Mke wangu ananipiga vijembe sana WhatsApp status

Mke wangu ananipiga vijembe sana WhatsApp status

Ila usimlaumu sana ndivyo wanawake wengi walivyo, cha msingi mpuuzie wala usipite kuzisoma akiona kila akiweka hujapita basi ataacha mwenyewe,usijaribu kushindana na mwanamke...ila wako amezidi kwa maneno lazima uwe na paracetamol pembeni sio kwa uswahili huo, vijana wenzangu mkioa muangalia na anaefaa
 
ivi kina mama zetu ,mashangazi na hata wana wetu-mtakua wa kukoselewa mpka lini kwa tabia izi mbovu-kaka mpuuzie kwani ukiamua kuacha kulingana na visa vyao utakua wa kuo kuacha-jibu la mjinga ni kumpuuzia tuu,na ikifikia ume pata nae watoto basi mfanye mlezi wa watoto wako,
 
Na wewe nenda whatssap umjibu ...kuwa #I bealive with u my wife A.K.A Danga ...nakuambia atoludia.
 
Wazee kwa vijana
wadada kwa wamama.
Jina la bwana lihimidiwe!

Kwa muda mrefu sana hili jambo huwa linatokea baadae linapotea kisha linajirudia tena!

Huyu wife wangu amekuwa akirusha vijembe sana huku whatsap status! Kwa uchunguzi nimegundua kila ikitokea tumepishana kidogo kauli haipiti dakika unakuta ameweka status whatsup:

Mara "USIZARAU DAFU EMBE TUNDA LA MSIMU", siku yingine utakuta "KIKIWA NDANI CHAKO KIKITOKA SIO CHAKO"

LIMEKUSHINDA LIMAO UNAFATA NDIMU"
"WE NI KONOKONO KAMA KONOKONO WENGINE"
"UKITAKA HALUA KUNDU PANUA"

Hizo baadhi ya vijembe ambavyo moja kwa moja najua vinanihusu mimi ni zaidi ya hapo nishamkanya kama anaona tofauti yoyote anieleze kuliko kuanika huko ili kila mtu ajue tumekosana lakini hasikii!

Nikaanza kufikiria niwe namjibu lakini haitakuwa fresh kidume kurushiana maneno mitandaoni. Yaani hata akinipigia simu bahati mbaya sijapokea nikija kuingia tu whatsapp nakuta "MBUZI KUWA NA NDEVU SIO NDIO UANAUME" au "MWANAUME BUKTA".

Kiukweli huwa inanikosesha amani maana kila nikimweleza polepole hanielewi hembu nisaidieni mawazo nifanyaje!
Umemwendekeza mwenyewe sasa anakutoa jasho. Hakuna namna. Japo sina hakika kama una uhakika kama ni wewe anayekusema.
 
pole kama umeshamweleza aelewe mwache aendelee na vijembe vyake we kuwa kama husomi tena mwisho atajiona mjinga lakini ukiendelea kusoma na kumsemesha anazidisha vijembe. lakini wanawake wengine bana sasa mnagombana na mwenzako unaweka vijembe ili iweje kwamba ndio mtakuwa mmesuluhisha matatizo.
Mi Naona na yeye aweke vipanga au vishpoka hapo wataenda sawa
 
Wazee kwa vijana
wadada kwa wamama.
Jina la bwana lihimidiwe!

Kwa muda mrefu sana hili jambo huwa linatokea baadae linapotea kisha linajirudia tena!

Huyu wife wangu amekuwa akirusha vijembe sana huku whatsap status! Kwa uchunguzi nimegundua kila ikitokea tumepishana kidogo kauli haipiti dakika unakuta ameweka status whatsup:

Mara "USIZARAU DAFU EMBE TUNDA LA MSIMU", siku yingine utakuta "KIKIWA NDANI CHAKO KIKITOKA SIO CHAKO"

LIMEKUSHINDA LIMAO UNAFATA NDIMU"
"WE NI KONOKONO KAMA KONOKONO WENGINE"
"UKITAKA HALUA KUNDU PANUA"

Hizo baadhi ya vijembe ambavyo moja kwa moja najua vinanihusu mimi ni zaidi ya hapo nishamkanya kama anaona tofauti yoyote anieleze kuliko kuanika huko ili kila mtu ajue tumekosana lakini hasikii!

Nikaanza kufikiria niwe namjibu lakini haitakuwa fresh kidume kurushiana maneno mitandaoni. Yaani hata akinipigia simu bahati mbaya sijapokea nikija kuingia tu whatsapp nakuta "MBUZI KUWA NA NDEVU SIO NDIO UANAUME" au "MWANAUME BUKTA".

Kiukweli huwa inanikosesha amani maana kila nikimweleza polepole hanielewi hembu nisaidieni mawazo nifanyaje!
Pambana tafuta pesa mkuu, utaheshimika tu
 
Back
Top Bottom