Ni nini hasa kinafanya Marekani kujaribu mara kwa mara kuzungumzia vibaya uchumi wa China?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,062
1,071
1720422658314.png


Marekani inaonyesha dalili za kesi yake sugu ya wasiwasi juu ya China wakati ikitumia vyombo vya habari na maoni ya umma kuchafua maendeleo ya China kwa kutumia maneno kama “kuanguka kwa China,” “China kileleni” na “uzalishaji wa kupita kiasi wa China.”

Ni kwa nini basi maendeleo ya China yanazua wasiwasi mkubwa kwa Marekani na kuifanya kuchukua msimamo mkali zaidi wa upande mmoja? Na ni nini wanasiasa wa Marekani wanajaribu kutimiza kwa kuitangaza China vibaya na kuzuia maendeleo yake? Marekani imefanya propaganda nyingi kuilenga China, ikitumia mamlaka yake katika masuala ya kimataifa kuongeza wasiwasi wa kile kinachoitwa ‘tishio la China’ na kupuuza ukuaji wa China kama ‘uzalishaji wa kupita kiasi.’

Wakati Marekani inataka dunia nzima kufuata kitendo cha ‘kujitenga’ na China, hatua hiyo si kwa manufaa ya uchumi wa dunia, bali inachochewa na mahesabu yake yenyewe, ya ndani na nje ya nchi hiyo. Kwa upande wa ndani, uchumi wa Marekani unakabiliwa na changamoto nyingi kubwa, ikiwemo ongezeko kubwa la deni la umma, uzalishaji usiojitosheleza wa viwandani, na kuongezeka kwa gharama za maisha.

Kwa mujibu ya ripoti ya watumiaji iliyotolewa hivi karibuni na Chuo Kikuu cha Michigan, matarajio ya kupanda kwa gharama za maisha kwa mwaka mmoja nchini Marekani yamefikia kiasi cha juu zaidi katika miezi sita iliyopita. Mkurugenzi wa tathmini ya mawazo ya wateja Joanne Hsu anasema, watumiaji wameeleza wasiwasi wao kwamba kupanda kwa gharama za maisha, ukosefu wa ajira na riba kubwa ya mikopo vinaweza kuwa na mwelekeo mbaya katika miezi ya baadaye ya mwaka huu. Sasa wakati Marekani inashindwa kukabiliana na changamoto hizo za kiuchumi, iko tayari kutafuta mtu ama nchi ya kuhamishia lawama.

Stephen Roach, mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Yale anasema katika itabu chake kinachoitwa “Unbalanced: The Codependency of America and China”, kuwa China, ikiwa nchi kubwa ya pili kwa uchumi duniani, imeibuka na kuwa nchi inayotupiwa sana lawama na Marekani, na Marekani kuchukua nafasi ya nchi inayoonewa.

Baadhi ya wanasiasa wa Marekani pia wanatumia hisia za ndani kutetea kitendo cha kujilinda na kutumia mchezo wa ‘kadi ya China’ kwa ajili ya kushinda uchaguzi.

Hata hivyo, bila kujali ni ujuzi kiasi gani unatumiwa na Marekani katika kauli zake za kuichafua China, masuala ya msingi ndani ya nchi hiyo bado yapo, na matokeo yake ni kuongezeka kwa ukosefu wa uwiano wa kiuchumi, ukosefu wa haki kwa jamii, na viwango vikubwa vya chuki kwa raia wa kigeni. Kauli hizi za kuipinga China, pamoja na kushindwa kwa uongozi wa Marekani, kunaifanya nchi hiyo kuingia katika mzunguko mbaya ambao unachochea chuki kwa jamii, mgawanyiko wa kijami na mkingamo wa kisiasa.

Kwa kutia chumvi mtazamo wa ushindani na uhusiano wa pande mbili na uwezekano wa tishio la uchumi wa China, marekani pia inatafuta uungaji mkono kwa sera zake za kigeni za kujilinda na mikakati yake ya udhibiti, hususan katika sekta ya biashara.

Licha ya juhudi za kuzuia ushawishi wa uchumi wa China, mtandao wa biashara ya kimataifa wa China unaendelea kuongezeka kwa dhahiri. Nchi hiyo imekuwa mfanyabiashara mkubwa wa bidhaa duniani na mwenzi mkubwa wa biashara kwa zaidi ya nchi na sehemu 140, na kuchangia kiasi cha asilimia 30 ya ukuaji wa uchumi wa dunia. Zaidi, unyumbufu wa uchumi wa China katika ukosoaji wa Marekani na baadhi ya wenzi wake wa Magharibi unaonyesha kuhama kwa msingi kwa mienendo ya uchumi duniani.

Sasa dawa ya “wasiwasi wa China” unaoiandama Marekani iko wazi: kutoa kipaumbele katika kukabiliana na masuala ya kiuchumi ndani ya Marekani kupitia sera za kimkakati kuliko kuhamisha mawazo ya watu kwa kukashifu mwenzi mkubwa wa kiuchumi duniani.
 
Back
Top Bottom