Mke amwagiwa petrol na kuchomwa moto....

Mke amwagiwa petrol na kuchomwa moto....

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,111
Reaction score
34,943
​
Janet.jpg


Janet Udegba.​
attachment.php

Janet na Kehinde.



NINI tafsiri ya uelekeo wa dunia kutokana na matukio ya kutisha? Upo ukatili mkubwa umefanyika nchini Nigeria ambapo mume amemwagia mkewe mafuta ya petroli na kumchoma moto.

Kehinde Adesamuye, 39, mkazi wa Lagos, Nigeria anadaiwa kumchoma kwa moto wa petroli hivi karibuni mkewe Janet Udegba, 35, katika Mtaa wa Ikotun jijini Lagos baada ya kuwa na hasira kutokana na kuhisi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine.

Janet alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa katika eneo lake la biashara akiuza vyakula kabla ya Kehinde kufika hapo usiku huo na kumwagia petroli mgongoni kisha kuwasha moto kwa kutumia kibiriti.

​
Hata hivyo, alisema Wanigeria hawatamwachia huru Kehinde kutokana na kile alichokifanya. Akisimulia mgogoro wao, anasema:

“Mume wangu amekuwa na wivu daima. Amekuwa na tabia ya kunipiga kila wakati. Nimejaribu mara nyingi kuachana naye lakini huwa ananitishia kuwa lazima atanidhuru.


Niliendelea kuishi naye kwa kuwa nilikuwa na hofu ya maisha yangu, aliwahi kuniambia kuwa sitaweza kutoroka hata siku moja.
Ikeja20120916000401.jpg
Janet.​
“Serikali lazima ihakikishe kuwa Kehinde analipa kwa kile alichonifanyia. Mimi ni yatima, ninafanya biashara ya vyakula ili niishi. Sasa nimetumia pesa zangu zote kwa ajili ya matibabu. Kwa kweli kwa sasa nahitaji msaada,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi.


Kehinde alijaribu kutuma rafiki zake ili wamwombee msamaha kwa Janet lakini alikataa. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili.



 

Attachments

  • KehindenaJanet.jpg
    KehindenaJanet.jpg
    31.8 KB · Views: 286
Wanawake ni MAMA ZETU lakini AKILI zao wanazijua wenyewe; huyu angetayari haya yote yasingemtokea sasa ona. Hata kwa kumuangalia tu jamaa huyu mwanaumw ni ZIRAELI MTOA ROHO ZA WATU....
 
nawza sma huu n ukatili ambao haujawahi onekana ila mara nyng c tunaambiwa kwaba tusiamue ktu bla uchunguz ss ona kinach mkta jamaa hpo....
 
nasikita ana, ila kuna ile ya Yule Bint wa Ethiopia aliye mwagiwa Tindikari, ile ndo balaa
 
Huyu ni bint wa Kiethipoia alie mwagiwa Tindikali na Mpenzi wake, baada ya Bint kumchomelea

_42732273_acid203.jpg
 
Back
Top Bottom