Mke achoma moto nyumba baada ya Mumewe kuleta mwanamke mpya

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mwanamke mmoja wa kijiji cha Emaondo, katika jimbo la Kakamega nchini Kenya amechoma nyumba yake moto baada ya mumewe kurudi nyumbani na mwanamke mwingine.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea Jumatatu, ambapo mume huyo, Samuel Indeche, 25, alikwenda na mwanamke huyo nyumbani na kumtambulisha kwa mkewe kuwa huyo ni mke wake mpya.

Hata hivyo, mara tu baada ya wawili hao kuondoka, mke wa Indeche alichoma moto nyumba yao na kisha kutokomea pasipojulikana na hadi sasa polisi wanaendelea kumtafuta.

Indeche na mwanaye wa mwaka mmoja walilazimika kulala nje huku wazazi wa bwana huyo wakieleza kuwa kwa mujibu wa desturi zao, mtoto wao huyo ataendelea kulala nje na mwanaye kwa siku tatu mfululizo, ndipo atakapopewa hifadhi.

=====

1581421489204.png

A woman in Emaondo village, Kakamega County, on Monday burnt down her house after her husband brought home a new wife.

The woman’s husband – Samuel Indeche, 25 – is said to have showed up in the company of another woman whom he introduced as his new wife.

However, as soon as they left, his first wife torched their house before later fleeing and is presently being sought by police.

Mr. Indeche and his one-year-old son were reportedly forced to spend the night out in the cold.

Mr. Indeche’s parents, Francis Indeche and Paulina Amwayi, have since told Citizen Digital that – according to tradition – he and his child will spend three nights under a tree before they are allowed entry into any other house.

Source: Citizen TV
 
Cha kusikitisha utakuta huyu mwanamke ni wale type ya imani kali, wanasoma injili lakini hawaielewi.

Isaya 4:1

Wakati huo wanawake saba watamvamia mwanamume mmoja na kumwambia, “Chakula na mavazi tutajitafutia wenyewe, lakini wewe utuondolee aibu yetu, uturuhusu tuitwe kwa jina lako.”

Unforgetable
 
Kama walianza wote shida raha kisha anakuja kuingia mwanamke mwengine hajavuja jasho kiulaini tu hata mimi nafanya hivyo(joke)
 
Indeche na mwanaye wa mwaka mmoja walilazimika kulala nje huku wazazi wa bwana huyo wakieleza kuwa kwa mujibu wa desturi zao, mtoto wao huyo ataendelea kulala nje na mwanaye kwa siku tatu mfululizo, ndipo atakapopewa hifadhi.
 
That woman is now homeless

Wanawake hufanya mengi zaidi ya hapo ukiwafanyia dharau lililopitiliza, kuna huchinja mume, na kujiua kabisa. Labda nyie wanawake wa Bongo hamna wivu, kama vipi unitafutie wanne kama wewe ili niachane na hawa Wakenya ambao hawataki tusambaze mbegu na upendo.
 
nyie wakenya sijui kwanini, wanawake zenu wanawaweza kweli kweli, na huwa, mnapigwa makofi kabisa mkiletaga utani!
 
Nawashangaa wanaomkashifu Samuel kwa kuleta mke mwingine nyumbani. Rais Uhuru Kenyatta alitia saini sheria mpya kuhusu ndoa mwaka wa 2014. Sheria kwa sasa haina limit ya idadi ya wake ambao mwanaume anaweza akaoa. Tena wanasheria wa Kenya walitupilia mbali kifungu kwenye sheria hiyo ambacho kingemshurutisha mwanaume kupata kwanza idhini ya mke wa kwanza.
 
Lakini hakupaswa kumshtukiza kihivyo, yaani uibuke na mwanamke ghafla na kutangaza kwamba ndiye mkeo wa pili, tegemea mtiti wa akina Wanjiru na Akoth.
 
Lakini hakupaswa kumshtukiza kihivyo, yaani uibuke na mwanamke ghafla na kutangaza kwamba ndiye mkeo wa pili, tegemea mtiti wa akina Wanjiru na Akoth.
Huyo mke wake naye ni mshamba kupindukia, kiherehere chake kilivuruga kabisa mipango ya Samueli. Yaani hata hangengoja wacheze kamechi threesome kabla ya kuteketeza nyumba?
 
Back
Top Bottom