Mkazo zaidi unatakiwa kuwekwa kwenye Soko la Ndani katika kuendeleza Uchumi

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
72
111
Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito wa kuweka msisitizo kwenye kuunda mtindo mpya wa maendeleo, ambapo soko la ndani na solo la nje yanahimizana, lakini soko la ndani kuwa njia kuu ya kuendeleza uchumi. Rais Xi amesema hili ni “chaguo la kimkakati” kwa China kwenye ushirikiano wa kimataifa na ushindani wa kimataifa.

Rais Xi amesema China itaendelea kufanya mageuzi kwenye upande wa uzalishaji na kuhimiza mahitaji ya ndani, na kusisitiza kuwa uzalishaji, usambazaji, mzunguko na matumizi vitategemea zaidi soko la ndani, lakini mzunguko wa “pande mbili” utategemea zaidi soko la ndani na masoko ya nje. Rais Xi pia amesema soko linatakiwa kuwa na mchango mkubwa katika mgawanyo wa raslimali, na serikali inatakiwa kuweka mfumo wenye kutabirika wa maendeleo, na kulinda usimamizi wa haki miliki. Rais Xi ametoa mwito wa huo, wakati China inakusanya maoni kutoka kwa wananchi kuhusu mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mambo haya mawili, yaani mwito wa Rais Xi kuhusu kuendeleza soko la ndani, na kukusanya maoni na mapendekezo kwa ajili ya mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano, yamekuja wakati hali ya uchumi wa dunia inaendelea kuathiriwa na madhara ya virusi vya Corona. Sekta nyingi za uchumi hasa zile zinazohusiana na biashara kati ya nchi na nchi, zinaonekana kudorora na haijulikani ni lini hali ya uchumi itatengemaa na kurudi katika hali ya kawaida.

Kwenye mazingira yasiyoeleweka kama ya sasa, umuhimu wa soko la ndani unazidi kuonekana. Kutokana na maendeleo ya kiuchumi ya China kwa muda wa miongo minne, China imekuwa moja ya nchi zenye kundi kubwa la watu wa tabaka la kati ambao mapato yao yanazidi kuongezeka. Hali hii ni mazingira mazuri kwa China kuweza kuendelea na mageuzi ya muundo wake wa uchumi. Hata hivyo kutokana na uwezo wake mkubwa kwenye uzalishaji, China itaendelea kuwa sehemu muhimu ya mnyororo wa usambazaji wa bidhaa duniani, kwa hiyo soko la nje litaendelea kuwa muhimu kwa uchumi wa China.
 
... kulinda usimamizi wa haki miliki. ... na kukusanya maoni na mapendekezo kwa ajili ya mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano,
kwenye uzalishaji, China itaendelea kuwa sehemu muhimu ya mnyororo wa usambazaji wa bidhaa duniani, kwa hiyo soko la nje litaendelea kuwa muhimu kwa uchumi wa China.

China na kulinda hakimiliki kwenye sentensi moja :D

Wanakusanya maoni? Mbona tayari keshatoa hitimisho!
 
Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito wa kuweka msisitizo kwenye kuunda mtindo mpya wa maendeleo, ambapo soko la ndani na solo la nje yanahimizana, lakini soko la ndani kuwa njia kuu ya kuendeleza uchumi. Rais Xi amesema hili ni “chaguo la kimkakati” kwa China kwenye ushirikiano wa kimataifa na ushindani wa kimataifa.

Rais Xi amesema China itaendelea kufanya mageuzi kwenye upande wa uzalishaji na kuhimiza mahitaji ya ndani, na kusisitiza kuwa uzalishaji, usambazaji, mzunguko na matumizi vitategemea zaidi soko la ndani, lakini mzunguko wa “pande mbili” utategemea zaidi soko la ndani na masoko ya nje. Rais Xi pia amesema soko linatakiwa kuwa na mchango mkubwa katika mgawanyo wa raslimali, na serikali inatakiwa kuweka mfumo wenye kutabirika wa maendeleo, na kulinda usimamizi wa haki miliki. Rais Xi ametoa mwito wa huo, wakati China inakusanya maoni kutoka kwa wananchi kuhusu mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mambo haya mawili, yaani mwito wa Rais Xi kuhusu kuendeleza soko la ndani, na kukusanya maoni na mapendekezo kwa ajili ya mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano, yamekuja wakati hali ya uchumi wa dunia inaendelea kuathiriwa na madhara ya virusi vya Corona. Sekta nyingi za uchumi hasa zile zinazohusiana na biashara kati ya nchi na nchi, zinaonekana kudorora na haijulikani ni lini hali ya uchumi itatengemaa na kurudi katika hali ya kawaida.

Kwenye mazingira yasiyoeleweka kama ya sasa, umuhimu wa soko la ndani unazidi kuonekana. Kutokana na maendeleo ya kiuchumi ya China kwa muda wa miongo minne, China imekuwa moja ya nchi zenye kundi kubwa la watu wa tabaka la kati ambao mapato yao yanazidi kuongezeka. Hali hii ni mazingira mazuri kwa China kuweza kuendelea na mageuzi ya muundo wake wa uchumi. Hata hivyo kutokana na uwezo wake mkubwa kwenye uzalishaji, China itaendelea kuwa sehemu muhimu ya mnyororo wa usambazaji wa bidhaa duniani, kwa hiyo soko la nje litaendelea kuwa muhimu kwa uchumi wa China.
Sawa.
 
Back
Top Bottom