Mke wangu ana Mawasiliano na Mkwe na Mashemeji wa X wake. Pia ana account ya Social Network ambayo ameniblock siwezi kuiona anachoweka huko

giphy.gif
 
Wewe hadi umeoa basi unaakili timamu.

unasema unampenda mkeo basi zidisha upendo ipo siku ataacha hayo mambo mkuu.

Ndoa sio mchezo mkuu...kuoa na kuacha unajitia GUNDU tu....

Tuliza akili itulie huwenda pia anakupima IQ yako inauwezo wa namna gani katika kufikilia.....ACHANA NA MHEMKO
 
Hapana Hana mtoto
Sawa sasa uzoefu wangu unaniambia hivi......
1. Huyo mkeo alikubali kuolewa na wewe kwasababu alihitaji harusi na sio ndoa.
2. Inavyo onekana mkeo bado anaupendo wa dhati kwa X wake na bado anamatarajio na mipango flani ya mbeleni kwenye familia ya X wake.
3. Kwa mtazamo wangu mimi huyo sio mke wako, bali unaishi na mke wa mtu.
4. Ulijikuta unaoa mwanamke ulie mpenda pasipo kujipa nafasi ya kumjua vizuri.
5. Nahisi unamadhaifu flani kwa mkeo na tayari amesha yagundua.

Ushauri wangu ni:-
Ingekua mimi ndio wewe, baada ya kupata ushahidi ulio jitosheleza wala nisinge hangaika kutafuta ushauri na nisinge waza mara mbili, bali ninge mpiga chini pasipo kujali maumivu yangu ama yake. Baada ya hapo ningezima masikio kwa maneno na mashambulizi yoote ambayo ningetupiwa na ndugu jamaa na marafiki.
Na mwisho kabisa nisinge kubali ushauri wa aina yeyote kutoka kwa mtu yeyote kwasababu hakuna kati yao ambae angenisaidia kuyabeba maumivu ambayo nimeyapata.
Mwisho kabisa, dalili ya mvua ni mawingu walisema wahenga.
 
Mambo.
Mi Ni mwanaume mimeoa muda si mrefu Sana, nampenda mke wangu, lakini changamoto ninazoziona hata raha ya ndoa siioni.
Tatizo ninaloliona kwa mke wangu Kwanza Ni Mawasiliano na Mashemeji zake na Mkwe wa X wake.

Hili Jambo nimejaribu kumueleza aliache naona Mawasiliano yapo vile vile. Nimegundua Jambo lingine ana Account ya Social network ina picha Nyingi alizopiga na X wake, na ameandika maneno mengi ya mahaba kumuhusu huyo X wake anavyompenda. Kiukweli nimeumia kwa kuwa nampenda. Hiyo account ipo active anaitumia Mara kwa Mara kuandika maneno ya mahaba anavyompenda huyo X wake. Mpaka leo nimeona maneno mengine ya mahaba.

Najikuta naumia kwanini alikubali kuolewa na Mimi ili Hali Moyo wake Bado unampenda X wake.

Nawaza na kuwazua sikupenda kuoa na kuacha Ila changamoto hii ya kuwa na Mke ambae ametunza picha za X wake na Mawasiliano na mashemeji, naona Kama ipo siku atarudi kwa X wake. Au Tuta shere(Magonjwa mengi ya zinaa)

Naomba ushauri wako, ndugu Yangu.
Bila shaka huyu mke ni single mom.
 
Back
Top Bottom