dotnet
JF-Expert Member
- Mar 5, 2013
- 393
- 153
- Thread starter
- #61
Umesema vema sana ndugu yangu. Ushauri wako huu naufanyia kazi na nitarejea hapa.Washauri wengi hapa, ukiondoa wale walioshauri kuhusu vyakula, wamekushauri kuchukua hatua ya mbele sana kuliko ile unayopaswa kuchukua sasa ambayo ni rahisi na ipo ndani ya uwezo wako. Kama una low sperm count unachotakiwa kufanya ni kutokufanya tendo la ndoa mara kwa mara, ili sperm zijae ziwe nyingi ndo ufanye tendo la ndoa na ndo uweze kumrutubisha huyo mkeo. Kula vyakula vya mboga za majani, wanga (wali, ugali, mikate), matunda kwa wingi, EPUKA vyakula vya mafuta mengi (fat) pia fanya mazoezi mara kwa mara na kunywa maji ya kutosha kilasiku (angalau lita moja ya maji kwa siku - siyo chini ya hapo). Aliyekushauri kunywa maziwa lita moja/zaidi kakudanganya. Maziwa kikombe yanatosha. Yakizidi yatakujazia mafuta mwilini na kukuweka hatarini kiafya. Pia EPUKA vinywaji vya kulewesha vya aina yeyote ile. EPUKA pia vitu kama soda na kahawa. Ukiweza hata chai. Maana hivi vina kemikali inaitwa "caffeine" ambayo inapunguza nguvu ya mbegu zako. Kunywa maji tu Kaka. Kaa bila kufanya tendo la ndoa kwa muda wa kama mwezi mmmoja (wakati unaendelea kutekeleza ushauri huu) ndo ufanye. Atapata ujauzito bilashaka. Hata usihofu, low sperm count siyo tatizo kubwa hata kidogo. Ukiwa na low sperm count bado unaweza kumpa mwanamke ujauzito kwa njia ya asili (yaani tendo la ndoa).