Behind the camera
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 315
- 757
Nikiwa ni mwanandoa miaka minne sasa namshukuru Mungu kwa hili.
Ila katika tasnia hii ziko tabia ambazo zinavumilika na nyingine ngumu kuvumilika. (Hutofautiana mtu na mtu)
Ziko tabia za kurithi, kuiga na za kwako mwenyewe.
Upande wa ndoa ya wakwe zangu, Ni mtihani mkubwa sana kwani yule mama (mkwe) ana tabia ambazo sijazipenda. (Mimi Kama Mimi)
Nimekusudia kabisa kama mkewangu ikitokea amekuwa kama mama yake... Kwakweli sitoweza vumilia.
Hizi ni baadhi ya tabia
1. MATUSI
Ebwanaee,,,, yule mama anatukana jaman, sikuwa najua kumbe Kuna watu wana kipaji cha kutukana. Akiamua kuyaporomosha kwakweli hata watu wa Mtaa wa 4 watazima redio na kusikiliza zile cheche.
2. UGOMVI
Mama mkwe wangu Ni ngumi jiwe, mda wowote kinanuka na mtu anavimba.
3. UCHAWI
Hili nahisi ni kubwa zaidi.
Huyu mama amerithi toka kwa mama yake (Bibi wa mkewangu) huyo bibi bado yu hai na Ni MCHAWI wa dhahiri kabisa.. hata ndugu zake humkimbia.
Sasa mama amesharithi mavitu Yale. Na inasemekana mzee ameshikwa. (Kimadawa)
4. UCHOYO
Chake Ni chake lakini chako Ni chenu
(Nadhani nimeeleweka)
5. WIVU WA KITOTO
Huyu mama akimkuta mumewe amesimama na mwanamke yeyote yule gubu linaanzia hapo. Na maneno machafu kwa huyo mwanamke kuwa muache mume wangu. Wacha waume za watu sijui Nini na Nini... Mambo kibaaaaao.
NB
Mama wa mwenzio Ni sawa na mama yako, lakini kwa tabia hizi nimekuwa si mwenye kupenda kwenda ukweni. Na ukizingatia tunaishi mikoa mbali mbali kidogo imenisaidia.
Laa sivyo nami yangeshanikuta na ningeshaachia ngazi.
Nimeshamgusua mke wangu kuwa "Kuwa makini usije ukawa kama bimkubwa bwana, mimi sitoweza kuvumilia Mambo yale"
Atajua mwenyewe kama kamwambia au kaamua kupitezea, ila mi ujumbe umefika.
HAKIKA
Mke wangu akirithi tabia hizi, KAMWE sitoweza kuwa naye tena.