Ajaribu haya hapa;
1. Aangalie kwanza upande wake kwa kutafuta mapungufu yake mwenyewe; kama vile lack of polite language, kuwa na affair nje, kutomwandaa mwenzake ipasavyo nk. then arekebishe kabla ya yote.
2. Akae na mkewe chini na kujaribu kumweleza (in a serious intention) yanayomsibu na madhara ambayo yanaweza kutokea katika ndoa kwa ajili hiyo.
3. Atambue tu kwamba life has no a fixed fomula to apply, sometimes force is fruitful and sometimes freedom, so let him try to apply whichever is seem to be so and available by the time and situations. Too much freedom might be harmful also.
4. Inaonekana mahusiano yao hayakuwa na background imara, alipaswa kuwa na walau consultant juu ya mahusiano yao tofauti na mchungaji, paroko nk.
5. Asisahau haya katika maombi yake ya kila siku, hivyo ajaribu kuyakabidhi kwa Mola wake atie marekebisho kwa mkewe.
6. Ajaribu kuchunguza kwa undani na taratibu sana, huenda mwenzake anawajibika huko nje; hii ni feeling niliyoipata kwa kiwango kikubwa sana.....!
7. Kama anaweza kuongea na mama mkwe wake basi ayaeleze haya, kama hawezi amtume hata mtu wa kuongea naye ili ajaribu kuzungumza na bintiye na kumuelewesha kuwa hakuja kuimba kwaya, bali yupo kwenye ndoa. Mara nyingi wake zetu wanareflect wanachoshauriwa na mama zao.....!
8. Aache mara moja kufua na kupasi nguo, kudeki, kupika, na kumpakua chakula; provided mkewe yupo na ni mzima wa afya kabisa. Akiweza kufanya hivi mkewe atafanya maamuzi yatakayoashiria alichojiandaa nayo; kama vile kumleta mwanaume ndani, kuondoka na kurudi kwao, nk.
9. Ampunguzie haosegirl kazi na kumwekea mipaka ndani ya nyumba; kama vile kutofika chumbani kwao, kupika siku za weekend, kufua nguo zao, nk. Abaki tu kufua nguo za watoto, kudeki sehemu zingine za nyumba (with exception of master bedroom yao).