ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
nakumbuka rafiki yangu wa kike alikuwa na gari ambayo ilikuwa imenunuliwa na mumewe (but kwa mkopo wa mama) na gari hiyo ikaandikwa jina la mdogo wake mama ambaye aliwagaia exemption yake. Baada ya muda ile gari Mr akaamua kuiuza ila kwa makubaliano kuwa anataka amnunulie mkewe gari ya kutembelea- (huyo Mr naye analo gari lake-kwa jina lake) sasa after kununua ile gari ya wife akaandika jina lake Mr- bila kuweka Mr and Mrs wala jina la mtoto!! Kama una mke mwenye kufikiria mbali ni lazima ataona ubinafsi hapo.
So mimi simlaumu kabisa huyu mama ila namshauri tu atafute vya kwake- hivyo vya mumewe afight viwe mali ya wana wao.
Kwani ukiweka Mr & Mrs Ngoshwe ina maana mkiacha au kutengana hilo neno "MRS" linatakusaidia? Kama nilikuwa na ma "MRS" wengine chochi wakaibuka na kusema "mimi ndo MRS mwenyewe" utabisha kama jina lako halipo?. Cha msingi ni kuona kuwa mali na matakataka mengine yote ni ubatili tu na utu wa mtu ni zaidi ya hayo. Mke au Mume ambaye ana anza kuzungumizia masauala ya mali binafis katika ndoa ni hatari sana. Jaribu katika maisha yako yote kutafuta jambo liliko jema ambalo ni kuwaachia watoto urithi wa elimu ambayo haitapotea kamwe, nyumba na gari si urithi mwema!.
Ni busara pia hata kwenu wanawake, kutuhimiza tuzae watoto wa kutosha na kusomesha vizuri, manake ikiwa mtoto amesoma kama mumeo akikuona kimeo na kukuacha, mwanao msomi ataweza kukusaidia ikiwemo hata kukujengea hiyo nyumna na kukununulia hilo kwa jina lako!.