Mke wangu amezaa mtoto mzungu

Mke wangu amezaa mtoto mzungu

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Jamani jumatano majira ya saa tisa usiku mke wangu amejifungua.

Si masihala, amezaliwa mtoto mzungu kabisaaa ila amefanana kila kitu na mimi (copy kabisa).

Hii ni hali ya kawaida? Ukoo wetu hamna mzungu kabisa wala half cast. Nikifikiria naona kama nimeliwa hivi ila tatizo ni kwamba mtoto amefanana sana namimi kiukweli. Tayari nimeanza kuwa na wakati mgumu baadhi ya ndugu na marafiki kuongea maneno pembeni.

Naombeni mawazo ya kujenga jamani. Asanteni.
 
...kichwa maji,asa mawazo gani ?kwamba ni mzungu ?,sio mzungu ?,stori ya uongo ? au kuwa ni upuuzi...?! PUNDA wee ...!
 
Last edited by a moderator:
mzungu kamgida mkeo siku ya kutengeneza ngozi ya mtoto. Wewe mbegu zako zimetumika kwa sura ya baby wenu!! Teh Teh! chezea wanawake.
 
Imeshatokea baadhi ya waafrika, waliosikika mwisho miaka michache imepita ni wa Nigeria walizaa mtoto mzungu na ni wao.

Fanya DNA ujirizishe kuwa ni wako. Inatokea. Ungetafuta bbc/ccn utajipatia vihela kwa interview.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Maadam huyo ni mkeo then huyo ni mwanao!, acha mawazo potofu ya kibaguzi, njoo nikupe tuition, mbona hata mimi ni mweusi, na wife wangu wa US pia ni mweusi tii, ila tunakabinti keupe!,ni kabinti ketu na ninakapenda wala DNA sihitaji haswa kwa kuzingatia she lives huko, mimi naishi bongo, na bado ni binti yetu na ndoa iko imara!.
Pasco
 
Tulia Mkuu usikurupuke, kama angekuwa ni mtoto wa Mzungu basi asingefanana nawe hata chembe.
 
Mmmh, hapo sio bure, lazima kuna namna, by the way DNA test ndio jibu.


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Back
Top Bottom