Mke hataki nimpe mimba nyingine!

Mke hataki nimpe mimba nyingine!

Kuzaa kwa kisu haimaanishi atazaa tena kwa kisu. Kuzaa kwa kisu hakuna muda najua hata waliozaa watoto wakiwa mwaka na kitu au miaka miwili. Cha muhimu ni uamuzi wenu.
Na kama unazaa kwa kisu incase scars hazijapona basi huko mbeleni kuna labda kuzaa kwa kisu tena. Kisu wanashauri mwisho kukatwa mara nne as mascar yanajiweka kila baada ya kisu na inakuwa hatari zaidi pa kukata kuingia kumtoa mtoto.

So kwa kesi yako mie nadhani kuna tatizo, hakuna mwanamke alie ndani ya utamu wa ndoa atatoa sheria ya miaka 5 ndo nitazaa tena, unless anadhani scars zitakuwa zimetoka ndio azae kikawaida ila kwa dunia ya sasa na maisha ya kula ovyo mtu huwezi jua kama hata utaweza kuzaa au hata kushika mimba tena.

Wanawake wengi wanazubiri baraka za Mungu, wengi wanalilia kids hawapati hata mimba.

Ongea nae ujue tatizo kubwa nini, I hope haendi nje maana dunia ya siku hizi wanawake wetu wa bongo wanatabia mbaya na ya kujisahau.

Au alipozaa mtoto ulimwangaliaje? Ulimpa memory ya kujuta why na wewe au?

Nimeandika mengi kwa mifano tofauti.
 
..mpe mimba,miaka miwili mingi sana,mchape mimba huyo kwani alikuja kula ugali hapo,kwao mbona upo . Wanawake bana akiwa hana mtoto tabu,akiwa anauwezo wa kuzaa taabu,mbona wanawake hatuwaelewi aaagh..
 
mwenzio akiangalia lile kovu
pale pembeni maumivu yanarudi upya atiii
mwache mtt afikishe miaka 4 o 5 atakuelewa!
 
Kama una haraka ya kuzaa kupitia nyumba ndogo, basi tafadhali mruhusu na yeye mkeo baada ya hiyo miaka mitano naye atafute nyumba ndogo ya kuzaa naye.
 
Wakati amezaa mtoto wenu huyo kwa operation inawezekana hukumu-andle vizuri, pengine ndiyo sababu anajishauri kuzaa mapema. Pia jaribu kuangalia sababu gani ilimsababisha kuzaa kwa kisu huyo mtoto. Muda mzuri wa mwanamke aliyezaa kwa siku ni baada ya miaka 3 ili aangalie chance ya kuweza kuzaa kawaida. Pia naye mwili uwe umerudi katika hali ya kawaida na kidonda kupona kabisa.

Kuzaa siku hizi ni mipango ya baba na mama siyo baba tu kuamua bila kukubaliana. Ndiyo maana mwenzako anakupa muda mrefu wa miaka mitano ndiyo azae tena. Hongea naye mtapata muafaka.
 
Hili si jambo la wewe kutaka na lazima liwe - Ni swala la nyie wawili kujadiliana/kupeana hoja hadi mwafaka upatikane. Usiwe dikteta wakati anayekula kisu ni mwenzio.
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu......
 
..mpe mimba,miaka miwili mingi sana,mchape mimba huyo kwani alikuja kula ugali hapo,kwao mbona upo . Wanawake bana akiwa hana mtoto tabu,akiwa anauwezo wa kuzaa taabu,mbona wanawake hatuwaelewi aaagh..
Kwa komenti kama hizi ni Umri wetu wengine unatusumbua!!!! Wengine ni hisia hata kuweka mtu ndani baaaaaado
 
Mwache afikishe japo miaka minne ndio umpe mimba,nakumbuka wa kwangu daktari alimwambia naomba nikuone tena at least baada ya miaka mitatu na huu ni wa nne na niliona jao nimpe minne ili na yeye apone vizuri,haraka ya nini kaka!Usije poteza mke kama ikimletea matatizo
 
MKuu ni bora mkafanya utaratibu wa kuwaona watabibu, humu JF utapigwa mawe wee hadi ushindwe pa kushika, sana sana hapa wengine watakupa mawaidha tu na Ushauri Usio wa kitabibu, mshauri mkeo mwende kwa watabibu.
 
Au mwanamke anapojifungua kwa oparesheni inatakiwa akae miaka mingapi ndio apate ujauzito mwingine!
!
hili ndio swali unapaswa kuuliza kabla hujalalama ukishapata jibu ndio uanze kumlaumu ,je ulihudhuria cliniki na mkeo wakati wa mimba hiyo na tahadjhari alizopewa na docta wakati amepatiwa operation ulizipewa.nafikiri wadau watakupa darsa zuri
 
Wanaume wengine Bana pttttttttttttyuuuuuuuuuu!!!!!!!!! yani hata hamuwaonei huruma wake zenu hamsikii au hamoni jinsi watu wanavyokufa kwa ajili ya uzazi mke wako hata miaka mitatu hajafikisha unataka umpe tena ujauzito au kwa vile leBa hauendi unayafahamu maumivu ya kujifungua kwa upasuaji,ingawa wengine wanajifunguaga mara moja kwa kisu akkienda tena kawaida,na wengine maungo yao kawaida haiwezekani nyonga ni ndogo na vitu kama hivyo sa inakuaje mke wako yuko kwenye kujifungua kwa upasuaji,heBu jariBu kuwa na utu walau hata kidogo,na kama ndo unataka kwenda kwa nyumBa ndogo Basi ufike salama muache mtoto wa watu apumzike

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hayo ni mambo ya kuongea ninyi wawili na kufikia uamuzi na sio kutumia nguvu kama unavyofanya, amekueleza sababu ya kuchagua hiyo miaka mitano? na wewe hiyo hoja kuzaa sasa ili arudi kwenye usichana mbona haina mashiko mkuu.

Kumbuka umekiri mwenzako alijifungua kwa kisu, hivyo mpe nafasi apumzike hata kama sio hiyo miaka mitano anayosema mnaweza endelea na mazungumzo hayo na baada ya muda mtafikia muafaka sahihi wa lini mpate mtoto na wakati huo mambo mengine ya kimaisha yanaendelea.
 
:nono: hahahahahaaaa,, jamaa anataka kuhalalisha nyumba ndogo tuu.... acha hizo broo,, mpende mkeo....ndio yy alikufikisha hapo mlipo... unaitwa baba nani vilee?
 
Wasi wasi wake ni kuwa utampa hiyo mimba na baada ya muda si mrefu sana utataka mimba nyingine na nyingine
 
Hili mkiliongea chumbani mbona linaisha.Una haraka ya wapi?Ushauri unaoutafuta humu, nakutakia kila la kheri.
 
Mtego wa note, mimi naona hapo ni swala la kuelewana tu, wala hakuna haja ya kuwa na hasira na jazba, utaharibu kila kitu, wewe la kufanya usizungumzie tena kuhusu mtoto, nyamaza kimya, halafu anza kwa taratibu sana umuulize kuwa angependa kuwa na watoto wangapi? akikujibu, tulia anza kuweka mitego , tena ni rahisi sana ikifika wakati anakwambia vaa zana wewe vaa, ila iko siku atajisahau hapo nawe usikosee fanya vitu vyako.
Sisi wanawake tunapenda sana wanaume wanaotusikiliza, so wewe jifanye mjinga msikilize halafu utasahau wewe utaendelea, mimba ikishika mbembeleze azae, kuwa ilikuwa bahati mbaya hukudhamiria. ataelewa na atakuzalia mtoto mwingine kama ulivyopanga. na kutakuwa hakuna kuvutana kati yenu.
 
huyu wa sasa hivi anapata matunzo stahili??angalia usikute kashaona matunzo yote unamuachia yeye
 
Mimi namshangaa huyu mke wangu! nimezaa naye mtoto mmoja ila alijifungua kwa njia ya upasuaji miaka miwili iliyopita. kwa sasa mtoto keshakuwa mkubwa maana ana umri wa miaka miwili na mimi nilitaka nimpe mimba nyingine ili azae halafu ndio tupange mipango mingine ya maisha.

Cha kushangaza sasa ni kuwa kila ikifika muda wa yeye kupata mimba hukwepa sana ikiwemo kutaka tutumie zana ili asipate mimba.

Nishamwambia tupate mtoto mwingine ili tupumzike kabisa ili mwili wake upate nguvu aruie hali yake ya usichana lakini hataki kunielewa ati anataka tuzae mtoto mwingne baada ya miaka mitano! huku si kutaka kunifanya nikatafute nyumba ndogo ya kuzaa nayo ili niweze kujiongezea familia?

Au mwanamke anapojifungua kwa oparesheni inatakiwa akae miaka mingapi ndio apate ujauzito mwingine!
Kwa kweli nashindwa kumuelewa huyu mwanamke!

Uchungu wa mwana aujuaye mama (lakini wengine wanasahau hadi wanatupa watoto) maana yangu ni kwamba anajua uchungu alioupata alivyopigwa mkasi. Give her sometime
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom