Mke kampeleka mme polisi

Mke kampeleka mme polisi

bahati mbaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
578
Reaction score
193
Mme na mke waligombana, wakati wa ugomvi mme kachukua msumemo kamkata mke kwenye paja. Damu zikatoka kwa wingi. Mke akaamua kwenda polisi kufungua kesi na kupewa PF3 ili aweze kutibiwa.

Polisi walikuja kumchukua mme wake na kumuweka Rumande. Je ni haki?
 
haki kabisa......kwa nini amkate......? sh**i type....tena aozee lupango.....
 
wewe ulitakaje??
je kuna mwenye haki ya kuumiza/kudhuru mwili wa mwenzie??
 
Ni haki kabisaaaaaa ajiuguze apone na kesi pia iendelee tena afungwe ili iwe fundisho kwa wengine.
 
haki kabisa......kwa nini amkate......? sh**i type....tena aozee lupango.....
Nina uhakika akipona atarudi kwa mumewe... Chezeya malove weye... Na ataenda mwenyewe kufuta kesi
 
Hivi mwanamke akiumizwa hana haki eti??Kwa hiyo mwenye haki ni aliyeumiza,kisa mwanamme???Hebu wanaume tuwe na utu kwa hawa wasaidizi wetu.
 
Inasikitisha sana katika karne hii bado kuna wanaume wenye tabia kama hizi.
 
++
Mapenzi yakikuchanganyia ni faraja moyoni LAKINI yakikuchachia polisi,mahakamani watu hufikishana.
++
 
Vipi kama ingekuwa mwanaume kachanwa na msumeno ungeamuaje???????????? Tabia hizi za kuumizana kisa mapenzi zinatakiwa zikomeshwe kwa nguvu...Ningekuwa na mamlaka ya kupitisha kijisheria kidogo cha haya mambo ningeshauri kusiwe na haja ya kufikishana mahakamani akikamatwa mhusika na ushaidi wa muumizwaji upo kituo cha kwanza ni gerezani miezi sita bila hata kesi then tunarudi kuendelea na kesi kama tukimfunga mwaka tupunguze miezi sita.. Lazima adabu itachukua mkondo wake.
 
Ni haki,

Ingawa mwanamke ni kama mtoto, anatakiwa kulelewa kiupendo na aelimishwe anapokosea ikizidi ndo afundishwe adabu kidogo.

ila haitakiwi kumdhuru kwa lolote lile,
 
Mme na mke waligombana, wakati wa ugomvi mme kachukua msumemo kamkata mke kwenye paja. Damu zikatoka kwa wingi. Mke akaamua kwenda polisi kufungua kesi na kupewa PF3 ili aweze kutibiwa.
Polisi walikuja kumchukua mme wake na kumuweka Rumande. Je ni haki?

Upo nje kwa dhamana au huyo nduguyo yupo nje kwa dhamana au siku hizi mahabusu kuna namna ya kutumia mitandao?
Mtu ambaye yupo kwenye neutral grounds lazima aone kama hili ni kosa maana ni shambulio la kimwili...lakini ndugu mleta mada ninahisi una mkono kwenye hii kadhia ndio maana umevaa miwani ya mbao na kushindwa kuona kuwa kuna mushkeli hapo.
 
mbona ni hakki sana tena apewe adhabu kali sanaaaa, hvi umemaanisha nini ulipo maanisha kama hiyo ni haki????
 
wala siyo haki
tena ukafuatilia chanzo cha ugomvi atakuwa ni mwanamke.

kwani mkishindwa kukaa na hao wanaume si muanze tu
mbona maisha yapo tu kwanini kukaa hadi kumlaza mwenzio lupango
not good.
 
Nina uhakika akipona atarudi kwa mumewe... Chezeya malove weye... Na ataenda mwenyewe kufuta kesi
Kwa jinsi alivyokuwa na mapaja mazuri ni lazima POLISI na MaDr waonje kwanza wakati Balozi mate yakimdondoka
Wakishakinai atajutia na kumtoa Mzee ili aendelee kula vyake
CHEZEA MWANAMKE WEYE
 
Case nyingine jamani khaa....Ukataji wa msumeno ni kwa kupeleka mbele na nyuma, kwa hiyo mtu katega paja na kukatwa!

Anyways, sina uhakika kama kuna haki ya mtu mmoja kumuumiza mwingine, regardless ya kosa, awe mwanaume au mwanamke. Kwa sababu tu case iliyopo mbele yetu ni ya mke na mume, je angekatwa na mtu tofauti na mumewe angepeleka kesi polisi? kama ndio, basi bado haki yake itabaki pale pale. Tatizo tu ni kwamba mambo ya upendo yana vizungumkuti vyake, wape wiki mbili tatu mambo yapoe utakutana nao barabarani wameshikana mikono. Na bibie akimsimulia mumewe kuwa vizabinazabina ndio walimsukuma ampeleke polisi, lakini yeye akhuuu....wala hakutaka!
 
Jamaa yuko nje kwa dhamana.

Yupo nje kwa dhamana. Tatizo kubwa jamaa huyu anapenda sana kutumia nguvu hata katika mambo ambayo hayahitaji nguvu. Maana emekuwa ni mzigo katika familia yake ndiyo maana mkewe ameamua kumfunza adabu katika tukio hili. Jamaa kwa kipindi hiki hatoki ndani, akitoka mwenye mihangaiko yake anaingia kwenye net hata kama jua bado linatoka. Nadhani itakuwa fundisho kwake na kwa wote wenye tabia kama yake. Maana sheria inachakua mkondo wake.
 
Akifungwa ile huduma ya ku t.o.m.b.w.a. na zile za kijamii atazipata polisi au.....!???

Ni haki kabisaaaaaa ajiuguze apone na kesi pia iendelee tena afungwe ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Back
Top Bottom