Mke wangu ananilazimisha nimuombe msamaha mbele ya Kanisa

Wakuu nawasalimu,

Niko katika hali hii kwa sasa.

Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.

Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.

1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.

2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.

3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.

Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?

Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?

Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.

Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.

Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.

Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.

Bora kaombe kanisani, mbona nappe na makamba wameomba msaaha tena mwanaume mwenzao, kwa magoti toka IFM mpaka ikulu
 
Kisha danganywa na mchungaji huyo. Hapo hakuna msamaha kinachotafutwa ni promo ya kanisa.
 
hii thread ilinifanya nipigwe ban, leo sitii neno , naunga mkono upuuz wa huyu mwanamke 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kama ni swala la kweli yani inaonyesha ndoa za vijana wa leo hazina misingi mizuri ya kimakuzi na heshima ya ndoa. Wazee wetu walioana vijana sana ila maadili na uadilifu wa nafasi zao ulikuwa wa kiwango cha juu sana. Tuwe na maandalizi mazuri kwa watoto wetu aisee maana sisi tumeshakuwa maututi tayari, wanaopona ni wachache sana.

Kwa sasa ni kheri kuchelewa kuoana ili kujitafakari na kufanya maamuzi yaliyotukuka ukiwa umeiva na sekta hii ya ndoa na sio maandalizi ya harusi nzuri/kifahari. Issue ni mda tu, haina kufeli.
 
Mkuu wewe kama ni kristo una kazi kubwa ya kufanya,kama mlifunga ndoa na ulikuwa na msimamizi wako wa ndoa haya ni mambo unayotakiwa kumshirikisha kama yupo.Lakini pia baada ya kutenda hiyo dhambi ambayo hujaitaja,umeona sehemu ya kupata ushauri kwa mambo yako ni hapa JF?Si manishi hapa JF hakuna watu watu wa kukushauri lakini naona kabla ya kuleta hapa kwa watu ambao wengine wamejificha nyuma ya ID wanazotumia ungetafuta watu wenye hekima huko kanisani kwenu wakakushauri.Umekosa kabisa wenye hekima huko kanisani kwenu?Kama ulikuwa hujui,mkeo anakujua kuliko hawa watu hapa JF hata kama ana mapungufu,nani hapa anyekujua wewe zaidi ya mkeo?Kama wewe unaufahamu naamini ulioa mwanamkem mwenye ufahamu na ulikuwa makini katika kuoa labda kama ulikutana naye instagram kama wengine wanavyokubeza.
Wewe inawezekana unapenda sana siri hivyo umeogopa kushirikisha watu wanaokujua ili matatizo yako wasiyajue na umekuja hapa JF ili upate ushauri kwa watu usiowajua na wao hawakujui.Swali kwako,una uhakikia mkeo hayupo hapa JF na hajaiona hii post?
Waombe viongozi wa hapo unapoabudu wawape mafundisho ya ndoa na mambo ya familia kwani unasafari ndefu,hakuna general formula kwenye ndoa.Nikimlinganisha mkeo na wewe naona yeye amejitahidi kukupeleka kanisani ila wewe umemleta JF,hapo wewe huoni tofauti?Mambo ya wewe umwite mama na akurekodi inawezekana aliyaongeza kama chumvi tu akuone je ni kweli unampenda na umejutia kosa lako kutoka ndani.Inshort umefail mtihani wake,biblia inawasihi wanaume waishi na wake zao kwa akili si kwa mabavu.Kuna mshauri wako mmjo anaitwa Joka mweusi sasa kweli ndugu yangu unashauriwa na joka mweusi anakwambia yeye anatisha.Soma alichokushauri.
Ndoa ni mpango wa Mungu na haijawahi kuwa ndoano,ndoa ni ndoano ni maneno ya wapagani wasiojua aliyeanzisha ndoa ni nani. Na kama ulichepuka biblia inasema "azinie na mwanamke hana akili kabisa,afanya jambo loitakaloiangamiza nafsi yake".
Ni muhimu mwanadoa upate ushauri kwa mtu mwenye ndoa au mtaalam wa mambo ya ndoa na familia.Ushauri wa bure muda mwingine huwa ni matatizo hasa kama anayeshauri hana ufahamu wa kutatua tatizo husika.
Mimi napita tu.
Asipochukua huu ushauri basi, ndoa sio ubabe !
 
Kama ni swala la kweli yani inaonyesha ndoa za vijana wa leo hazina misingi mizuri ya kimakuzi na heshima ya ndoa. Wazee wetu walioana vijana sana ila maadili na uadilifu wa nafasi zao ulikuwa wa kiwango cha juu sana. Tuwe na maandalizi mazuri kwa watoto wetu aisee maana sisi tumeshakuwa maututi tayari, wanaopona ni wachache sana.

Kwa sasa ni kheri kuchelewa kuoana ili kujitafakari na kufanya maamuzi yaliyotukuka ukiwa umeiva na sekta hii ya ndoa na sio maandalizi ya harusi nzuri/kifahari. Issue ni mda tu, haina kufeli.
Wanandoa wengi hawana ufahamu wa kuishi na ndoa wanachojua ni kimoja tu
 
Alifanya dhambi gani huyo mpk akupe sharti la namna hiyo? Kama umeamua kuja hapa hebu weka hilo kosa hapa unaloliita dhambi!

Nakushauri usikubali, unajua hilo ni kanisa la kiroho ndilo linatoa nafasi kama hiyo, mkeo anataka kukudhalilisha na pia aonekane mbele za washirika kwamba amekuweza? So usijaribu huo ujinga, wewe ni mwanaume linda uanaume wako!? Ndio maana ataka mrecord ili aibu hiyo usiweze kuifuta, kwanini anataka watu wengine waje kuona? Kwa masharti hayo mm mke wng angekuwa ameshindwa ndoa!

Je alifanya hiyo dhambi hadharani? Je mlimgegeda mshirika ukamtia mimba? Au umemtia mimba Mdogo wake? Acha ufala wewe komaa mmalizane ndani!
Hii dhambi itakuwa alichepuka na mchepuko 😂😂😂
 
Kuna siku nilienda kubariki pete ya ndoa kanisani, wife akaona ndio fursa ya kuchomekea kwa mchungaji mambo (madhambi) yangu mengine mchungaji anishauri, nilimkata jicho moja akajua leo huko home hakukaliki akabadili hapo hapo na kumwambia mchungaji ananiombea na anaona mabadiliko, baada ya kutoka hapo church aliomba msamaha meenyewe kwa kuwa nilishamuambia mambo yetu ya ndani ni ya ndani nisikie tena kwa mtu mwingine
 
Kuna siku nilienda kubariki pete ya ndoa kanisani, wife akaona ndio fursa ya kuchomekea kwa mchungaji mambo (madhambi) yangu mengine mchungaji anishauri, nilimkata jicho moja akajua leo huko home hakukaliki akabadili hapo hapo na kumwambia mchungaji ananiombea na anaona mabadiliko, baada ya kutoka hapo church aliomba msamaha meenyewe kwa kuwa nilishamuambia mambo yetu ya ndani ni ya ndani nisikie tena kwa mtu mwingine
Kama madhambi yako mwenyewe unayaonea aibu si uache jamani...heee
 
Kama madhambi yako mwenyewe unayaonea aibu si uache jamani...heee

Ishu siyo madhambi yangu, ni namna ya kutatua changamoto zetu za maisha ya ndoa, sasa yeye kutaka kumwambia mchungaji ninarudi usiku ama ninakunywa pombe inasaidoa nini?na kuacha siwezi

Pili kupeleka mambo kanisani maana yake yameshindikana kabisa katika ngazi zote kuanzia kwetu wanandoa, wasimamizi wa ndoa, na wazazi...hatujapitia kote huko na tatu hayakuwa mambo ambayo tulienda kufanya hapo siku hiyo
 
Hahaha
Msimamo wako na uwe huo huo mkuu,

umeshamuomba msamaha yeye kama yeye, na bila shaka ulimkosea yeye kama yeye!
Sasa inakuaje tena ukaombe msamaha mbele ya kanisa?
Tena eti na mkanda wa video uchukuliwe.

Aise mliooa walokole kazi mnayo.
Mimi akinitamkia huo upuzi eti nikapige magoti mbele ya kanisa na huku narekodiwa, nitamnasa kibao huyo.
Kumuomba msamaha tu umempatia heshima, yake inatosha.
 
Hahaha
Naskia ucchungu wanaume tunazidi kupungua...

Mke wako amepata wapi ujasiri wa kukwambia upuuzi huo aiseee !!!

Hata Mungu hapendi ujinga kama huo kasema tuungame dhambi zetu kimya kimya sio kudhalilishana..

Au ndugu yetu umekwama jogoo hapandi mtungi
 
Back
Top Bottom