Mke wangu ananichanganya

Mkuu, kabla hatujaelekeza lawama zetu kwa mkeo labda ungejibu maswali haya machache;
1) Hali yenu ya kiuchumi ilikuwaje wakati mnaoana na huyo mkeo?
2) Leongo la yeye kutafuta kazi lilikuwa ni lipi?
3) Mlijadiliana na mkeo kwa kina sababu za yeye kutafuta kazina namna hiyo kazi itakavyo wanufaisha katika maisha yenu?
4) Mipango yako ya kuoa ilikuaje? Kwa maana ya mama wa nyumbani ama mfanyakazi, ili uweze kukabiliana na changamoto za maisha?
5) Nini falsafa yako kuhusu ndoa na mke wa kuishi nae?
 

mkuu posti zako 2 umemaliza kila kitu mi naunga mkono na mguu hoja zako.

ila hapo kwenye bold umenifurahisha sana siyo hili jiwe la mwadui .
 

ndo maana nimemwambia apambane kiume siku mkewe akijisikia atachangia kipato coz hana option nyingine.
 
Mkeo tabia zake ulitakiwa uzijue kabla hujamuoa.

Kama zinakuboa huwezi kuvumilia mtaliki.

Kama unaweza kusuluhisha au kuvumilia pelekana naye hivyo hivyo.

Wengine tukikataa kuoa kuepuka drama mnatucheka lakini ukweli ni kwamba ukishaoa halafu mwenzako akaamua kukucharukia imekula kwako.

Ndoa ndoana, Kiranga hujambana.
 
mmoja wapo ni huyo dada uliyemquote, kupitia comments zake tu utagundua ni aina gani ya mwanamke...

yaani mi huwa nawacheki tu. Kuna wachache huwa nawachukulia kwa umakini kwani ushauri wao uko kifamilia zaidi. Lakini hawa mafeminist mara nyingi ushauri wao uko kimatumizi zaidi. Sehemu kubwa ya hawa hawana familia au zimewashinda au wanabambia waume za watu.
 

Biblia iko wazi inasema asiyefanya kazi na asile, na pia inampa wajibu mwanamke kutafuta chakula cha familia yake, someni kitabu cha mithali, tatizo wanawake wengi wanataka kuendesha ndoa zao kwa umbea na ushauri wa vijiweni badala ya kutafuta maongozi ya biblia. mpeleke kwa mchungaji akampe ushauri nasaha,

mkumbushe familia haijengwi na mtu mmoja bali ni joint efforts
 

This is your private business. Solve problems. Acha kutoa siri za ndani ya nyumba yako.
 


Umesahau kumuuliza,kabla hajapata kazi maisha yalikuwa rahisi kiasi cha yeye ku-provide mahitaji yote?
 
kasome mithali 31:10-31. mke mwema analisha familia yake na kuhudumia kwa kila kitu. Binafsi huwa namuomba sana Mungu anizidishie uwezo wa kuhudumia familia yangu ingawa mume wangu yupo responsible sana, natamani niwe mke mwema anayetajwa katika mithali 31.
 
Ndiyo maana kuna Adamu na hawa (Siyo Hawa). Meaning Adam and "these". They are weak at some points.
 
pole sana kiukweli hili jambo ni kama utamaduni,nje ndio wana huo utamaduni wa kushare cost of living ila kiafrica mwenye rensponsibility ya kulisha familia ni baba lol ila hali imebadilika ongea naye taratibu naye acontribute...........................,ila hujasema exposure yake ya education na kipato chake nahisi pengine kapata kazi ya kipato kidogo sana sana inatosha kwa vitu vidogo,na pengine kabla ya kupata kazi alikuwa anasuffer in silence kwa kukosa(wewe kutomprovide) pesa ya mambo yake madogo.....all in all ndoa yenu inahitaji tena kufufua mawasiliano kabla haijafa lol
 
kuweza ni kusaidia majukumu pia,sio kukaa kwenye media na kupiga kelele na sisi tunaweza wakati vitu vidogo tu vyawashinda
 
pole, jifanye kama mkeo hana ajira kwani kabla hajapata ajira maisha yalikuwa mepesi?
 

haya maswali yangepata majibu tungekushauri vyema zaidi!!
 
Kaka usidhani kama uko peke yako uwezi amini yaani karibu wanawake wote ndo wako hivyo ila usihofu ni ulimbukeni tu ndo unawafanya wawe hivyo ila baada ya muda atajiona ni mjinga na ataacha hiyo tabia!
 
sio fair bwana,mwanamke ni msaidizi wa mume. si amsaidie mume wake tu jamani.
sasa usaidizi si akileta nyama wewe unapika? Ama mnasaidiana, heheheh!
Kua uyaone maghorofa ya ndoa mdogo wangu. Mie.msaada natoa kwenye kununua magari na kujenga maghorofa, lol! Ngoja nsiseme mie, tutakuambia kwenye kitchen party!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…