Mke anashinda Kanisani !!

Ni wazi kabisa kuwa tunabomoa, lakini naomba ajaribu haya yafuatayo;

1. Ajaribu kumsomea mkewe mistari ya vitabu takatifu yanayohusiana na ndoa/mapenzi, huenda akatambua nafasi na majukumu yake kwenye ndoa.

2. Amwekee facilities zote, kama vile vitabu vya Mungu chumbani, na amfungie aombe huko, huenda akaona kuwa kumbe maombi sio kanisani tu, bali ni imani, matendo na moyo wako tu.

3. Amrudishe kwa waalimu wao wa maswala ya ndoa, huenda hakutoshelezwa, hivyo akapatiwe kisomo tena, huenda ikamsaidia kujua palipo na pungufu.

4. Atambue kuwa "LIFE HAS NO A FIXED FOMULA". Hinyo, kama vipi atumie nguvu na nafasi yake ya ukichwa cha nyumba kumpiga stop mara moja.

5. Hayo yakishindikana, basi inaonesha huyu mwanamke yupo tayari ndoa ivunjike, hivyo awe na "PEACE OF MIND" kwa msimamo wake...! Amtafute mke mwingine, huenda huyo amekwishachukuliwa huko...!
 
Ukweli ni kwamba wanawake wengi kwenda kanisani, na kushinda na kukesha huko ni kukosa uwepo wa mume ndani ya nyumba. I mean kuwa wengi wetu tunaona kwenda kanisani na kuomba na kufunga ndiyo suluhisho la mume kuacha Uzinzi, nz pombe , na atajali familia. na tunaamini kuwa YESU ndiye atakaye mrudisha na kumbadili. LKN MWANAME ANAYEELEWA HUWA ANAJIRUDI NA KWENDA NA MKEWE KANISANI, HATIMAYE MKE ANAKUWA SAWA KIAKILI. HIVYO BASI ENYI WAUME ZETU TUPENDENI NA TUJALINI. HATUTAKWENDA KUKESHA NA KUSHINDA KANISANI. WE NEED PEACE OF MIND.
 
Preacher... you dont have to be uni-dimensional kamwe; sidhani kama kwenye hii thread tunaongelea pombe, sigara, uzinzi au mipira... we are talking of the family na nadhani unaelewa vyema kuliko mistari miwili au mitatu uliyoamua kui-quote kuhalalisha mtu kukaa mbali na familia yake full time

we dont condemn mtu kusali, but we condemn extremism kiasi cha kuacha jukumu mama la familia

Je yesu alishinda kanisani kutwa?
Ukishinda kanisani utasaidia vipi kuwavuta waliopotoka?
je wewe unashinda kanisani?
je tukishinda kanisani tutakula mbao?
Je unadhani kama unashinda kanisani kutwa wakati unahukumu kila aliye nje ya kanisa ndivyo tulivyofundishwa?

MImi si strong muumini kama unavyoji-portray wewe lakini kumbuka [i read it somewhere though] kwamba bible imeandika neno wisdom mara nyingi kuliko neno salvation!!!!

ask your self why?

DN

1. INAONYESHA WAZI HUYU MAMA HAFANYI KAZI - OTHERWISE ASINGESHINDA KANISANI BALI KAZINI AU KWENYE BIASHARA -

2. KWENYE MAKANISA KUNA VIPINDI (SPECIAL) VYA KUFUNGA NA KUOMBA - NA HUYU MAMA ANAENDA KWENYE HIVI VIPINDI

3. MIMI SIKU ZA JUMAPILI - NDIO NASHINDA KANISANI - KWANI NDIO SABATO YANGU YA KUMTOLEA MUNGU IBADA.

4. HUYU MUME WAKE ANAONEKANA HAPENDI KANISA KABISA WALA MAPAMBIO (SHORT CHOROUSES) ZA KUMSIFU MUNGU - NDIO MAANA ANALALAMIKA - ANAPENDA MKEWE AENDE KWENYE TAARABU, NGOMA AU??
5. UNASOSEMA HII NI ISSUE YA KIFAMILIA - KUMBUKA HUWEZI KUSEPARATE - FAMILIA NA MUNGU KWANI MUNGU NDIO MWANZILISHI WA FAMILIA (SOMA KITABU CHA MWANZO KWENYE BIBLE)

6. HAKUNA KANISA LENYE IBADA KILA SIKU - ASUBUHI HADI JIONI KILA SIKU - ILA KANISA LINAKUWA WAZI - KILA ATAKAYE KWENDA KUOMBA ANAWEZA - MUME HUYU ATUELEZE MAZINGIRA YA NYUMBA YAKE KUNA UTULIVU WA MKEWE KUFANYA IBADA???
KABLA YA KULAUMU MKE ANASHINDA KANISANI - ZIPO SABABU YA YEYE KUFANYA HIVYO NA MWISHO KABISA MTU ANAYECHUKIA NYIMBO ZA MUNGU ANA MAPEPO - ANAHITAJI DELIVERANCE - MKE HUYU ASHINDE KANISANI ILI MUNGU AMFUNGUE MUMEWE ASIYEPENDA KANISA ... BWANA YESU ASIFIWE SANA - AMEEEEEEEEEEEEEEEEEN!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kaka angalia mwenenndo wa mke wako, maana kwa kuinyima familia muda mwingi anamkosea Mungu. Mimi na wasi wasi sana na makanisa haya ya upako wakati mwingine wanakuwa na mabo yao mengine akja home anapotezea kwa mapambio. Muishi na wake zenu kwa akili. anatakiwa akuheshimu huyoooo azitii mamlaka zako maaana wewe ni head.
 
Hilo sio kanisa bali ni kitu kingine. Vp mchungaji wake ni yule wa viti maalum CCm asiye ishi na mume?

Isije ikawa ni UPAKO maana jamaa wa Upako wanamega wake za watu kwa kwenda mbele.
Hebu chunguza taratibu utakuta ana uhusiano wa kariiibu na huyo Pastor.Ukiona hivyo ujue kumegwa ndio kunamtaahirisha . Pole Mkuu
 
Hapa naona hakuna cha kujadili, suala ni huyo mume akae chini na mkewe waulizane na kujibiana sababu za mke kushinda kanisani na kutelekeza familia kwa muda wote huo, na kama anaijali familia yake basi angewashawishi kuwa waende wote kanisani na si kuwaacha nyumbani wahudumiwe na dada! Na istoshe huko kanisani kuna kipi spesho cha kumfanya apang'ang'anie kiasi hicho kwa sbb kama ni ibada pekee yatosha nusu saa kwa siku au basi ujitoe siku nzima katika juma moja yatosha kabisa kumshukuru Muumba na kumuomba au kutubu dhambi zako kwa sbb kila jambo jema ulifanyalo katika maisha yako ya kila siku tayari ni ibada tosha kwa Muumba wetu! Huyu mama ana lake jambo, kama mumewe hatajali apoteze muda wake na kufatana nae japo wiki moja tu atagundua kinachoendelea!
 
Daily new stories are coming out. Horny priests continues to play havoc with followers from children molestation to having affrairs with wifes - just a matter of time you will hear men are also in danger !!! Keep away for you and your family safety.
 
Mahali fulani biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Katika habari hii ya huyu mwanamke mie niseme kwamba kwenda kanisani siyo shida. Tatizo kubwa inawezekekana imekosekana hekima na kiasi katika jambo hili; kila mwanadamu anapaswa kujua kuwa anawajibika kwa pande tofauti kwa Mungu, mme/mke, familia, kanisa, mwajiri n.k Katika kuwajibika huku ni lazima mtu utafute namna ya kuhakikisha kuwa kila upande unautendea haki.

Ninalojua ni kuwa hata katika makanisa haya yanayosemwa vipo vipindi vilivyokubalika katika wiki (Zipo siku, yako masaa) kwa hiyo sioni shida ya mke wangu kuhudhuria vipindi vya kanisani hata kama vinapelekea yeye kufika nyumbani saa mbili usiku mara tatu kwa wiki. Linapokuja suala la maombi maalum kama ni ya kanisa ninakuwa ninaelewa na nampa huo uhuru ambayo mengine yanaweza yakawa ya kushinda kanisani au kukesha usiku. Haya siyo ya kila siku ni ya kipindi maalum na kwa kuombea mahitaji maalum. Kwa mme anayejali maisha ya kiroho ya mke na familia sioni shida kumruhusu na ukawa na amani kwa hili.

Shida iliyopo hapa ni kwa sababu mme siyo sehemu ya kanisa hili, hivyo hajui ibada zikoje na haya maombi ni ya namna gani. Kwa hiyo ningemshauri kama anampenda mke wake na kumpenda Mungu wake, ajaribu kuwa sehemu ya kanisa hili ili ikiwezekana hata kwa maombi mengine wawe wanaongozana kwenda kuomba.

Kwa mwanamke naye, anapaswa kujua kuwa katika mambo yote anapaswa kuwa na kiasi, hakuna sababu ya kushindwa kuhudumia familia kwa kisingizio kuwa uko busy kanisani. Na katika mambo yote inabidi aishi maisha yenye ushuhuda ambayo hayataleta maswali kwa familia na watu wengine, kwani wanaweza kufikiri kuwa inawezekana kanisani yuko mwanaume mwingine uliyempata na ndiyo maana haujali familia yako.
 

thanks kwa maelezo, but kuna maswali hayajajibiwa na tukawa tunahukumu
je mtoa post amesema kwamba huyo dada anaenda kanisani jumapili tu?
je kwa jamaa kusema akirudi ni mapambio tu, ina maana hapendi? what if he doesnt mind as long as iko within the limit?
I will never separate family na faith/ibada/mungu kwani dini zote zatuelekeza hivyo na wazazi hutufunza hivyo, lakini naamini kwamba a question of balance ni key. sisi husali kila siku kama wanafamilia nyumbani, jee hiyo haikubaliki, hadi tukeshe kanisani?
Je kwa maelezo ya mtoa hoja, amesema huyo mama yuko kwenye mafungo?
Kama mkatoliki naamini kuna mafungo lakini pia naamini kwamba haiwezekani watu kukesha muda wote kanisani ndio njia ya uzima; kwani suala la malezi ni wajibu pia, na sikumbuki mtu aliambiwa aache watoto akeshe kanisani! kwani ni mpumbavu tu anaweza kuvuruga nyumba yake

sijui mafundisho ya ndoa ya siku hizi au ya wana ngurumo yakoje, so i may be wrong
 
Huyu mama anayeshinda kanisani, hata tatizo bali ni jicho la watu wengine.

Kwa kuamua kumtumikia Mungu ana wito mkuu zaidi, kuliko hata kumtumikia mume au jambo jingine lolote. Bwana Yesu alisema, anayetaka kunifuata mimi ajikane mwenyewe!
Hili ni la msingi sana, ila kwa watu wa nje watasema , ooh hahudumii mume , watoto, nk nk, acheni visingizio, mtu akimtafuta Mungu wake, acheni amtafute Mungu wake. Ni Yesu ni zaidi ya mume,watoto, nk.

Mbona Ibrahim alimtoa mwanawe Isaac kwa ajili ya Mungu. Mungu ni zaidi ya vyote, kuna haja ya kuwa makini na ndoa nyingine, kwani zinatumika na adui kuwazuia watu wasimtumikie Mungu, ukiuliza sababu ataachwa na mume!!!! Mbona mume ni kitu cha kupita tu?
 





NDUGU WAPENDWA KUSUDI LA MUNGU KUTUUMBA SISI NI ILI TUPATE KUMCHA YEYE MUNGU USIKU NA MCHANA, NA KAMA BABA YETU ADAMU NA MAMA YETU HAWA WASINGEFUKUZWA KTK BUSTANI YA EDENI KWA KUKOSA,HIYO NDIO INGEKUWA KAZI YETU SAWASAWA NA KULE MBINGUNI, HIVYO KUMCHA BWANA HAKUNA WAKATI, BALI PIA TUMEPEWA MAJUKUMU MENGINE BAADA YA KUKOSA ,KWAMBA KWA JASHO LETU TUTAILIMA NCHI ( TUTAKULA )mtoa hoja amesema MAMA AKITOKA KAZINI ANAISHIA KANISANI NAPENDA KUKUMBUSHA YAFUATAYO:
1.KWA HUYO MKE " 1TIMOTHEO 5:8 '' LAKINI MTU YEYOTE ASIYEWATUNZA WALIO WAKE,YAANI WALE WA NYUMBANI MWAKE HASA ,AMEIKANA IMANI ,TENA NI MBAYA KULIKO MTU ASIYE AMINI''
2.JE MUME ANA UPENDO KWA FAMILIA??!!! ANAMWAMINI MUNGU??? ANA HOFU MBELE YA MUNGU??? KAMA HAYO HANA NENO LA MUNGU LINASEMA:
" TORATI 28:30 "UTAPOSA MKE NA MUME MWINGINE ALALALA NAYE, UTAJENGA NYUMBA USIIKAE, UTAPANDA MIZABIBU USITUMIE ( USIFAIDI ) MATANDA YAKE.
3.WAKE WENGI WAMEPELEKEA WAUME ZAO KUWA WALEVI NA MALAYA KWA MIDOMO YAO KWA KUKOSA UVUMILIVU PIA WANAUME WENGI KABISA WEMETEKWA NA MAKAHABA NA ULEVI WAKAZISALITI NDOA ZAO NA KUSABABISHA WAKE ZAO WAJAE HOFU NA KUTAFUTA MSAADA WASIUPATE HIYO HUJISALIMISHA KWA BWANA MUNGU ASIYESHINDWA NA CHOCHOTE.
 

i love you!
 

umeongea vyema mwishoni, lakini kuna maneno mengine hapo, bora usingechangia kabisa kwasababu unakuwa kama unapromote watu wasiwe wanaenda kanisani. imefika mahali tuenende kwa roho na wala si kimwili tena, pamoja na kwamba Mungu ametupatia akili na utashi wa sisi wenyewe kuamua mambo, lazima tujue ya kuwa, akili ya kibinadamu, hekima za kibinadamu kamwe haziwezi kuwa juu ya kile ambacho Mungu amesema. NASAPOTI ASILIMIA MIA huyu mama aendelee tu kwenda kanisani, huko atapata pumziko la moyo, na Mungu atamsaidia kwa chochote anachokitafuta. unaposema mtu asiyewakumbuka wa kwao ni mbaya kuliko hata yule asiyeamini, hauna uhakika kama ni kweli huyo mama amewasahau wa kwao. umeanza kumhukumu tu bila kujua kama huwa anaweka mazingira mazuri kwaajili ya watoto wake kwanza ili pale atakapokuwa ameenda kanisani wasipate shida. kuna makanisa mengine hapo Dar es salaam, ibada zao zinaanza saa kumi na moja, mfano ni pale ubungo kwa ufufuo na uzima.nasikia wamehamia kawe kwa sasa. watu wanafunguliwa na wanapona mambo mengi, wanaacha kwenda kwa waganga wa kienyeji wanamtegemea Mungu. inawezekana huyu mama huwa anakuja kusimama hapo kupata ibada kabla ya kwenda home, na ibada haichukui muda mrefu. so instead of judging her kwamba amesahau wa kwao, ungesikiliza kwanza upande wa pili, usiamini kila mada inayoletwa hapa yenye upande mmoja biased, tayari ukaanza kuponda mambo ya Mungu kwamba wanaoenda kanisani wamesahau wa kwao, I HOPE HAUTARUDISHA ROHO ZA WATU WENGINE WATAKAOSOMA MSG YAKO HAPA NYUMA, kwasababu kwa ufahamu ninaouona kwako wa neno la Mungu, utadaiwa wewe. acheni wanaomtafuta Mungu wamtafute wapendavyo, na ninyi msiomtafuta Mungu endeleeni na dunia yenu...siku inakuja wale waliokuwa wanaonekana wapumbavu watakapoonekana wana akili. watu wengi wametanguliza dunia mbele kuliko hata mambo ya Mungu, wametoa muda kidogo sana kwaajili ya Mungu, wakatoa muda mwingi sana kwaajili ya dunia. na watu wengine bado wanasapoti, ati mtu awe anakumbuka wa kwao, are we sure kwamba hakumbuki wa kwao? wakati issue hapa iko wazi, huyu mwanaume anampiga vita huyu mama asiende church, ndo tatizo hapa, na wala si kusahau watoto. hakuna mlokole anaesahau watoto wake nawaambieni, hivyo naomba usijiunge na watu wanaowachukua watu waliookoka, ambao siku zote msg zao huwa ni kuponda na kudharau watu waliompa Bwana Yesu maisha yao, labda kama na wewe uko kwenye kundi hilo....usijiunge kwenye kundi la wapinga kristo, labda na wewe kama ni mpinga kristo. acha watu wamwabudu Mungu, hata kama ni masaa yote, unayajua mazingira ambayo huyo mama na familia yake wanaishi?unamjua huyo mume alivyo?

pengine mume mlevi wa kubebwa kwenye tolori, mzinzi na ameshaleta ukimwi ndani ya nyumba kwa mama watoto aliyekuwa ametulia yeye akaenda kuchuma ukimwi kwa machangu doa huko baaa, sasa mama wa watu anahangaika na mzigo ambao hakuuchuma yeye. you never know, don'g judge kabla ya kufikiria kuhusu upande wa pili, hasa katika mambo ya Mungu, utajikuta umetumika na shetani hivihivi. ndo ushauri wangu huo kwako.
 

Hivi,shemeji za masiku lakini?

Kwenye kitabu cha Mwanza si imeandikwa ' tazama mtu atamwacha baba yake na mama yake, nye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja"...sasa huyo mke anasoma biblia gani? mbona hilo andiko halioni wakati Yesu pia alikazia kwenye agano jipya?
 

anasoma biblia hio hio,imesema atamuacha baba na mama yake haikusema atamuacha na mungu wake,mwacheni mama watu afanye lililo heri...
 
Hii tabia ya watu "kushikwa vibaya" na imani imekuwa kubwa sana siku hizi jamaa ikiwezekana ampeleke mkewe wa wataalam wa magonjwa ya akili(hasa Msongo)
Muhimbili. Tatitzo linatibika, kuna watu nawafahamu wamefunguliwa kutoka kwenye hali hiyo.
 
mcha Mungu hutenda matendo mema, inakubidi uulizane na mkeo,

kwa mwili tunayafanya maovu, kwa roho tunamwabudu Mungu

basi yashinde ya mwilini ili umwabudu Mungu katika roho na kweli.

maana imeandikwa ,,,basi nasema enendeni kwa roho maana hamtazishinda

tamaa za miili yenu,,,,maana yake enendeni kwa kumhofu Mungu ili kuishinda dhambi
 
Mh...

Mungu ni mmoja mwenye nafsi tatu nae alituumba kwa mfano wake, akatuagiza tuyashike na kuyatenda yale yaliyo mema..na tukijua wajibu wetu na kuufuata.

Tafsiri ya maandiko katika Kitabu cha Mungu ni pana na wawezao kutafsri ndio waliofunuliwa kuwavuta hata wale ambao imani na matendo yao yanadhirishwa kwa mambo ya mwili na roho.

Pengine dini zetu zinatafiriwa kama "Bangi" ambayo ikikulevya sana, waweza kuchangaya ya "Kaisari" na yale ya "MUNGU"...Ipo mistari inaonya:

"Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika masunagogi, na kuchukua nafasi za heshima katika karamu. Huwanyonya wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu. Siku ya hukumu watapata adhabu kali!"

"Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa! au Yupo pale! msimsadiki. Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu, kama ikiwezekana. Lakini ninyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea"

Je, yatupasa kushika imani ipi, ya Kristu au ya Madhehebu na Makanisa???..
 
inawezekana kabisa mchungaji akawa anatembea na huyo mwanamke......
wachungaji hawa wa makanisa yanayoibuka kila siku kwa kupenda wanawake hao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…