Mke graduate

Mke graduate

Dah, mkuu hope1985 umegusa mulemule aisee me nilikuwa nae wangu wote ni graduates ila yeye kapata kazi kabla yangu tumekaa miaka sita ila baada yy kupata kazi kanivumilia mwaka mmoja tu kaanza kunifanyia vituko nikimuuliza anakuja halafu yy yupo mbali na mm. Juzi kati ameamua kunichana live hataki kuwa na mm na kigeo kikubwa ni kazi hakuna sababu nyingine. Kweli inabidi tukatafute form 4 au certificate kidogo stress zinaweza kupungua.
khaaa!
 
Acha udanganyifu mi wife wangu tumesoma darasa moja chuo kikuu kozi moja tuna miaka 4 kwenye ndoa na mtoto hakuna mushkeri adabu juu ya adabu labda huyo wako alilelewa na mama wa kambo
 
Mkuu umetisha embu nipe siri ya mautundu yako...!

Ebu mwambie huyo....tatizo vijana wengi wanakariri sana...mimi nishakua na demu mwenye PHD, na heshima ilikua tele tu...sijawai kudate demu asiye kuwa na masters degree....na wote walikua wananipa heshima kibao..elimu yangu mimi ni fom fwo ya ya kufeli. chezea mimi wewe.
 
Haiko hivyo kwa graduates wengi, hiyo ni tabia ya wachache wasojielewa kama huyo ulowahi kuishi naye ambaye elimu yake haikumkomboa kutoka kwenye ujinga wa kutojithamini.
Mwanaume huu ni ushauri wangu na uzoefu wangu maana niliwahi kuishi na mwanamke mwenye degree tena ya ualimu ni shida.

Kwanza graduates wengi wakati wowote akitokea mtu mwenye pesa nyingi kukuzidi ni rahisi sana kukuacha, wana tamaa sana. Pili wengi wao wametumika sana tena sana. Tatu hawataki uwakosoe na akikosea ukamkemea basi jua hatokubali zaidi ataanza kuleta porojo za kutetea alichofanya.

Nne wanajisikia sana hasa kama akiwa anafanya kaza na yeye anataka awe mwanaume ukimgusa tu atakwambia muachane maana anajua ana uwezo wa kulipa kodi. Tano wana marafk wengi sana wa kiume kuliko wa kike na kujidai kuishi kzungu yaan haoni hatari kula denda na mfanyakazi mwenzie au kukumbatiana au kupigiana na kuandikiana sms za usiku mwema hasa nyakati za usiku.

Sita hawana mapenzi ya kweli, anakuenda ukiwa nazo tu siku zikitoweka ujue ndo mmeachana.

Ushauri: Usikimbilie kuoa mwanamke graduate wakati wapo kibao form 4, na certificate kwani huenda utajipunguzia siku za kuishi kwa mawazo, maana mwanamke graduate omba asipate kazi, akipata ujue na yeye anaota ndevu, humwambii kitu.
 
mmmh jamani, msituponde sana. tutaolewa na nan sasa?
 
huyo mmoja asifanye uchanganye na wengine...........tafuta mchumba kwa kufuatilia chanzo chake hususani makuzi na malezi yake, aidha na we pia ujiangalie kwani hakuna binaadamu mkamilifu.
Mwanaume huu ni ushauri wangu na uzoefu wangu maana niliwahi kuishi na mwanamke mwenye degree tena ya ualimu ni shida.

Kwanza graduates wengi wakati wowote akitokea mtu mwenye pesa nyingi kukuzidi ni rahisi sana kukuacha, wana tamaa sana. Pili wengi wao wametumika sana tena sana. Tatu hawataki uwakosoe na akikosea ukamkemea basi jua hatokubali zaidi ataanza kuleta porojo za kutetea alichofanya.

Nne wanajisikia sana hasa kama akiwa anafanya kaza na yeye anataka awe mwanaume ukimgusa tu atakwambia muachane maana anajua ana uwezo wa kulipa kodi. Tano wana marafk wengi sana wa kiume kuliko wa kike na kujidai kuishi kzungu yaan haoni hatari kula denda na mfanyakazi mwenzie au kukumbatiana au kupigiana na kuandikiana sms za usiku mwema hasa nyakati za usiku.

Sita hawana mapenzi ya kweli, anakuenda ukiwa nazo tu siku zikitoweka ujue ndo mmeachana.

Ushauri: Usikimbilie kuoa mwanamke graduate wakati wapo kibao form 4, na certificate kwani huenda utajipunguzia siku za kuishi kwa mawazo, maana mwanamke graduate omba asipate kazi, akipata ujue na yeye anaota ndevu, humwambii kitu.
 
"Enyi waume ishini na wake zenu kwa akili" haijalishi ana elimu kubwa kiasi gani ilimradi ni mke mwema uliyepangiwa na Muumba,still atatambua kuwa mumewe ni kichwa cha nyumba na atakuheshimu tu na mtaishi maisha mazuri mnoooo mpk watu waone wivu

Kumbuka: Pia kuoa mwanamke mwny elimu ndogo kwa dunia ya leo ni changamoto kubwa zaidi.

Ushauri: Mwombe Mungu mke mwema tena mwny elimu,atakupa tu kwa6 uaminifu ILA nawewe utulie na kuwa mvumilivu la sivyo utapata ambaye hajatulia pia. Barikiwa!!!
 
Mwanaume makini atajibidiisha katika idara zote,kuanzia uchumi hadi elimu, angalau hiyo italeta tafsiri halisi ya mwanaume ni kichwa cha nyumba. kinyume na hapo utaishia kulialia tu. After all hujafungwa nae huyo msomi, kama unaona elimu ni kikwazo basi, kaoe ngumbaru mwenzio. Umeniangusha sana kuja na hasty gereralization ya namna hii.
 
Kuna ukweli ndani ya mada wanawake wengi waliosoma ndoa zao zina matatizo sana, wajuaji mno
 
we sio bure itakua yamekukuta yakukuta. nyie wanaume si mnasemaga wanawake waalimu ndio the best wives sasa leo imekuaje?? pole sana ila hauna point kabisa katika hiyo thread yako.
 
mwanamke ni tabia bhana syo elimu yake, umegeneralize sana, umalaya wa mwanamke syo elimu yake wengine ni four na std 7 lakini pasua kichwa . sijakubaliana Na mtoa maada
 
Oa huyo wako unayemtaka ili na waendesha bodaboda na wafyatua matofali nao wapate pa kujituliza;
kwani ni lazima uwashauri na wenzio?

Malaya ni Malaya tu regardless anawatuliza watu gani, acheni dharau Na ajira za watu, wewe tajiri/mwenye masters ungejenga nyumba yako bila mfyatua tofali? tunaishi kwa kutegemeana sana elimu au hali zetu zisitufanye tubaguane kihivyo. ni hayo
 
Kwa mtazamo wangu boys ones u need any serious relation zingatia vitu viwil HARDWORKING and DISCIPLINE mengine ni ziada pia hayawez change kama real kakupenda....i

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mi mbona nimeoa graduate wawili; wote nimeoa na nawa-manage bila shida yoyote? Labda wewe mwenyewe umeshindwa tu - tena umemshindwa mmoja!!!!!
 
inategemea malezi ya kwao,malezi ya kwenu,nidhamu ,upendo(anakupenda au mnapendana au unampenda)
baada ya hapo ndo mambo ya pesa na elimu yanakuja na yanategemea zaidi vigezo vya juu.
 
Back
Top Bottom