Mke wangu amekunywa sumu,nifanye nini.

Mke wangu amekunywa sumu,nifanye nini.

Bahimba

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
510
Reaction score
346
Habari wana jf,

Sina budi kumshukuru alie juu kwa kuendelea kunipa pumzi ambayo mpaka napata hata muda wa kuweza kuwatafuta wana familia ya jf, ili kupata mawazo yenye hekima japo wapo wachache wenye akili kama kina Mwigulu ya kuwaza kutengeza story za kusadikika kisha kuwafanya watu wapoteze muda wao mwingi kwa jambo ambalo halipo.

Ni wiki sasa toka nimeleta uzi wangu hap jamvini kuomba ushauri juu ya kisasi cha mke wangu niliemkamata aki du na shamba boy wetu, mlinipa mawazo mengi sana juu ya nini nfanye baada ya kitendo hicho kichafu cha mke wangu japo yeye alidai kua alikua analipa kisasi cha mimi kua na mwanamke nje ya ndoa yetu takatifu na aligundua hilo baada ya mimi kukosea msg ambayo nilikua naituma kwenda kwa nyumba ndogo badala yake nikaituma kwa my wife, mlinipa mawazo mengi juu ya nini nifanye lakini mwisho wa siku niliona hakuna maana ya kuendelea na ndoa ambayo dhahili niliona imeshaingia dosali kubwa.

Niliamua kumwambia mke wangu kua sina shida tena ya kuendelea kua nayeye mke wangu alinibembeleza sana ili nibadili msimamo wangu lakini haikua rahisi kwakua tayari nilikua nimeamua hivo, basi ikabidi nimpeleke kwao, niliporudi nyumbani kwangu nikapata taarifa kutoka kwa mamakwe kua mke wangu kanywa sum baada ya kuona hakuna sababu ya yeye kuendelea kuishi duniani bila mimi.

Hatua za awali walizo chukua baada ya tukio hilo nikumkimbiza hospitali na mpaka sasa yupo hosipitali hali yake sio nzuri nifanye nini nawakilisha nisaidieni mawazo wana jamii.
 
Why ulichukua hatua ya kumuacha wakati nawe ulikuwa msaliti? Pole.. mhamishie hospital ya taifa.
 
Siku zote uamuzi wa mwisho kabisa upo moyoni mwako! Kama kuna msaada wa matibabu wanahitaji na unauwezo nao wasaidie, lakini suala la kumrudia au kumrudisha kwako usikilize zaidi moyo wako.
 
Mshahara wa dhambi ni mauti, ulifanya uzinzi mkeo akalipiza ukagoma kumsamehe akanywa sumu,ungetulia na mkeo bila kutafuta free v haya yote yasingetokea,so utajibeba mpenda chini wewe
 
Jamani kama ameshapelekwa hosptal unataka ufanye nini? Subir mkeo apone ndipo uanze kusema ufanye nini. Vingnevyo ni kufanya mchezo wa maigizo katika maisha.
 
Sasa baada ya kumshauri mnamnanga! Nenda mwaya kasaidiane na mamamkwe kumtibia ni wazi kuwa akikuona atapata faraja

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wewe ndio chanzo cha yote. Na utalaanika,
Yeye alikusamehe hakudai talaka alipojua una mwanamke mwingine nje.
Lazima usamehe ili mungu akusamehe makosa yako.
Kama hauwezi kusamehe basi hausameheki pia.
Na akifa mzimu wake utakutesa daima kama ni hukumu yako duniani,
Jua tu ndoa yenu imevamiwa na shetani, shetani ambae atakuangamiza wewe hapa duniani.
Mwisho unakuwa chizi, ni bora kumsamehe tu na tafuta padri au shehe akuombeni akusomeni dua.
Hamna ndoa hisio na dosari, wanawake wengine wanafikia kuzaa nje ya ndoa, mwanamme anakausha tu.
Maisha ni kukabiliana, ukilikoroga mwenzio analilipua, tuliza akili omba mungu amponje umsamehe
 
Kama nyie ni Wakristo tafuta laki na nusu na kama ni waislam tafuta elfu 35 halafu mPM Mwana Mtoka Pabaya. Utahitaji aidha JENEZA au MKEKA na sio ushauri.

Huyo hawara yako hajanywa sumu sababu ya kuachwa na wewe, kanywa sumu sababu umemharibia dili lake la kugegedwa na cattle boy wenu.

solid_cambridge_oak.jpg

Hili ukilipa 180,000 nadeliver popote hapa dar.

Willow-eco-coffin.jpg

Hii culture, haipo kwenye stock lakini ukitoa oda nadeliver kwa siku 3. Bei yake 390,000

coffin-rockingham-zoom.jpg

Hili nalo 180,000. Mninga huo usidhani varnish babu, kitu quality na hizo handle ni za Italy

Iko mipodo na mkangazi kama huna fedha ya kutosha lkn. Kuanzia 120,000 hadi 90,000 unapata. Tunalipolish vizuri tu wala mtu hatojua sio mbao ngumu. Mpende mkeo babu

mat1.jpg

Huu ukitaka tunakuandikia jina na ayat unayotaka, kama ya kumuombea dua hivi. 45,000

table-mats-and-runner.jpg


Hii bidhaa ya Uturuki. 60,000 zipo rangi nyingi tu

Kama vipi niPM nikupe catalog, tuna bidhaa nyingi tu kaka. Na incase na wewe upendo ukakuzidi na wewe ukaona huwezi kuishi bila wife wako uka-opt kumfuata, I will serve you better Sir!

100114181037_hanging-rope226.jpg

Hiyo ni just 25,000 ila ukitaka na aluminium tripod nitakufanyia 100,000. Haiachi wrinkles usoni hiyo, unatabasamu to the last minute.
 
kuna wale watu ambao wananifanya niwaze "Hivi na huyu kwa nini nae alioa?" ..mmoja wapo ni wewe
 
Haifai kulipiza kisasi lakini kwa vile imetokea na tayari mkeo kanywa sumu na wewe kunywa sumu ili kulipiza kisasi.
 
Mshahara wa dhambi ni mauti, ulifanya uzinzi mkeo akalipiza ukagoma kumsamehe akanywa sumu,ungetulia na mkeo bila kutafuta free v haya yote yasingetokea,so utajibeba mpenda chini wewe
jamani jamani!!... mpenda chini tena!!!
 
pole sana. Lakini mbona hukujiuliza yeye alivyogundua mahusiano yako ya nje mbona hakukuacha?? au unadhani wewe kutembea nje ya ndoa yako ni sahihi lakini yeye akifanya hivyo ndoa imeingia dosari???
 
Back
Top Bottom