Mke kuzaa nje ya ndoa

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,998
Reaction score
135,207
Wakuu, hii mada imekuwa inspired na
Ndo maana nikasema sio kila mwanaume
wapo wanaoibiwa hawajui but wengine huwa wana kama sixth sense hivi
au strong connection.....labda Pasco aje atusaidie.....
Mkuu The Boss, kwanza asante kwa hili la "sixth sense". Hapa siizungumzii bali naanza na mazingira ya mke kupata mtoto nje ya ndoa!.

Kuna sababu nyingi za wamama walioko ndani ya ndoa zao, kujiiba nje na kuleta mtoto wa nje ndani ya ndoa, kunakuitwa kubambikiwa, au hata kubambikiwa tuu mimba ni kisha kusingiziwa mtoto.

  1. Sababu kuu ya kwanza ambayo ndio maarufu zaidi ni kwa Wachagga wa zamani, wana kitu kinaitwa "curse" laana!. Ikitokea mkalaaniwa kizazi chote cha mfano cha Mkuu The Boss, ikitokea mkakorofishana na mtu (people with powers) akakulaani, then uko wako wote mnakuwa wiped out, one after the other within a specific period of time, mwisho wa siku, wore mtakwisha and there will be no trace ya jina la The Boss,at a survive!, kwa kulijua hili, wamama wa Kichagga wa enzi hizo, walikuwa wanafundishwa jinsi ya kuiba, na huyo unae iba nae unamchagua mtu anae fanania fanania na mmeo, ili dili isistukiwe!. Mwenye mtoto kamwe haambiwi, and no one will know zaidi ya mama, mara nyingi hutokea huyo mtoto aliyeibiwa kuja kuwa odd man out, au very bright, au kuwa na tabia za ajabu tofauti na wengine wote!. This was usually done in good faith!.
  2. Wizi wa pili ni pale Baba ana tatizo, hawezi kutengeneza watoto!, zamani ikiamini ugumba ni tatizo la mwanamke tuu, na kikawaida wanaume huwa hawapimi!. Mke kaolewa miaka inapita hashiki ujauzoto, anayelaumiwa, kunyooshewa vidole, kunyanyaswa na kusimangwa na mke! huku akitukanwa "mgumba" kazi yake ni kujaza tuu choo!. Mke anapimwa anaambiwa yuko normal, kumshauri mume akapime anaogopa kwa vile ugumba ni tatizo la mwanamke tuu!. Kitakachotokea kwenye familia hii, mume ataanza kuwa rude na kucheza rafu za wazi kusaka mtoto nje!. Hivyo anakuwa mipiga nje mzuri huku mke akivumilia kusubiria kuletewa watoto wa nje kulea!. Hili lisipotokea, mke au kwa kushauri na watu wa upande wake, au kwa her own initiatives, naye ataanza majaribio ya nje kwa siri, akinasa tuu, ataonyesha mapenzi ya ajabu kwa mumewe hata kama mume hataki tena game, atalazimishwa kisha mke atampa taarifa mume kuwa ameshika!. Itakuwa ni furaha kuu nyumbani, mume atafurahi na ndoa itashine!. In this case the "dume la mbegu huwa lina taarifa ni nini kilikuwa kinatafutwa", na usually ataendelea kutoa mbegu kwa watoto wengine wote wa huyo mhusika!. Kuna familia nyingine mume anapina na kujikuta hawezi kutengeneza watoto, ili kuepuka aibu ya hawezi, anamuweka mkewe kwenye very compromised situations za kupigwa nje ili siri isifichuke!, au koo serious wadogo mtu au kaka mtu wanashauriwa kumsaidia ndugu yao ili kumfichia siri na kuepuka aibu ya ukoo. Hapa mume atajua watoto sio wake ila atawapenda tuu kiunyonge unyonge!.
  3. Mimba za tatu za nje ya ndoa ni zile za michepuko tuu, usually hizi ni au za bahati mbaya au za makusudi!. Hapa ni pale kiukweli wanaume wengi wa kibongo, ni very insensitive kwa mahitaji ya wake zao, hivyo mnamkuta mke tangu ameolewa hajawahi kufikishwa ndani ya ndoa yake!. Mume akishafika tuu ndio mwisho wa shughuli!. Siku ke akichepuka na kukutana na mafundi akafikishwa!, then frrom time to time, bingwa atapelekewa!, "secret lover concept!". Ni katika kuridhishana huko, mtoto wa nje atatengenezeka na baba wa nyumbani kubambikiwa, au kuna wanawake wengine as a sight ya appreciation kufikishwa, anadhamiria kabisa, kumzawadia mtoto huyo lover wake ili ku intensify the bond!, ambao in this case lover anaelezwa ila mume ndio anafanywa zoba!.
  4. Aina ya nne, ni mke anapobakwa nje na kushika ujauzito, hawezo kusema.
  5. Koo za wake wengi kama za Kisukuma wa zamani, mtu wake 20!, hawezi kuwa service wote, hivyo wake wengine kujikuta wanalazimika kwenda nje kukidhi haja na huko ndiko watoto wa nje hupatikana na kuwaleta ndani, na kikawaida Wasukuma ndio kabila linaloongoza kwa upendo kwa wanawake na watoto!, hata kama unajua fika huyu sii damu yako, sisi tunapenda tuu!. Mimi mwenyewe hapa nilipo nina watoto 7!, miongoni mwao mimi mweusi, wife (1) mweusi, miongoni mwa watoto wetu kuna "cheupe!" ni kibinti, kizuri na ndio kipenzi cha baba!.
  6. Kwa familia za wafugaji, waume wanapokuwa malishoni kipindi cha ukame, huweza kukaa hukohata miaka miwili na kuwaacha wake zao nyumbani, wakirudi, wanakuta watoto na ni "watoto wao!".

Kwa hiyo mke kupta mimba ya nje akiwa ndani ya ndoa, sio lazima iwe ni majanga, sometimes ni blessings!. Ila pia jamii zetu zimegubikwa sana na mfumo dume!. Sisi wanaume kila siku tunazaa nje ya ndoa and its usually not a big deal!.
Lets be fair kwa wake zetu!.
Thanks.

Pasco
 
eti Pasco ikitokea umeongopewa kuwa "sijaolewa" ukapiga mzigo kikanasa, "kutokuelewa" hakukupi nafasi ya namna yoyote kudai mwanao!!!?
 
Last edited by a moderator:
Hili la wanaume kupima kujua kama wana matatizo linakuwaga gumu sana. Wengi watakataa kupima na asilimia kubwa ya wale wanaopima hufanya kwa siri bila kuwashirikisha wake zao.

Nina rafiki, mume wake aligundulika ana tatizo baada ya kufanya vipimo kwa siri. Mke akagundua mume wake anashida baada ya kutonywa na nurse rafiki yake and she was warned not concieve with another man yeye hakusiki She went got herself pregnant. Mume aliposikia mke ana mimba ndio akaweka wazi tatizo lake, "umetoa wapi mimba na mimi sina uwezo huo" ona jinsi alivyoonyesha uselfish wake, mkw wake aliteseka kwa masimango ya mawifi kwa muda mrefu yeye kapiga kimya, mke hakusema kitu ingawa alijua hali halisi. In the end akaamua kuwaonyesha kwa vitendo after all actions speak louder than words.
 
Hili si tatizo kubwa sana kuna rafiki yangu alimpa mimba mchepuko wake kwa bahati mbaya na akamwambia asitoe atapata mtoto wa kiume na kwa kuwa alikuwa na watoto wa kike tu basi hakutoa ile mimba na kweli akapata mtoto wa kiume very bright, kwa hiyo wakati mwingine ni blessing na wala mume hajui kwa kuwa naamini wanawake wana Siri kubwa sana na ni majasusi haswa, refer Eva/ Hawa, Delila.wakiamua kufanya ujasusi hawafanyi kosa wanakuwa kama CIA na wala mwanaume huwezi kujua kabisa kwa kuwa mwanamke akishajua hivyo anakuwa na digrii ya hali ya juu ya unafiki.
 
Kule nchini Uganda wao wakigundua kama mtoto wao wa kiume hawezim kumtia mimba mkewe, basi wanateuwa mdogo wa mume au kaka wa mume ambaye yeye hafanyi makosa bila mwenye mke kuambiwa, kinachotakiwa, mke anaelezwa kila kitu na shangazi wa mume hivyo anaelewa somo,hivyo zle siku a hatr zikikaribia anatoa taarf kwa shangzi kisha mwenye mke anatengenezewa safari, akiondoka tu huyo ndugu yake aliyeteuliwa anamuingilia mke wa kaka yake hata kaka akirudi wanasiilizia kwa mwenzi mmoja mke akithibitisha amepata mimba inakuwa ni furaha ya familia.

Lakini hakutakuwa na uhusiano wa mapenzi na mtia mimba hadi pale itakapohitajika mimba nyingine, ndiyo zoezi hilo litafanyika.

Sijui kaka yangu Pasco hii imekaaje?
 
Pasco mkuu leo umekuja jukwaa la MMU i like it, umeelezea situation ya mwanamke "kumbambikia" mtoto mume wake lakini all in all according to my experience ya issue hizo mtu anabambikiwa huku akiwa ana uwezo wote kibalojia hapo ndipo unsolved conflict inapoanzia na sio situation ile ya mwanaume kujijua kua he is incaple to impregnante
Secondly wanawake wengi wa siku hizi ni opportunistic ana date na wanaume wawili au watatu etc siku aki conceive anaangalia wapi ampeleke mtoto basing on Uwezo wa kiuchumi hata kama anajua jamaa haiwezi kuwa ndo alipiga kitu
From my points above naweza ku justify na ku conclude kua wanawake wanaofanya hivyo wote enzi hizi ni kwa sababu ya UMALAYA and this habit is totally not accepted
 
Last edited by a moderator:

kwa mazingira ya siku hizi watu wanachapiwa sio kwa sababu za kibalojia kuwa hawawezi kujaza mimba bali ni kwa sababu za kiuchumi na tabia ya umalaya ya mwanamke
 
Wa siku hizi wakipewa kazi I swear watatangaza all over fb, instagram, twitter, jf you name it. Bora mtu akubaliane na mke wake akatafute anakojua yeye esp kama lengo ni kutunza heshima.

 
Kwa Ulaya Sperm Bank zinatumika vizuri kumpa mwanamke mimba kwa kuchagua sperm ya mtu anayemtaka ila gharama ya kufanya hiyo artificial insemination ni kubwa kidogo. Hapa kwetu bado Sperm Bank kwa binadamu haijaanza ila kwa wanyama kama ng'ombe, mbuzi n.k ipo toka siku nyingi sana na inarahisisha upatikanaji wa mnyama mwenye kinga ya mwili mwenye kuhimili hali ya hewa na faida ya nyama au maziwa kwa wingi.
 
Kule kwao umasaini mkuki unachomekwa mlangoni kidume kinapiga mzigo, ndani mwenye mke ukikuta mkuki unatakiwa kupitiliza na safari zako
 
Pia wanawake kutafuta mbegu nzuri, labda kaona mume wake hana sura/umbo nzuri, sio bright n.k inaruhusiwa kusaka mbegu nzuri sio kuzaa binadamu wajingawajinga/wabaya wabaya, sura za ajabu ajabu!
 
Kama kuna kitu naogopa katika maisha yangu, ni hiki. Eee Mungu niepushie mbali kitu hiki.

Imagine unaiba na mzungu, mara kitu ndani, unazaa chorichori? Mmmh, wasukuma wale lazima wamfanye mtoto 'shingila'.
Au baba tolu, unazaa andunje?
 
aiseeeee somo zuri ila kwa kizazi hiki ni ngumu kumesa kwanza jamii haina siri
 
He he he, watoto kwa asilimia kubwa hufuata akili za mama, sema mama ukijiona kilaza, na mume kilaza, inabidi uwaloweke kwenye madesa kwanza.

Pia wanawake kutafuta mbegu nzuri, labda kaona mume wake hana sura/umbo nzuri, sio bright n.k inaruhusiwa kusaka mbegu nzuri sio kuzaa binadamu wajingawajinga/wabaya wabaya, sura za ajabu ajabu!
 
Sijajua kama hizi ni compliments au...majasusi, CIA, degree ya hali ya juu ya unafiki...Hawa Delila...teh teh teh...lakini mnatupenda au siyo...

 
ama kuna kitu naogopa katika maisha yangu, ni hiki. Eee Mungu niepushie mbali kitu hiki.

Imagine unaiba na mzungu, mara kitu ndani, unazaa chorochori? Mmmh, wasukuma wale lazima wamfanye mtoto 'shingila'.

umenikumbusha hapa jirani kuna familia ya kipemba watoto wote weupe kasoro binti wa mwisho ana rangi ya kipekeee mama alipata misukosuko kutoka kwa mawifi lakini ndoa bado iko imara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…