pole kama umeshamweleza aelewe mwache aendelee na vijembe vyake we kuwa kama husomi tena mwisho atajiona mjinga lakini ukiendelea kusoma na kumsemesha anazidisha vijembe. lakini wanawake wengine bana sasa mnagombana na mwenzako unaweka vijembe ili iweje kwamba ndio mtakuwa mmesuluhisha matatizo.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]m-block watsapp ili usione hivyo vijembe.
Mkuu mtu mwenye dharau hata kama hujamlipia mahara atakudharau. Kuheshimiana hakuangalie kitu chochote. Labda kweli huyo bwana ana mapungufu ya kutosha kwa hiyo mke anatumia udhaifu huoAnamdekeza ndio maana anamdharau. Mwanamke umemuoa na ukamlipia mahari anawezaje kukuletea dharau za kijinga kiasi
hicho? Au inawezekana na yeye kama mume ana mapungufu mengi kwa mkewe yanayomfanya mkewe amdharau. Vinginevyo huo ni ubwege.
Mkuu nawewe mjibu mara moja tu"HILI NIKAMA DALADALA JIANDAE KUSHUKA UPISHE WENGINE"Jitahidi na wew kumpa vijembe
Mkuu ili limenikuta mwanzo ilikuwa tukigombana anatishia kuondoka nambembeleza ila nikaona ujinga, sasa juzi tumegombana nikamwambia kama sepa ..haaa kilichofuatia ni kurusha maneno oh siku hizi nimepata malaya ananitia kiburi mara oh....nilicheka kimoyomoyoMwanamke akigundua anachofanya kinakuumiza. Umekwisha !. Tena ukimuuliza kuhusu alichofanya anajua IMETICK ,atakusumbua wewe.
Mwanamke hata akikwambia baba fulani naona tuachane mwambie SAWA haina shida uone kama ataondoka, utaskia unataka ubaki na hao malaya zako eee. SIONDOKI. Huwa nacheka sana
Kuoa wanawake wa pwani lazima na wewe uwe umezoea hayo maisha lasivyo unaweza chinja mtu kimya kmyaWazee kwa vijana
wadada kwa wamama.
Jina la bwana lihimidiwe!
Kwa muda mrefu sana hili jambo huwa linatokea baadae linapotea kisha linajirudia tena!
Huyu wife wangu amekuwa akirusha vijembe sana huku whatsap status! Kwa uchunguzi nimegundua kila ikitokea tumepishana kidogo kauli haipiti dakika unakuta ameweka status whatsup:
Mara "USIZARAU DAFU EMBE TUNDA LA MSIMU", siku yingine utakuta "KIKIWA NDANI CHAKO KIKITOKA SIO CHAKO"
LIMEKUSHINDA LIMAO UNAFATA NDIMU"
"WE NI KONOKONO KAMA KONOKONO WENGINE"
"UKITAKA HALUA KUNDU PANUA"
Hizo baadhi ya vijembe ambavyo moja kwa moja najua vinanihusu mimi ni zaidi ya hapo nishamkanya kama anaona tofauti yoyote anieleze kuliko kuanika huko ili kila mtu ajue tumekosana lakini hasikii!
Nikaanza kufikiria niwe namjibu lakini haitakuwa fresh kidume kurushiana maneno mitandaoni. Yaani hata akinipigia simu bahati mbaya sijapokea nikija kuingia tu whatsapp nakuta "MBUZI KUWA NA NDEVU SIO NDIO UANAUME" au "MWANAUME BUKTA".
Kiukweli huwa inanikosesha amani maana kila nikimweleza polepole hanielewi hembu nisaidieni mawazo nifanyaje!
Kinondoni+sinzaduh...mademu wa Tandale hao .....utajuta
"hukufanya home work yako vizuri wakati unataka kuoa"Mwanamke mwenye tabia kama hizi ni rahisi kumfaham mapema sana, hukufanya home work yako vizuri waka unaooa, USHAURI WA MAANA KULIKO YOTE "MPUUZE WALA USIMUULIZE"
"hukufanya home work yako vizuri wakati unataka kuoa"
Quote of the year 2018
Sure umeongea kaka. Yani mimi kuandika status huwa nafikiria mno tena nikiwa nina stress au nimekwazwa ntaishia kuandika "In God we Trust" 😀Mke au demu tu???
Mkeo kuandika mambo ya kipumbavu kama hayo kwenye mitandao kama vile ulimtoa SEWA na unamwangalia tu...!!!!na hata kama hakuandikii wewe hivyo vijembe we unadhani imekaa powa kwa mtu anayeitwa mke kuandika hizo vitu kwenye mitandao???kama ni kweli ni mke rudisha ulipomtoa kama ni demu tu unasumbua tu wadau bure
umemjibu vizuri! sanaUmeoa mswahili au mlikutana whatapp group nini
🙂🙂Mkuu nawewe mjibu mara moja tu"HILI NIKAMA DALADALA JIANDAE KUSHUKA UPISHE WENGINE"