Mke wa Nyalandu asema mumewe hakutaka kutoroka nchini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema, Lazaro Nyalandu amezuiwa Namanga kwasababu hakuwa na nyaraka muhimu na atafikishwa Mahakamani endapo atashindwa kuwasilisha nyaraka hizo.

Mke wa Lazaro Nyalandu, Faraja Kotta Nyalandu amesema wao wanaishi Arusha na mumewe hahitaji nyaraka ili kufanya shughuli zake akiwa upande wa Tanzania na wala hakuwa na mpango wa kuvuka mpaka wa nchi.

Pia amesema tukio hilo halikutokea Novemba 9, kama ilivyoripotiwa bali lilitokea Novemba 6.

Lazaro Nyalandu alikuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia CHADEMA. Iliripotiwa kuwa anashikiliwa na Maafisa Uhamiaji wa Tanzania kwa tuhuma za kutaka kuondoka nchini bila nyaraka muhimu.

Faraja.JPG
 
Hii maana yake nini?!

1. Polisi ndio waongo?

au

2. Mke wa Nyalandu ndie muongo?

Ila kwa muunganiko wa matukio, naanza kuamini mke wa Nyalandu ndie mkweli, kwasababu mtu kama Nyalandu siamini kama hajui taratibu za kusafiri nje ya nchi mpaka aache documents muhimu.

Alikuwa na safari zake maeneo ya mpakani, polisi kwa kutojiamini hasa kutokana na lile tukio lililotangulia la Lema, wakaona wamkamate, kumbe hata hakuwa na mpango wa kusafiri nje.

Nilijiuliza inakuaje mtu anaetaka kukimbilia nje atumie private car yake? kumbe alikuwa na mishe zake tu.
 
Hii nchi ukitaka kwenda nje tu, unataka kutoroka. Tulipofikia ni pabaya sana. Tuheshimu katiba yetu.

Uhuru, uhuru, uhuru.

Kastukiwa huyo, wanaacha nyaraka halali ili wakaombe hifadhi ya ukimbizi. Serikali ya Tanzania inashindwa kumtimua balozi wa Ujeremani akawa kielelezo cha msimamo wetu kama Taifa. Kwa nini hawa wanaachwa watuchezee hivi?
 
Tunasubiria episode ya nne ya bwana mashavu Boniface Jacob, sijui yeye atatokea border gani na igizo jipya la Chadema
Nyalandu kuwa salama haina maana na wengine wapo salama pia, tumia akili kidogo; kama kuna huo usalama mbona Lissu anaishi ubalozini?!
 
Kastukiwa huyo, wanaacha nyaraka halali ili wakaombe hifadhi ya ukimbizi. Serikali ya Tanzania inashindwa kumtimua balozi wa Ujeremani akawa kielelezo cha msimamo wetu kama Taifa. Kwa nini hawa wanaachwa watuchezee hivi?
Kwa jinsi ulivyoandika, nina imani utakuwa uliishia darasa la Nne B.

Kama vipi washauri wenzio kesho muandamane muishinikize serikali imfukuze Balozi basi...
 
Kwa jinsi ulivyoandika, nina imani utakuwa uliishia darasa la Nne B.

Kama vipi washauri wenzio kesho muandamane muishinikize serikali imfukuze Balozi basi...

Kwani Lissu akijifungia ubalozini Tz inaathirika vipi, acha akae humo ndani hadi January akitoka train za SGR zitakuwa zimefika 😂.
Au Lissu akikaa ndani ubalozini ndio fanatics wake watagoma, hizi strategy na mipango ya Twitter na JF ni ya kitoto na kipuuzi, hata hao mabalozi watakuwa wanamdharau Lissu saivi.
 
Kastukiwa huyo, wanaacha nyaraka halali ili wakaombe hifadhi ya ukimbizi. Serikali ya Tanzania inashindwa kumtimua balozi wa Ujeremani akawa kielelezo cha msimamo wetu kama Taifa. Kwa nini hawa wanaachwa watuchezee hivi?
Thubutu yake! Magufuli hana ubavu huo hata kichaa chake kinapata ufahamu!
 
Kwani Lissu akijifungia ubalozini Tz inaathirika vipi, acha akae humo ndani hadi January akitoka train za SGR zitakuwa zimefika 😂.
Au Lissu akikaa ndani ubalozini ndio fanatics wake watagoma, hizi strategy na mipango ya Twitter na JF ni ya kitoto na kipuuzi, hata hao mabalozi watakuwa wanamdharau Lissu saivi.
Unajidharauzisha mwenyewe kwa pumba unazomwaga hapa?
 
Unajidharauzisha mwenyewe kwa pumba unazomwaga hapa?
Vipi Mbowe anaenda ubalozi gani ? Au na yeye ataibukia Kenya, mna drama kama ma slay queen vile 😂...
Mkianzisha CDM reality TV show mtapata pesa nzuri zaidi hata ya ruzuku, maana mpo vizuri kwenye maigizo.
 
Back
Top Bottom