Mke wangu ana HIV nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wangu ana HIV nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Hemed Maronda, Nov 2, 2010.

 1. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeanza kuishi na huyu mwanamke toka mwaka 2007 wakati huo tulikuwa tunaishi kama wapenzi na tulikuwa tunatembeleana tu yeye akiwa Dar na mimi nikiwa nafanyakazi Mbamba Bay lkn ilipofika mwezi Desemba 2009 niliamua nipeleke barua kwao ili nioe,jambo la ajaabu lililotokea nilitajiwa mahali kubwa sana yaani Tshs 4,500,000/= mimi nilkawa nimeshindwa kuilipa na ndoa ikashindikana na yeye akarudi kwao Arusha, niliumia sana kwa kukosa kumuoa ilipofika mwezi Machi 2010 yeye alinipigia simu na kunieleza kuwa yuko tayari kuja kuishi na mimi Mbamba Bay ingawa wazazi wake walinitajia mahali kubwa,nilikubali kumpokea na kweli alifika.
  Maisha yetu yalikuwa mazuri sana na kila mmoja wetu alisahau tofauti zilizotokea, lkn baada ya kama mwezi mmoja alianzisha ugomvi ambao tulishindwa kuusuluhisha na aliomba nauli ya kurudi kwao na nilimpa.
  Ilipofika mwezi Juni 2010 aliomba radhi na akaniomba tuishi tena na mimi bila kinyongo nilikubali ila moyo wangu ulikuwa na wasiwasi kidogo nikaona kuwa safari hii atakapokuja basi ni lazima tucheki HIV.Nikikwenda kumpokea Mbeya na alipofika tu nilimweleza kusudio langu la kupima HIV mimi na yeye .Tarehe 6 Julai tukaenda kupima pale Hospitali ya Rufaa matokeo yake yeye akawa amekutwa na Virusi vya UKIMWI na mimi nikawa sina! Tulipewa maelekezo ya jinsi gani ya kuishi katika mahusiano yetu.Mwenzangu aliipokea hali yake kwa majonzi na mimi nikawa na kazi ya ziada kumtuliza,tukarudi wote Mbamba Bay ila baada ya kurudi tu kama wiki mbili akanywa sumu ili afe,tulimuwahisha Hospitali na tukafanikiwa kuokoa maisha yake,lkn ghafla akanijengea chuki ambayo haina mfano na aliahidi mbele yangu kuwa ni lazima aniue! Niliwaelezea wazazi wangu na wazazi wake pia,wazazi wangu wakanishauri nimrudishe kwao na mke wangu akawa hataki kurudi kwao na tuliendelea kuishi hivyo hadi mwezi Oktoba tarehe 16 alipoamua kuondoka mwenyewe.Ingawa mke wangu ameondoka bado nampenda ila nilipokuja kufanya uchunguzi zaidi nimekuja kufahamu kuwa maisha yake yalikuwa ni ya kutangatanga sana na hivi sasa yupo Dar! Nifanyeje?
   
 2. TWISA

  TWISA Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nenda taratibu dogo, waone washauri wa hizo issue!!!!
   
 3. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa ushauri wako ila naumia sana moyoni kila siku nakosa usingizi kwa kufikiria jambo hili naona UTAMU WA MAPENZI UMEKULA KWANGU!
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ....daaaahhhh, am speechless kwakweli. Ngoja nikalale. kesho naweza amka na ushauri wa busara.
   
 5. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Ndg yangu
  kwanza mshukuru Mungu kwa kukuponya na janga hilo,kuna methali inayosema kuku akilala polini anageuka kwale.
  kitendo cha maambukizi hayo kina ashiria kuwa mwenzako hakuwa mwaminifu ktk ndoa. Ninajua ilivyo ngumu hasa jambo linapomtokea mtu wa karibu yako.Kwa mawazo yangu mimi ningekushauri ujitenge naye hasa kimahusiano ya kindoa japokuwa huzuiliwi kumsaidia kama ambavyo unaweza kumsaidia mtu yeyote.
  Hawezi kukulaumu kwani anajua hali harisi akikulaumu huyo hakupendi. Uwe mwangalifu (siku zote wema hauuwi bali huleta matatizo).
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  unfortunately hemed... hadithi yako inakosa consistency sana tu, sasa sijui n wewe, nyie au mimi

  Ili nisikuvunje moyo nakushauri ujiangalie wewe mwenyewe kam ni mzima kabisa na una akili sawasawa.... maana nahisi kama habari imechakachuka kidogo

  nashindwa kuelewa kama ni mkeo, nashindwa kuelewa kama alitaka kukuua ni kwanini unasikitika
  sielewi mtu mmehangaika ana kuwa pamoja na baada ya mwezi akaondoka tena
  mara akakataa kuondoa
  mara kaondoka tena
  mara wazazi walikata... halafu tena nimeongea na wazazi

  nahisi una matatizo makubwa wewe kama wewe... na yeye nadhani anajaribu kukuelewa lakini haiwezekani... saas kisa cha kuja kutuambia ana ukimwi nini?
   
 7. mbogodume

  mbogodume Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu mbona unamuita mke wakati ndoa ilishindikana, embu tuweke sawa ,kabla ya kukushauri.
   
 8. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  lol, kama ni mkeo piga ua mlikuwa mnadu bila ndomu, kama mliachana just for few months mama akarudi 'connected to the grid' inamaanisha hata wewe kaka upo njia panda.

  kuna mzee fulani alikua na ngoma. akasema kwamba mkewe amepima hana. baada ya miezi 6 mama alipima tena akakutwa na ngwengwe! kwahiyo mkuu....i feel sorry for you....so sorry....huyo mkeo alikuja kukumaliza tu...alikuja ku revenge'....:)
   
 9. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,512
  Likes Received: 2,103
  Trophy Points: 280
  CBZ huyo ni unyanyapaa, muombe radhi mshikaji for sure hutakiwi kumkatisha tamaa mtu kihivyo. Hili janga ni letu wote usimnyooshee kidole kimoja mtu wakati vinne vinarudi kwako
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu naomba sana ukapate elimu ya uzazi na jinsia

  jinsi ulivyoandika, inainekana upeo wako ni sawa na APPT maendeleo --- no offense, ntamuomba kamanda MJ1 akusaidie kukunahisi ili uelewe unayozungumzia
   
 11. T

  The King JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu amekuepusha na huu ugonjwa (kama utaendelea kuwa negative) na inabidi umshukuru sana. Kwa ushauri wangu pamoja na kuwa bado unampenda lakini inabidi ujiepushe naye sana hasa ukitilia maanani kwamba ameshakutamkia kwamba ni lazima akuue.
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  shemeji na wewe naomba upime mara tatu ili uwe na uhakika na afya yako .baada ya hapo chukua hatua sahihi ya kuachana nae kwani tayari ana kisasi cha kukuua na wewe ..
   
 13. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #13
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa kunishauri hivyo,ninajitahidi sana kujitenga nae lkn namba zangu za simu zote anazo sasa anachokifanya haipiti zaidi ya siku tatu aidha atanitumia sms za kunitukana ama atanipigia moja kwa moja na kuanza kunitukana mimi huwa simjibu na wala siwezi kuzima simu yangu kwa ajili yake!
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  Wala usihofu na matusi yake kwa njia ya simu na message ..siku zote debe tupu haliishi kuvuma cha msingi jaribu ku ignore ..then usisahau kupima zaidi ya mara tatu mpendwa .wish you good luck
   
 15. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #15
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafikiri labda ndugu yangu haujanielewa vizuri huyu mwanamke mimi nilimpenda na yeye alinipenda sasa hata mimi nilishangaa kuwa kwa nini hataki kutulia nyumbani wakati kila kitu namtimizia sasa yawezakuwa tayari pengine yeye alishapima kabla yangu na akakuta kuwa tayari ni mgonjwa na ndo maana hakuwa na amani nami,mimi tayari nimerudia kupima tarehe 9 Oktoba bado sina maambukizi
   
 16. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #16
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  FirstLady1 nashukuru kwa ushauri tayari nimesharudia mara yapili Oktoba 9-2010 na nitafanya hivyo kwa mara xa tatu Januari 9-2011 na nilipopima mara ya pili bado niko NEGATIVE niombeeni kwa Mungu mara ya tatu nibaki hivyo
   
 17. K

  Kasungura Member

  #17
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 12, 2007
  Messages: 72
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndugu, yote ni maisha.
  Kama mkeo anaumwa Ujue kuwa hata kisaikolojia atakuwa mgonjwa sana.
  Plz uwe makini kwa chochote unachotaka kumfanyia, kumjibu na nk.
  Nitumie PM ili tuwasiliane zaidi.
   
 18. O

  Optimistic Soul JF-Expert Member

  #18
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kaka pole sana, tungeweza kukushauri otherwise ili wewe na huyo mwenzio muishi kwa pamoja kwa furaha bila kuambukizana lakini inaonekana itakua suicidal (mhanga), kwa hiyo ni vyema tu ukajiepusha nae sio kwa kumnyanyapaa bali ni kwa kujihami wewe mwenyewe kwani kama ulivyosema bado unampenda sana anaweza kutumia udhaifu huo na akakuambukiza makusudi. narudia tena pole sana, ila unapoenda kupima jaribu pia kupata ushauri nasaha utakusaidia kisaikologia. God protect u.
   
 19. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #19
  Nov 2, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  yote ulioeleza, kama isingekuwa hapo kwenye RED.... ningekushauri umpende na umhimize kuwa kuwa na HIV si mwisho wa nyie kuwa na maisha mazuri... Ila kwa halihiyo na viapo..... nakushauri ukubali kuanza upya kusaka wa maisha... na mweleze mhusika nia hiyo.!!
   
 20. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #20
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninapata faraja kubwa kwa haya yote mnayonishauri,kumbe mtu ukiwa na tatizo uka-share na wenzako kwa namna moja unapata unafuu moyo unatulia na akili pia inatulia nawashukuru wote tena kwa moyo mmoja,ila kwa muda huu sina mpango wa kutafuta mwanamke wa kuoa ni mapema mno na nimepata funzo kuwa ndoa siyo jambo la kukurupuka!
   
Loading...