Mke wa mtu huyu

Mke wa mtu ambaye amezaa watoto wawili na huyo mume wake na anapete ya ndoa na uchumba.
Sasa kama unamzunguamzia huyo sawa... WENGINE HAWAPO HIVYO... We mtu umekutananaye njiani akiwa anaruka njia au umemuowa baada ya kumpokonya mwenzio hapo unategemea nini?
 
Nadhani ushauri angeomba kabla ya kuanza kulala na mke wa mtu, manake mke wa mtu si sumu akiwa bagamoyo tu hata mjini wanakofanyia maovu hayo kila siku. Anajua jema na baya,anajua yanayoweza kumpata. Ushauri ni kuwa atafute mke wake au mwanamke asiye na commitment ajenge uhusiano na sio kuharibu ya wenzie.
 
Mkuu naona umeamua kuchukua tahadhari kuogopa mchango wa matusi na kejeli mapema, hongera.

Kwa upande wangu hata kama nitakuwa nafanya uzinifu na mwanamke yeyote yule yaani a single lady or married one hakika nitakuwa wa mwisho kumshauri mtu yeyote kutenda kama ninavyofanya, zinaa ni dhambi kubwa na mbaya zaidi na mke wa mtu jamani haikubaliki hata kidogo.

Matatizo kwenye ndoa yapo mengi kama uliyoyataja ya huyo dada na mume wake, lakini bado sio sababu ya msingi kwa mmoja wa wanandoa kumsaliti mwenzake. Jamani maadamu tatizo limetokea wakati ndoa ilikwisha fungwa tena yenye watoto wawili, kumbe jambo la msingi kwa huyo mama ilikuwa kumsaidia huyu mwenzake aondokane na matatizo yanayomkabili kwa sasa ili apate tiba na kurudi katika hari yake ya kawaida na waendelee kutenda kadri ya Mapenzi ya Mungu (tendo la ndoa ndani ya ndoa ambalo kwao ni takatifu). Huyu mama (maharage ya mbeya) amefanya kosa kuisailiti ndoa yake ambayo aliapa kuilinda katika shida na raha, arudi nyuma na kumsaidia mwenzake.

Na huyu kijana hakika amepotea pakubwa, anapoteza muda kwa kuwa na mahusiano na mke wa mtu, zinaa yoyote ni dhambi lakini angelikuwa anafanya na binti (single) tungesema ipo siku watatubu hiyo dhambi na kuingia kwenye ndoa takatifu na kuanza maisha yao yenye kumpendeza Mungu na jamii kwa ujumla. Mwambie aache, anapoteza muda wake, anakuza familia ya mtu mwingine, atakumbuka shuka kumekucha, atasahau hata kuoa aliye wake, ipo siku ataazibiwa vibaya sana hapa hapa duniani.

Na kwa huyu kiunganishi wao sio mzuri hata kidogo, anafanya biashara haramu ya kuuza mke wa mtu, anachangia kuvunja ndoa ya mtu ilihari yeye anaendelea na ndoa yake, haikubaliki hata kidogo. Ndoa na iheshiwe na watu wote jamani, na kwenye ndoa sio tendo la ndoa tu (ngono).

Pole, ila mwambie aache kwa manufaa yake binafsi na familia yake
 
kwani haoni huyo dada yeye ana familia yake!!!!!,hafikirii future yake huyooo.......mwambie atafute mchumba aoe,,, ale kwa raha zake..
 
aliyemshauri kumpigia simu na kumtongoza huyo mdada ndio anapaswa kuendelea kumshauri hadi sasa.maana yaonekana akili zao zinarandana.
 
WA KISHUA mpelekee huyo rafiki yako huu ujumbe, aache kucheza na Mungu, Mungu ameshampa nafasi ya kutosha ya kujutia makosa yake, mwambie atubu vinginevyo hiyo safari ya Bagamoyo ndiyo mwisho wake. Nakuambia haya nikiwa na imani kubwa na amri ya Mungu dhidi ya zinaa na uzinifu
 
Dah, wengine bado tunaishi zama za mawe. Hivi imefika mahali hayo mambo yamerahisishwa hivyo?
Hamjuani, hamjawahi kukutana, mtu unaunganishiwa tu na unaelezwa kuwa ni mke wa mtu na siku hiyo hiyo unajiachia!

Ndio maana nikaleta huu UZI hapa ili mawazo yenu yenye BUSARA na HEKIMA kisha niyawaclishe kwa huyu MUHANGA wa hili tukio. Ty for ur cooperation Wimana
 
hakuna cha rafiki yake wala nini niyeye mwenyewe matusi na kejeli ayakubali tu WA KISHUA kwani hauna akili timamu ya kuwaza jema na baya

Huu MKASA sio wangu naomba nieleweke ivyo, huyu MUHANGA ambaye ni friend yngu hayupo JF kwaiyo nikaona ili nipate MAWAZO mengine ukitoa yangu niulete huu UZI hapa., kila kilicho na ROHO kina mapungufu tyr na fahamu kwamba kukosea ni sehemu mojawapo ya kujifunza...
 
Nadhani ushauri angeomba kabla ya kuanza kulala na mke wa mtu, manake mke wa mtu si sumu akiwa bagamoyo tu hata mjini wanakofanyia maovu hayo kila siku. Anajua jema na baya,anajua yanayoweza kumpata. Ushauri ni kuwa atafute mke wake au mwanamke asiye na commitment ajenge uhusiano na sio kuharibu ya wenzie.

I buy ur Ideal Michelle ila fahamu kwamba KOSA haliitwi KOSA mpk pale linapokamilika kuwa KOSA, kwaiyo jamaa wkt anafanya madudu na mke wa m2 alijua yuko sawa ila baada ya kukaa chini kutafakari na kuona roho inamsuta ndio akaja kwangu kunipa Movie kamili kisha mimi nikaona ni vyema niilete hapa kwa w2 wenye Fikra Pana waweze kutoa michango yao kwa namna moja au nyingine. Hope umenielewa...THnks kwa mchango wko mayne..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom