Mke wa mtu aning’ang’ania

Mke wa mtu aning’ang’ania

Kijana wa miaka 36 halaf huna akili kiasi hicho? Ni akili hizo hizo ndogo ndio zimekufanya ukaishindwa ndoa na bila aibu tena unataka kuvunja ndoa ya mtu asiyekuwa na hatia eti kwa kisingizio mke wa mtu anakupenda na wewe unampenda.
Baada ya kufanikiwa kuvunja hiyo ndoa ya mwenzako utapata adhabu hutaisahau mpaka unaingia kaburini, malipo ni hapa hapa. Na kama utazinduka kiakili kimbia hiyo kitu tafuta wanawake waliokwisha achika tena sio kwasababu yako.

naomba uelewe mm sijavunja ndoa ya watu.na matatzo walionayo kwenye ndoa yao na mmewe mm hayaniusu.mm nampa faraja ya kutosha.na nipo upande wake na si vinginevyo
 
hahahaah, ukiona ivyo unanyota ya kupakuliwa kisamvu , we endelea nae tu badobado
 
Habari zenu humu ndani,bila shaka wote humu wazima.Mimi ni kijana mwenye umri 36,ni mfanyakazi wa taasisi ya uma.Ndoa yangu ilinishinda muda mrefu sana kutokana na makwazo ya wanawake zetu.nilishindwa kuvumilia na nikaachana na mke wangu.Hivyobasi katika kuishi maisha ya u bachelor nikiwa kazini nikawa karibu sana na mdada ambaye alikua ananielezea shida anazozipata kwenye ndoa yake.Mwisho wa siku nilimfariji na tukawa marafiki wakubwa mpaka leo natoka naye.Ananipenda kupita maelezo.na mimi kwa kweli nampenda jinsi anavyo care.ameniahidi yuko tayari aachane na mme wake ili tuishi wote.naombeni ushauri wenu wadau,nifanyaje ili niishi na huyu mke wa mtu.
Ingekuwa ni wew mimi namfanyia hivyo mkeo ungefanyaje....mwache na awe rafiki yako acha tamaaa utaumiza familia isiyo na hatiaa
 
Back
Top Bottom