Habari wana jf,
Sina budi kumshukuru alie juu kwa kuendelea kunipa pumzi ambayo mpaka
napata hata muda wa kuweza kuwatafuta wana familia ya jf, ili kupata
mawazo yenye hekima japo wapo wachache wenye akili kama kina Mwigulu ya
kuwaza kutengeza story za kusadikika kisha kuwafanya watu wapoteze muda
wao mwingi kwa jambo ambalo halipo.
Ni wiki sasa toka nimeleta uzi wangu hap jamvini kuomba ushauri juu ya
kisasi cha mke wangu niliemkamata aki du na shamba boy wetu, mlinipa
mawazo mengi sana juu ya nini nfanye baada ya kitendo hicho kichafu cha
mke wangu japo yeye alidai kua alikua analipa kisasi cha mimi kua na
mwanamke nje ya ndoa yetu takatifu na aligundua hilo baada ya mimi
kukosea msg ambayo nilikua naituma kwenda kwa nyumba ndogo badala yake
nikaituma kwa my wife, mlinipa mawazo mengi juu ya nini nifanye lakini
mwisho wa siku niliona hakuna maana ya kuendelea na ndoa ambayo dhahili
niliona imeshaingia dosali kubwa.
Niliamua kumwambia mke wangu kua sina shida tena ya kuendelea kua nayeye
mke wangu alinibembeleza sana ili nibadili msimamo wangu lakini haikua
rahisi kwakua tayari nilikua nimeamua hivo, basi ikabidi nimpeleke kwao,
niliporudi nyumbani kwangu nikapata taarifa kutoka kwa mamakwe kua mke
wangu kanywa sum baada ya kuona hakuna sababu ya yeye kuendelea kuishi
duniani bila mimi.
Hatua za awali walizo chukua baada ya tukio hilo nikumkimbiza hospitali
na mpaka sasa yupo hosipitali hali yake sio nzuri nifanye nini
nawakilisha nisaidieni mawazo wana jamii.
Naona wenye ushauri kuwa umrudie mkeo hawajawahi kuolewa na kama wameolewa waume zao ni Bushoke.Nakushauri mruhusu boy wako aende kumuona.Wewe endelea kumfungia vioo ili wengine wajifunze.uliona wapi mw'mke ana waume wawili?