cheeter
JF-Expert Member
- Apr 19, 2011
- 475
- 155
Habari zenu humu ndani,bila shaka wote humu wazima.Mimi ni kijana mwenye umri 36,ni mfanyakazi wa taasisi ya uma.Ndoa yangu ilinishinda muda mrefu sana kutokana na makwazo ya wanawake zetu.nilishindwa kuvumilia na nikaachana na mke wangu.Hivyobasi katika kuishi maisha ya u bachelor nikiwa kazini nikawa karibu sana na mdada ambaye alikua ananielezea shida anazozipata kwenye ndoa yake.Mwisho wa siku nilimfariji na tukawa marafiki wakubwa mpaka leo natoka naye.Ananipenda kupita maelezo.na mimi kwa kweli nampenda jinsi anavyo care.ameniahidi yuko tayari aachane na mme wake ili tuishi wote.naombeni ushauri wenu wadau,nifanyaje ili niishi na huyu mke wa mtu.