Jamani hii sio hadithi ni ukweli yamenikuta.
Huyu mdada sasa mama nitaeleza Historia yake ili muelewe, mimi na yeye tulisoma Primary tukiwa darasa la sita nikamtongoza akanikatalia mimi nikawa mpole, wakati wetu darasa la sita miaka 18, baada ya muda akapata mimba na shule akaacha akataka nimuoe mimi nikamkataa kwa siri bila kumwambia basi shule ilipoisha tulitawanyika na mihangaiko ya maisha hatujakutana tena mimi nikaenda sekondari mpaka elimu ya juu.
Hapa majuzi akapata Namba yangu akanipigia akasema ameolewa yupo Arusha nikampongeza akasema, niende Nyumbani halafu akasema useme mimi ni kaka yake kwa mumewe siku nyingine akapiga simu tukaongea na mumewe safi tu ila siku moja mwaka juzi nilikuwa Arusha kikazi siku ya krismas nilienda kanisani kwao kusali basi tukasalimiana pale mumewe akijua mimi ni kaka yake basi tukaagana.
Tatizo likaja mumewe alisafiri akapiga Simu usiku sana kanitamkia kabisa anataka nifanye mpango niwe naye mapenzi yake kwangu bado yanamsumbua angalau tufanye mapenzi.
Mimi nimekataa ila ananisumbua sana.