapo nishamkanya kama anaona tofauti yoyote anieleze kuliko kuanika huko ili kila mtu ajue tumekosana lakini hasikii!

Nikaanza kufikiria niwe namjibu lakini haitakuwa fresh kidume kurushiana maneno mitandaoni. Yaani hata akinipigia simu bahati mbaya sijapokea nikija kuingia tu whatsapp nakuta "MBUZI KUWA NA NDEVU SIO NDIO UANAUME" au "MWANAUME BUKTA".

Kiukweli huwa inanikosesha amani maana kila nikimweleza polepole hanielewi hembu nisaidieni mawazo nifanyaje!
Achana na mambo ya kuhukumu kwa hisia pasipo fact wewe, yaani unafikia hitimisho la hoja yako kwa njia ya hisia! Kweli?! Pole sana
 
Pole sana...
Fanya utafiki kwanza ili uwe na uhakika kama hivyo vijembe ni vya kwako kweli au kuna mtu anagombaniwa hapo na wala siyo wewe...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom