Unaongea kama una 'mkataba' wa kuishi milele...ukifa je na mna watoto!?
Kwaiyo watakaje labda?
Mkishaumizwaga huko mnaona hapa ndio pakutolea stress zenu eeeeh?
Mwanamke ni mwanamke tu, awe ana Elimu ya chuo, sekondari, msingi au chekechea atabaki kuwa chini ya uongozi wa mwanaume ndani ya nyumba. Kinachotakiwa uwe mwanaume wa ukweli tu.
Mwanamke ni mwanamke tu, awe ana Elimu ya chuo, sekondari, msingi au chekechea atabaki kuwa chini ya uongozi wa mwanaume ndani ya nyumba. Kinachotakiwa uwe mwanaume wa ukweli tu.
Anakumbatiana anapigana denda na wafanyakazi wenzie....ulikuwa unaishi na changudoa wewe usituletee generalization zako za kishamba hapa
Oa huyo wako unayemtaka ili na waendesha bodaboda na wafyatua matofali nao wapate pa kujituliza;
kwani ni lazima uwashauri na wenzio?
mbona unakuwa mkali?
Kwan hamna wanawake wa aina hyo?
hahahaaa! Ushauri wa bure na tahadhar yake!
sijui kwanini watu wanaendelea kujipa stress za kuwaza ndoa!!!
Kwan nimesema hawapo?? huyo ni changudoa tu si kweli kwamba anafanya hayo kwa sababu ni graduate
Mzee achana na misemo iyo...rudi in reality...asilimia kubwa ya ndoa za wasomi ni shida....m ni mmoja ya wasomi....na nmedate wanawake weng tu wasomi kuna siku le mbebez ashanambiaga wanaouting its ladies nite so nimwache aende club na mashost zake...nkamruhusu bt as a men tayar nlishampunguzia maksi za kuwa mke
dah! muwage fair jamani. Mbona wakaka wakiwa na wapenzi au wake hawaachi kwenda soccer city kucheki mpira na washkaji? au kwenda kucheza pool au bao au kupata mbili 3 na kupiga soga? haja ya socialization ni tabia ya binadamu wote. Yaani jamani mwanamke akiwa na mpenzi ndo aweke maisha yake yote pembeni aandamane na mpenziwe tu? Kwa mtazamo wangu huyo dada angeweza kuwa mke bora sana tu maana anajua kujitofautisha yeye kama mpenzi na yeye kama kitu kingine. Swala ni uwezo wake wa ku-balance mambo yake. Halafu mimi ni mmoja wa "wasomi" lakini sina hiyo "ladies nite". Inapatikana chuo gani? Tabia zingine ni za kihaiba (personality) hazina uhusiano na elimu. Kwani hakuna mabinti wasio na elimu wanaruka kuta kwenda kwenye clubs usiku? Mtu kuwa outgoing au indoor haina madarasa. Unaweza oa mwenye elimu ndogo lakini akawa hapungui kwenye matukio mpaka vigodoro vya usiku na atakulazimisha umnunulie sare kwa kila tukio na ole wako umnyime! Cha msingi ni mtu kutafuta mwenzi wanayeendana katika mambo ya msingi kuanzia maumbile mpaka mitazamo. Kutoa ushauri kuwa wanaume wasioe wasomi ni kumaanisha wanaume wote wote wanasumbuliwa na wanawake wasomi kitu ambacho hakina ukweli wowote. Mtu akiona mwanamke amemshinda na akapata uhakika kuwa mwanamke ameshindikana kwa sababu ya usomi naunga mkono hoja kuwa aoe "mjinga" au mwenye elimu ndogo.
hili vijana wengi hawalijui
eti mke hana cha kujisifia kwako, atakuheshimu kweli!!!
Kinyume cha usomi si ujinga, tatizo la wasom weng wanaiga sana...hatusem wote weng wao...then wanadhan wakipata kaz bas mwanaume kwake si kitu
nimesema "aoe mjinga au mwenye elimu ndogo". Elimu ni "scalar". Neno mjinga hapo limetumika kumaanisha asiyeenda shule. Na nijuavyo mimi mwanamke akijiweza kiuchumi huhitaji mwanaume kwa ajili ya ulinzi wa kihisia. Sasa asipoupata huwa hana sababu ya kukaa na mwanaume kwa ajili ya "itifaki". Mwanamke asiye na elimu au fedha humtegemea mwanaume kwa ulinzi wa kifedha na kihisia. Asipopata ulinzi wa kihisia huendelea kubaki kwa ajili ya ulinzi wa kifedha. Akipata ulinzi wa kihisia akakosa wa kifedha uwezekano wa kuvumilia shida za kiuchumi ni mkubwa. Elimu na kipato vina athari chanya au hasi kwenye mahusiano. Na wasomi hawawezi kufanana mienendo na maamuzi. Kila mmoja anaathirika kipekee hivyo sidhani kama ni sahihi kusema wanaigana.
Inferiority complex at work. Mama yangu ni phd holder na kakaa na baba yangu mwaka wa 40 sasa! Inategemeana na mtu, kuna watu darasa la saba na ana nyodo utasema ceo fulani. Wanaume kama nyie mnapenda ku control wanawake na kuwakandamiza with all your bullshit na mwanamke asiseme kitu kwa kuwa hana economic power anahofia atakula nini ukinuna. Mnapenda kuabudiwa mwanamke asichangie chochote ukisema wewe yeye afyate atekeleze tu. Unaongelea kauli kama kumkemea mwanamke... huna haya huyo ni your partner hupaswi kuona kuwa hicho ni "kitu" cha kukemea. Mwanao huyo?! Kila mtu akijua nafasi yake kama mke na kama mume hata mke awe profesa haijalishi. Kwa taarifa yako naniliu hizo huko chini hazijui degree! Haya sasa... mwanaume ukiwezeshwa unaweza. Jiamini!