Baba_Enock
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 7,076
- 2,465
Hapa naongelea wanaume wanaofanya maamuzi ya kuachana na wake zao na kuoa mke mwingine au wake wengine - kutokana na sababu wanazozijua wao. Kwa waliofiwa na wake zao - poleni sana - hii mada haiwahusu au kama itawagusa - samahani sana...
Baada ya kufatilia kwa takribani miaka 40 - ndiyo arobaini na ushee - nimeonelea kuwa wanaume wengi ambao wameoa mara ya pili au zaidi wamekubwa na misukasuko mingi ya kimaisha kuliko wale ambao wamekuwa kwenye mahusiano ya ndoa na mke mmoja tu. Wanaume wengi ambao wameo mara ya pili au zaidi "wameharibikiwa" sana katika maisha katika njia nyingi mbalimbali....
Ninayo mifano zaidi ya 50 ya wanaume ambao "wameoa tena" na uzee wao umeishia pabaya sana ... Wengi wamegeuka kuwa ombaomba na masikini wa kutupwa pamoja na kwamba kabla ya "kuoa tena" walikuwa na maisha mazuri ya wastani au ya juu...
Ninapenda kuuliza, "kuoa tena" ni kujongezea mabalaa au ni changamoto za maisha...
Note: Wale ambao wanweza kuoa zaidi ya mwanamke mmoja kuishi nao hamuhusiki hapa...
I beg to differ,..hebu kwanza tuambie huo utafiti wako wa zaidi ya miaka 40 umetumia vigezo vipi na samplie size yako tujuze,...mambo ya kuharibikiwa ama kutokuharibikiwa inachangiwa na mambo mengi _mengi...mbona mzee Mandela maisha yake yamenyooka,..na wengine wengi ninaowafahamu ingawa nikiwataja hapa hautawajua.....
@Ashadii: Kuoa mke wa pili mambo yakanyooka siyo sustainable - onaweza ikawa miaka mitano lakini haitazidi kumi - unakuta mwanaume amerudi mpaka kuwa mdoeaji wa Bia. Ukifuatilia sana unaambiwa huyu aliachana na mke akaoa mke wa pili akajenga maghorofa, akanunua magari, lakini baada ya muda mambo yakaanza kuharibika...
Mke wa pili anaweza akakunyanyua lakini utabakia hapo lazima utarudi chini kwa kasi ya ajabu... Kaa chini piga hesabu ya "matajiri" unaowafahamu ambao wanaweza kuwa kwenye miaka ya sitini au zaidi kidogo - waliosimama mpaka sasa ukifuatilia sana lazima utakuta ni wale wenye ndoa ambazo "hawakuoa tena"!
Narudia tena sio kwamba na Support but tuangalie logic;
Swali....
- Wangapi pia wameoa wana Mke mmoja na bado maisha ni mabaya or just Sustainable??
- Wangapi wameoa wana Mke mmoja but ana vimada kumi kidogo?? What's the difference??
Utafiti huu unafika hadi kwa mahawara aka smoli hauses?
Kama nakubaliana na wewe vileee.....................ngoja niangalie kwanza ndoa nazozifahamu za wababa wazeezee hivi halafu nitakuja kuchangia tena
yeah - 50+ and 60+ unakuta ameachana na mke halafu anaoa binti wa 30+! Mwisho wa siku yeye ndiye anakuwa mfungua geti na mwosha vyombo...
nimekusoma uzuri, kwa hiyo wake wawili au zaidi ni problem, that is what you concluded, from your vivid example that is.huo msemo sina uhakika nao,kwa mifano yangu mimi,wapo waliooa mke wa 2,maisha yakawaendea vyema kuliko mwanzo,na wapo waliooa mke wa 2,maisha yakawaendea vibaya.kwa hiyo ni mchanganyiko.na huku niliko,talaka kila kukicha na kama sio talaka basi watu wanaongeza wake wa 2,na wengi waliofanya hivyo,kimaisha sijawaona kutatareka,wengi ni hard work na maisha yao ni mazuri tu.ila kwa mfano wangu wa karibu,my father aliongeza mke na akatutelekeza kabisa,mama yetu alikuwa single mum kwa miaka yake karibu yote.kwa sasa baba yupoyupo tu,na huyo mke wake,yeye ana kipato kizuri kabisa,hataki kumuona baba tena.na kwa upande wa mama yetu,mambo yake sio mabaya.