Mke wangu ananifuatilia FB

Kumbe wanaong'ang'ania kukagua Simu za wapenzi wao wanakuwa si waaminifu eeh?

Pole sana kaka, mara nyingi macheaters ndio wanaoongoza kuwa na wivu!
 
IGWE jua kwamba huyu sio demu wangu, ni MKE wa ndoa na hapo ndipo nashindwa nifanye nini na kuamua kuwaomba ushauri
<br /> <br / mtandike kama humjui then mtimulie mbali, mke gani anamegwa hovyohovyo? Hy hana tofauti na jibwa koko.
 
Achana na Facebook.

Facebook imekuwa chanzo cha mitafaruku mingi sana kwenye mahusiano. Mimi kama mimi sipo huko Facebook. Nipo ila nipo ki JF zaidi. Natumia jina la Nyani Ngabu na hata hivyo sijaingia huko tokea sijui lini..hata sikumbuki.

Watu huko huuza sura tu. Kila leo wanabandika mapicha yao halafu wanasubiri kumwagiwa misifa...ooh sijui you are beautiful...sijui I miss you...mara you look gorgeous...sasa kaka hebu fikiria kidogo. Yaani kama una mwenzako yuko huko halafu minjemba inamwagia misifa hivyo utapata amani kweli moyoni na akilini mwako? Vivyo hivyo kwako. Kama wachuchu wanakumwagia misifa kem kem mkeo au mpenzio unadhani atakuwa na amani kweli? Mimi sidhani hata kidogo.

Uamuzi wa mwisho ni wako. Ukiamua kubaki..poa tu...ukiamua kuachana nayo...na yenyewe haina ubaya. Mwisho wa siku pima uone jambo lipi ni la muhimu zaidi na fanya uamuzi kulingana na majibu utakayopata.

NN twapaswa kutatua tatizo badala ya kulikimbia...... Atakimbia social networks ngapi? Maendeleo yatakua yanasonga sisi tunarudi hatua tatu nyuma na kujipongeza kama alivyosema Prof J.....

Kimsingi hapo jamaa yeye ndo anajua root of the prob. Naamini hajasema yote...... Ameonyesha kidogo tu kwamba there's a marital infidelity...... Kutoka kwa wote na hususani kwa mwenza wake.... Na it appears hawajakaa na kuongea.... Anasubiri wamarekani watoe tena mafungu ya matangazo ya kuhamasasisha wanandoa au waliok ktk uhusiano kukaa na ku-discuss kuhusu mahusiano yao??????????
 
Kwangu Facebook haina umuhimu wowote na siifagilii. Ninaweza kuishi bila nayo.
 
Kwangu Facebook haina umuhimu wowote na siifagilii. Ninaweza kuishi bila nayo.

NN kumbuka huko awali aliwahi kunituhumu kwa kutumia simu, je ningeacha kutumia simu? n baadae akadai kazini nina wapenzi, je ningeacha kazi pia? leo faceboo na kesho itakuwa kingine, kila kitu niwe nakiacha??
 
kumbuka alianzia katika simu, je ningeacha kutumia simu ili yaishe? akahamia kuwa nina wapenzi kazini, je ningeacha kazi pia ili aniamini?

daaah huyo wako kiboko.. hawa watu ni vigumu sana kuwaelewa japo sio wote! ukiona mtu anakushuku sana ujue yeye ndio anafanya hivyo
 
Mie Mlutheri, Mke mmoja maisha yote na hapo ndipo pananikosesha amani kila ninapofikiria kumuacha

Haya mambo ya kukariri hayana maana kabisa_wanandoa hawataachana ila kwa uzinifu(ugoni),....kama anamegwa na ushahidi unao achana nae,...ila mm hata kama nikifunga ndoa leo halaf kesho nikagundua mama igwe kamegwa_hapo hapo ni ooshhhh_koshiiii....sipendi maisha ya kujitesa wakati kuna way out
 
NN kumbuka huko awali aliwahi kunituhumu kwa kutumia simu, je ningeacha kutumia simu? n baadae akadai kazini nina wapenzi, je ningeacha kazi pia? leo faceboo na kesho itakuwa kingine, kila kitu niwe nakiacha??

Kwani ulikuwa unaificha ficha na kumkataza kuishika simu yako?
 
Hii story ya upande mmoja.why mkeo akufuatilie.inawezekana na ww hujatulia
 
Kwani ulikuwa unaificha ficha na kumkataza kuishika simu yako?

Sijamkataza, lakini ilikuwa akiishika asione msg toka kwa msichana yoyote hata ikiwa ni salamu tu patachimbika. baada ya simu kahamia kazini eti kaambiwa nano nina wanawake kibao
 
Hii story ya upande mmoja.why mkeo akufuatilie.inawezekana na ww hujatulia

Fe, siwezi kupingana na hisia zako, lakini kama umesoma vema posti utakuwa umeelewa kuwa kote anakofanya mie nikigusa tu namgundua kufanya uchafu. Kwenye simu nikagundua na akakiri, kutembea na rafiki yangu nikagundua na akakiri pia. Ninachohisi ni kwamba anahisi yale anayoyafanya basi na mie nayafanya pia kitu ambacho sio
 
Sijamkataza, lakini ilikuwa akiishika asione msg toka kwa msichana yoyote hata ikiwa ni salamu tu patachimbika. baada ya simu kahamia kazini eti kaambiwa nano nina wanawake kibao

Lakini kwa nini kama umeoa uachie/ uruhusu wasichana wawe wanakutumia salamu kwenye simu yako? Wewe huoni kama ulimpa sababu ya kukushuku?
 
mbona hyo ipo wazi kabisaa? Mkeo ana mahawara fb na kwingineko. Halafu wewe ni mwanaume hebu kuwa serious (mkali) na mkeo. Kakupanda kichwani then anamegwa. Kha!
 
Lakini kwa nini kama umeoa uachie/ uruhusu wasichana wawe wanakutumia salamu kwenye simu yako? Wewe huoni kama ulimpa sababu ya kukushuku?

NN unataka kusema kwakuwa nimeoa basi sitakiwi kusalimiwa na wasichana wa aina yoyote? mfano wale tuliosoma nao, wale tunaotoka nao kijiji kimoja ama mkoa mmoja? wale niliowahi kukutana nao kwenye mikutano ya kikazi il mradi tu eti mke wangu asione nawasiliana na msichana yoyote???? Tena sio msg ya mapenzi ama dalili ya kuwepo mapenzi, salamu tu???
 
Jamani waungwana naomba msaada wenu huyu mke wangu mie simuelewi kabisa.

mwanzoni mwa mahusiano yetu alikuwa na tabia sana ya kuchunguza simu yangu na hakuwahi kugundua message yoyote mbaya ingawa hata msg isiyo ya kimapenzi ikiingia kwenye simu yangu so long as inatoka kwa mwanamke basi siku hiyo ni vurugu kupita kiasi akidai huyo mwanamke atakuwa bibi yangu ama mpenzi wangu tu. siku mie niliposhika simu yake siku moja, nikagundua msg nyingi za kimapenzi toka kwa wanaume wawili tofauti, anaomba radhi nikamsamehe.

Baada ya muda alikuwa akinisumbua kwa kudai kuwa mimi nina uhusiano na wanawake chungu tele kuanzia wale ninaofanya nao kazi hadi mtaani. Baada ya kuchunguza nikagundua kumbe yeye ndio ana mahusiano ya kimapenzi na rafiki yangu. mini ni mvumilivu nilimsamehe ingawa ni baada ua kukana sana na mwisho wa siku akakubali. hayo yakaisha mwaka jana.

Sasa hivi amekuja na mpya. Anasema kila mwanamke ambaye ni rafiki yangu facebook kwamba ni bibi yangu na anakomaa kwelikweli. mie nashindwa hata nimwambie nini ili aamini kuwa mawazo yake sio kweli maana kuna wasichana zaidi ya 1000 kwenye orodha ya marafiki zangu fb na wavulana kama 1000 wengine. kila comment yangu kwa mwanamke yoyote inakuwa ugomvi hauna mfano, kisa eti na comment kwa bibi yangu. kwakweli sina amani kabisa na hali hii inanikosesha raha.

Naomba waungwana mnisaidie nifanye nini maana nahisi kama anaanza tena kuficha uovu wake kwa kunipakazia mie, nahisi tu hilo sijafanya uchunguzi tena.

Mkuu...
Unasema kwamba u mtakatifu katika uhusiano wenu?
Kwamba huna noma?
Kwamba unasamehe noma zote?
 
NN unataka kusema kwakuwa nimeoa basi sitakiwi kusalimiwa na wasichana wa aina yoyote? mfano wale tuliosoma nao, wale tunaotoka nao kijiji kimoja ama mkoa mmoja? wale niliowahi kukutana nao kwenye mikutano ya kikazi il mradi tu eti mke wangu asione nawasiliana na msichana yoyote???? Tena sio msg ya mapenzi ama dalili ya kuwepo mapenzi, salamu tu???

Mimi kwa kweli sidhani kama ni busara ku maintain mawasiliano na wana wa jinsia tofauti ilihali umeoa. Maneno yangu yanatokana na maoni yangu. Hivyo ndivyo nionavyo mimi. Wengine wanaweza wakaona tofauti.

Mwisho wa siku kila mtu na maisha yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom