Jamani nachokiona hapo ni kutaka sifa,haya na huyo Mwakasege anaposema yeye ndo aliwashauri kuwa wakatembelee Israeli alikua na maana gani? Na hao maaskofu wanasema watu siku hizi wanasulubiana pia ana maana gani?Kwamba EL hakutendewa haki au? Nijuavyo aliyoyapata anastahili,na wala hakusulubiwa na mtu ni yeye mwenyewe aliyoyafanya ndo yalomsulubisha alijitundika mwenyewe,kingine nachokiona hapo ni kama vile kupigana vijembe kwa sababu anaposema watu wanasulubishana ina maana kuna watu fulani hapo wanasemwa ki-aina fulani,na huo ni usengenyaji kwa nini usimfate mtu live na kumwambia kuwa wewe acha kusulubisha wenzako kuliko kuanza kurusha maneno kwenye zinduzi kama hizo,Swali,walienda kuzindua kitabu au ndo walipata sehemu ya kutoa madukuduku yao?
Natatizika na kauli zao.
Ni mtizamo wako. Tukifikia hapo pa kutohoji lolote wafanyalo kwa kuwa tu wao ni viongozi wa dini, basi hata uumbaji aliyoifanya Mungu utakuwa hauna maana. Yafaa nini basi kujitofautisha na ng'ombe au hayawani mwingine?
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo, alisema.
.
Mhubiri maarufu mwenye makazi yake mjini Arusha, Christopher Mwakasege, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, alisema ni yeye aliyetoa wazo kwa Lowassa na mkewe kutembelea Israel baada ya matatizo yaliyowakuta.
COLOR]
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, aliwahimiza watu kujenga moyo wa kupendana ili kujenga nchi yenye maelewano.
Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.
Mungu wangu siamini ninayoyasoma...Mke wa Lowassa azindua kitabu
Na Mwandishi Wetu,
MTANZANIA, Aprili 15, 2009.
Watu mbali mbali jana jioni walimiminika nyumbani kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kushuhudia uzinduzi wa kitabu kilichotungwa na mkewe Regina, uliofanywa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Regina aliandika kitabu hicho wakati akiwa katika matembezi binafsi inchini Israel, siku chache baada ya mumewe kujiuzulu uwaziri mkuu Februari mwaka jana kutokana na sakata la Richmond.
Kitabu hicho kilichoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kiitwacho Walk The Path With Diary in Israel, The Holy Land kina kurasa 15 na dibaji yake imeandikwa na Monsinyori Julian Kangalawe kutoka Kanisa la Mtakatifu Joseph la Dar es Salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo, alisema.
Mhubiri maarufu mwenye makazi yake mjini Arusha, Christopher Mwakasege, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, alisema ni yeye aliyetoa wazo kwa Lowassa na mkewe kutembelea Israel baada ya matatizo yaliyowakuta.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, aliwahimiza watu kujenga moyo wa kupendana ili kujenga nchi yenye maelewano.
Mbali na Mlasasusa, Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ni Pwani, Elinaza Sendoro, pia alihudhuria hafla hiyo, na akatumia nafasi hiyo kuwashawishi watu kutembelea Israel kujionea namna watu wa dini tofauti wanavyoishi.
Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.
katika ziara hiyo walitumia pesa zipi?
Mkuu Dr na post zako zaidi ya 2000 JF una vitabu zaidi ya 80Mazee hiyo hata sio booklet hio ni handout tu.