Mke mwema: Tunamsubiria au tunamtafuta

Mke mwema: Tunamsubiria au tunamtafuta

Lucky One

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2013
Posts
663
Reaction score
431
Habarini za asubuhi wanajamvi,

Natumaini mmeamka vyema katika siku hii.

Kama kichwa cha habari kilivyo ni kwamba nimekuwa nipo katika mtanziko kuelewa kuwa mke mwema mtu humsubiria tu bila kuhangaika au inambidi mtu atafute mwenyewe.

1. Mke mwema huja kwa kumsubiria tu bila kuhangaika
Katika dhana hii kwa wakristo, watu husema inambidi mtu atulie tu maana Mungu kwa wakati wake atampatia mke mwema. Hoja kubwa hapa ni kwamba Adamu binadamu wa kwanza alilala tu kisha Mungu akampatia mwanamke na alipomuona akasema huyu ni nyama ya nyama yangu na mifupa ya mifupa yangu. Hivyo katika muktadha huu watu husema mtu hatakiwi kuhangaika kutafuta mke bali Mungu kwa wakati wake atampatia mtu mke mwema.

2.Mke mwema huja kwa bidii ya kutafuta
Hapa watu husema mke mwema hupatikana kwa bidii ya mtu mwenyewe kutafuta. Hivyo mtu anatakiwa ajue jinsi ya kumshawishi mtu awe mke wake katika hili watu hupinga kwamba kuna mke ambaye mtu humsubiria bali mtu mwenyewe anatakiwa afanye jitihada.Kulingana na maelezo haya nilikuwa naomba kusikia kutoka kwa wanandoa au watu ambao washapata wenzi na wanamatarajio ya ndoa,je mlifanya jitihada za kutafuta au mlisubiria tu?

Karibuni kwa michango.
 
Kwa reference ya maandiko ya biblia, mke mwema anatafutwa lakini mume mwema anasubiriwa.
Refer rebeca na isaka, mtu alitumwa kumfuatia isaka mke na rebeca alikutwa katika harakati zake ila wema wake na tabia ya ukarimu ndio iliyomthibitishia yule mtu anayemtafuta mke wa isaka na kumbe ni wa nyumba aliyoagizwa aende.
 
Kwa reference ya maandiko ya biblia, mke mwema anatafutwa lakini mume mwema anasubiriwa. Refer rebeca na isaka, mtu alitumwa kumfuatia isaka mke na rebeca alikutwa katika harakati zake ila wema wake na tabia ya ukarimu ndio iliyomthibitishia yule mtu anayemtafuta mke wa isaka na kumbe ni wa nyumba aliyoagizwa aende.
Ndio, mwenyewe huelewa hivyo ila kuna mchungaji katoa somo eti wanaume hatuna haja ya kutafuta bali Mungu kwa wakati wake atatupatia tena anadai ukikutana naye tu utamwona tofauti na moyo utakutuma kuwa ndiye. Sasa hapa nabaki njia panda...
 
Uelewa unatofautiana hapo, utakutana nae vipi bila kutoka nyumbani kwako. Nadhani alimaanisha usiwe in panic mood kwamba lazima umpate mda flan n.k yaani u relax ili ukikutana nae umtambue
 
Uelewa unatofautiana hapo, utakutana nae vipi bila kutoka nyumbani kwako. Nadhani alimaanisha usiwe in panic mood kwamba lazima umpate mda flan n.k yaani u relax ili ukikutana nae umtambue
Yawezekana ila alichomaanisha yeye ni kuwa yule asubiriaye ni yule ambaye anampata kwa tukio flani la bahati yaani bila kutarajia.....wakati yule wa kutafuta ni yule anayehangaika kutafuta yaani leo huku kesho kule akisaka.sasa je kati ya hawa nani anampata mke mwema???
 
Wakati unasubiria hilo zali, shetani naye anapiga misheni zake akuletee vyake fake au amchengeshe asikufikie. Kusubiri ina maana pana sio tu unakaa huombi huchukui hatua yoyote.
 
Wakati unasubiria hilo zali, shetani naye anapiga misheni zake akuletee vyake fake au amchengeshe asikufikie. Kusubiri ina maana pana sio tu unakaa huombi huchukui hatua yoyote.
Yah,.. kweli kusubiri inahitaji imani sana hivyo maombi yatahusika sana ila kwa wengi wetu ndo hivyo kutafuta muhimu sana....
 
Yawezekana ila alichomaanisha yeye ni kuwa yule asubiriaye ni yule ambaye anampata kwa tukio flani la bahati yaani bila kutarajia.....wakati yule wa kutafuta ni yule anayehangaika kutafuta yaani leo huku kesho kule akisaka.sasa je kati ya hawa nani anampata mke mwema???

Ninachojua mimi ni kwamba Mwanaume unatakiwa ufanye vyote viwili,yaani umwombe Mungu na pia umtafute mke anayekufaa kulingana na vigezo flani flani ulivyojiwekea kama tabia,rangi,umri n.k

Kwahili kuna Watumishi wengi sana wanawadanganya waumini wao na kuwapa moyo kuwa waombe na kusubiri tu watawapata,ni Uongo huo au atakuja mtu asiye sahihi kwako kwani hana vigezo unavyovitaka na mwishowe mnaachana.

Hata hivyo Watumishi wengine wanasema uongo kuwa wameoneshwa huyu ndiye mkeo,kumbe sio.

WATUMISHI HAPA INAWAPASA WAWE MAKINI SANA NA WAKWELI.
 
Habarini za asubuhi wanajamvi, natumaini mmeamka vyema katika siku hii. Kama kichwa cha habari kilivyo ni kwamba nimekuwa nipo katika mtanziko kuelewa kuwa mke mwema mtu humsubiria tu bila kuhangaika au inambidi mtu atafute mwenyewe.1. Mke mwema huja kwa kumsubiria tu bila kuhangaikaKatika dhana hii kwa wakristo, watu husema inambidi mtu atulie tu maana Mungu kwa wakati wake atampatia mke mwema. Hoja kubwa hapa ni kwamba Adamu binadamu wa kwanza alilala tu kisha Mungu akampatia mwanamke na alipomuona akasema huyu ni nyama ya nyama yangu na mifupa ya mifupa yangu. Hivyo katika muktadha huu watu husema mtu hatakiwi kuhangaika kutafuta mke bali Mungu kwa wakati wake atampatia mtu mke mwema.2.Mke mwema huja kwa bidii ya kutafutaHapa watu husema mke mwema hupatikana kwa bidii ya mtu mwenyewe kutafuta. Hivyo mtu anatakiwa ajue jinsi ya kumshawishi mtu awe mke wake katika hili watu hupinga kwamba kuna mke ambaye mtu humsubiria bali mtu mwenyewe anatakiwa afanye jitihada.Kulingana na maelezo haya nilikuwa naomba kusikia kutoka kwa wanandoa au watu ambao washapata wenzi na wanamatarajio ya ndoa,je mlifanya jitihada za kutafuta au mlisubiria tu???Karibuni kwa michango......

Dr Myles Munroe katika mafundisho yake ya ndoa kwa ss wakristo anasema Mungu hakupi mke o mume bora. Yeye anafundisha kuwa ukisoma vizuri biblia ni kuwa Mungu ameweka vigezo ambavyo cc binadamu inabd tuangalie when looking for a spouse. So when looking for a husband o wife..angalia hivyo vigezo je huyo mtu anavyo and instead sitting and waitng kupewa mke/mme mwema..So kwa mafundisho yake ni kuwa we ourselves ndo tupo responsible kutafuta hao wenzi nad God has already given us criteria to look for..wenye muda watafute hayo mafundisho on line "Kingdom Keys to Successful Relationships
 
Kwa reference ya maandiko ya biblia, mke mwema anatafutwa lakini mume mwema anasubiriwa.
Refer rebeca na isaka, mtu alitumwa kumfuatia isaka mke na rebeca alikutwa katika harakati zake ila wema wake na tabia ya ukarimu ndio iliyomthibitishia yule mtu anayemtafuta mke wa isaka na kumbe ni wa nyumba aliyoagizwa aende.

hata mume mwema anatafutwa mkuu.... huo mfano uliutoa si kugezo sana maana pia ukumbuke ni Rebeca huyohuyo ndio alipanga njama za kudhulumu haki ya mtoto wake Esau... tayari sifa mbaya hiyi kwake...

kutafuta na kusubiri vyote vinatenda kazi pamoja, ikisema usuburi bila kutafuta utakuwa umekisea sana.
 
Ninachojua mimi ni kwamba Mwanaume unatakiwa ufanye vyote viwili,yaani umwombe Mungu na pia umtafute mke anayekufaa kulingana na vigezo flani flani ulivyojiwekea kama tabia,rangi,umri n.kKwahili kuna Watumishi wengi sana wanawadanganya waumini wao na kuwapa moyo kuwa waombe na kusubiri tu watawapata,ni Uongo huo au atakuja mtu asiye sahihi kwako kwani hana vigezo unavyovitaka na mwishowe mnaachana. Hata hivyo Watumishi wengine wanasema uongo kuwa wameoneshwa huyu ndiye mkeo,kumbe sio.WATUMISHI HAPA INAWAPASA WAWE MAKINI SANA NA WAKWELI.
Hehehe!!! Sawa mkuu mimi mwenyewe katika kuishi kwangu nimeona kwamba wanaume hutafuta tena wengi wakiwa wamemtanguliza Mungu kwanza ila nashangaa sana kwamba hatuhitaji kutafuta bali Mungu atatuonyesha tu wakati ukiwadia au labda wengine tuna Imani haba?????
 
Dr Myles Munroe katika mafundisho yake ya ndoa kwa ss wakristo anasema Mungu hakupi mke o mume bora. Yeye anafundisha kuwa ukisoma vizuri biblia ni kuwa Mungu ameweka vigezo ambavyo cc binadamu inabd tuangalie when looking for a spouse. So when looking for a husband o wife..angalia hivyo vigezo je huyo mtu anavyo and instead sitting and waitng kupewa mke/mme mwema..So kwa mafundisho yake ni kuwa we ourselves ndo tupo responsible kutafuta hao wenzi nad God has already given us criteria to look for..wenye muda watafute hayo mafundisho on line "Kingdom Keys to Successful Relationships

Nakubaliana na huyo Mtumishi kwa 100%
 
Ndio, mwenyewe huelewa hivyo ila kuna mchungaji katoa somo eti wanaume hatuna haja ya kutafuta bali Mungu kwa wakati wake atatupatia tena anadai ukikutana naye tu utamwona tofauti na moyo utakutuma kuwa ndiye. Sasa hapa nabaki njia panda...

huyo mchungaji hapo kawadanganya.... tumia tu akili yako, ukiwa mtu mzima kuna mamvo tu yanakuja automatically ....
utasubiri sana kumbe Mungu amepanga kukupa mke kwa njia usiyoitarajia kabisa.
 
Hehehe!!! Sawa mkuu mimi mwenyewe katika kuishi kwangu nimeona kwamba wanaume hutafuta tena wengi wakiwa wamemtanguliza Mungu kwanza ila nashangaa sana kwamba hatuhitaji kutafuta bali Mungu atatuonyesha tu wakati ukiwadia au labda wengine tuna Imani haba?????

Ukiamua kusubiri ashushwe kutoka juu....Utasubiri sanaaa kumpata unayempenda. USIDANGANYIKE MKUU.
 
huyo mchungaji hapo kawadanganya.... tumia tu akili yako, ukiwa mtu mzima kuna mamvo tu yanakuja automatically ....
utasubiri sana kumbe Mungu amepanga kukupa mke kwa njia usiyoitarajia kabisa.

Ndio sawa na wale wanaosema usioe mtu ambaye hajaokoka au ambaye si wa kanisa lako,wanasahau Mussa alioa wapi,wala hakumuoa muisrael mwenzake bali mmisri.
 
Kabla hujaanza kumsaka mke mwema, make sure na wewe ni "Mume mwema", kwa sababu tumeambiwa Mungu anakupa mtu wa kufanana na wewe.

Kinachofuata ni maombi. Kwa kuomba unamaanisha kuwa unahitaji msaada kwa Mungu, wewe Peke yako huwezi kufanya chaguo sahihi. Mungu atakudirect upite wapi ili ukutane na mke mwema na utakapokutana naye utambuaje kuwa huyu ndiye

Unaingia kumsaka sasa, na kwa muongozo wa Mungu Ukikutana naye utamjua tu huyu ndiye. Tatizo letu wengi ni kwamba tunajichagulia mtu either kwa tamaa zetu afu unaanza kujisikilizisha sauti yako wewe mwenyewe ikisema "huyu ndiye", na sio sauti ya Mungu. Mwisho wa siku maumivu tuuu

N:B
Wema" wa mke ndiyo nguzo ya sifa nyingine zote za mke. Ndo maana imeandikwa "mke mwema ni nani awezaye kumwona" Mithali 31 :10- 31 imemuelezea vizuri sana mke mwema. "Wema" ni universal then vifate uzuri, rangi, height, figure, kabila etc kwa sababu hivi vyote ni subjective kutegemea na muhusika.
Then Kila mwanamke ni mke, but sio kila mke ni mke wako, so Mungu akuongoze kumchagua yule wa kwako
 
Kizuri ni kile ulichokifanyia jitihada. Mungu nisaidie sawa lakini na wewe inabidi ujisaidie kwa kujitahidi kutafuta pia. Adam hakuletewa tu, baada ya kuwa peke yake kwa miaka kibao, akaomba kupata msaidizi ndiyo akaletewa Hawa. Lakini angekaa kimya angepelekwa "neutral" mpaka leo.
 
Back
Top Bottom