Mke wa Bilionea Msuya ataka tume ya uchunguzi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Dar es Salaam. Mke wa marehemu bilionea, Erasto Msuya, Miriam Mrita ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuunda tume kuichunguza kwa kina kesi ya mauaji inayomkabili akidai kuna uonevu unaoendelea.

pic+msuya.jpg

Miriam amewasilisha ombi hilo leo Juni 4 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba mara baada ya wakili wa serikali, Patrick Mwita kuiambia mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, lakini jalada halisi lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kuomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.

Baada ya Mwita kueleza hayo, Miriam alinyoosha mkono ambapo hakimu Simba alimruhusu kuongea.

Miriam alisimama na kuiambia mahakama kuwa huu ni mwaka wa pili sasa wanaendelea kusota mahabusu.

"Mimi ni mama mjane, mume wangu ameuawa, mimi nipo mahabusu gerezani kwa miaka miwili, kama mama sijui watoto wangu wanaendeĺeaje huko nje." Ameongea Miriam.

Ameongeza kuwa amechoshwa na wimbo wa upande wa mashtaka kuwa upelelezi bado haujakamilika.

"Mtu ukishafiwa na mume kuna vurugu mechi zinaendelea huko nje, naomba iundwe tume ya uchunguzi wa kina ya kuichunguza kesi hii kwa sababu kuna uonevu ambao unaendelea."Ameeleza Mrita.

Amebainisha mahakamani hapo kuwa kesi yake ipo kifamilia zaidi na kuomba iangaliwe zaidi na kwamba watagundua mambo mengi zaidi.

Anadaiwa kumuua kwa makusudi dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Anathe Msuya Mei 25, 2016 huko Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.



Chanzo: Mwananchi
 
Hii kesi ya mauaji ina mambo mengi sana inaweza kusababisha hata mauaji mengine
 
Yule Dada aliuawa kinyama sana aisee ingawaje inatakiwa uchunguzi wa kina kujua wahusika ila Bongo kwenye kesi za mauaji wapo makini sana wanajitahidi kwenye upelelezi...
 
Kesi za mauaji bongo kama haukuwa red-handed uchunguzi wake MANJEGEKA sana.......Wafanye uchunguzi haraka maana mda umepita zaidi ya miaka miwili unachunguza nini? Kesi kama hizo ndani ya miezi miwili ushamaliza kazi kama kahusika unampa mva zake za maisha au kunyongwa biashara inaisha mnafanya mambo mengine.
 
Updates:

Mke wa marehemu Bilionea Msuya Bi. Miriam Mrita Leo Amekiri mbele ya Mahakama kupanga njama za kumuua Wifi yake (mdogo wa Bilionea Msuya) Marehemu Aneth Msuya....Jela imemuaita kaitika...Life sentence in jail is coming to her!!
 
Mwanamke ana roho mbaya sana huyu, kukiri kumuua wifi yake napata shaka hata kuuwawa kwa mumewe anaweza kuwa alishiriki, aliuwawa kinyama sana Aneth,,dah! Mungu wape faraja na nguvu wazazi wa Aneth.
 
Back
Top Bottom