Mkataba wa SportPesa: Hans Pope wa Simba SC abwaga manyanga

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,476
4,447
Simba walikuwa wanapitia kipindi kigumu sana sababu ya ukata wa pesa mpaka baadhi ya wachezaji walikuwa kwenye mgomo wakidai mishahara ,kila mtu ni shahidi wa hili.

Tukishuhudia namna mashabiki na wanachama wa simba wakilia mo mo mo kama vile Ng'ombe kwenye mkutano wakimshinikiza Dewji akubaliwe wakiamini shida zao zingeondoka ,kama kifuta jasho Deuji akatoa 100M pesa kwaajili ya usajili na hiyo ilikuwa ni pesa ya mchango tu "nje ya budget" na hiyo pesa ndio ilimleta Mavugo.
9c4a10212271bf565878d56e89b1ea36.jpg

Kulikuwa na mkataba wa awali Kati ya simba na Mo na ndio maana mishahara ya wachezaji,usajili nk ilikuwa inafanywa na Mo.

Ilikuwa busara Mo ashirikishwe.

IMG_6436.jpg

Poppe aachia ngazi:

IMG_6437.jpg

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe ameachia ngazi.

Habari za uhakika zimeeleza kuwa Hans Poppe ameandika barua ya kuachia ngazi akiona mambo yanaendeshwa ndivyo sivyo.

“Hans Poppe ameachia ngazi kwa kuwa hakufurahishwa na mlolongo ulivyokuwa hadi Simba kuingia mkataba wa SportPesa,” kilieleza chanzo.

"Hans Poppe ameandika barua kujiuzulu kwenye kamati ya utendaji, maana yake anaondoka automatically katika nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya usajili.

"Kilichomchukiza, kuna kundi lililoongozwa na Rais Evans Aveva na makamu Geofrey Nyange Kaburu, lilifanya mambo kimya kimya na Hans Poppe amesema hana Mo Dewji aliyeisaidia Simba mishahara naye hakushirikishwa hata kiungwana tu, hivyo amepinga hilo."
 
Mo the billionaire wasamehe Mikia wenzio kwa maana hawajui walitendalo. Ikiwezekana waongezee kama 500 M kwa ajili ya usajili ujao maana inaonekana mtakua wa Kimataifa in case Mbao wakiwaachia zile dk 10 za mwisho.
 
Simba walikuwa wanapitia kipindi kigumu sana sababu ya ukata wa pesa mpaka baadhi ya wachezaji walikuwa kwenye mgomo wakidai mishahara ,kila mtu ni shahidi wa hili.

Tukishuhudia namna mashabiki na wanachama wa simba wakilia mo mo mo kama vile Ng'ombe kwenye mkutano wakimshinikiza Dewji akubaliwe wakiamini shida zao zingeondoka ,kama kifuta jasho Deuji akatoa 100M pesa kwaajili ya usajili na hiyo ilikuwa ni pesa ya mchango tu "nje ya budget" na hiyo pesa ndio ilimleta Mavugo.
9c4a10212271bf565878d56e89b1ea36.jpg

Kulikuwa na mkataba wa awali Kati ya simba na Mo na ndio maana mishahara ya wachezaji,usajili nk ilikuwa inalipwa na Mo.

Mpira wa Tanzania unaenda kijima

Tumeshuhudia namna mchezaji ana kadi 3 za njano akicheza tena zaidi ya Mara 3 kesi hiyo hutokea unajiuliza hivi bench ya ufundi inajielewa kweli ,mchezaji husika anajielewa kweli

Referee ,kamisa hawana takwimu na data yaani shaghalabagala

Yanga inaomba mechi ya away dhidi ya Ndanda wacheze home na wanakubaliwa

Leo hii viongozi wa simba wanatoa kichekesho ,ni kama vile Barca wanamdhamini wao Qatar halafu wamgonganishe na Samsung na awekwe fent page bila ya Qatar kutaarifiwa?

Mo Fanya kweli i ili hizi timu zijue kuheshimu mkataba na ziendeshwe kisasa na kitaalamu

Pale mkataba unapovunjwa mapenzi unaweka pembeni akina Aveva wameonyesha unprofessional behaviour

Pesa ya mishahara,usafiri nk ziende bure ase
c83e9cc9ffa3ed42b2a784c9e31c4dc0.jpg
Mchezaji gani alicheza akiwa na kadi tatu? Unavuruga bandiko lako kwa kuleta ushabiki usiotija. Timu mojawapo ilifoji nyaraka kulazimisha kadi tatu, get your arcs together brother. Tusitetee ujinga.

Kwa hilo la Hanspope, kwani kujiuzulu kwake kutafanya mkataba na Spotipesa uvunjike na mkataba wa awali wa Mo kuwa honoured?
 
Ukiachana na kesi hii ya fakhi, simba walilalamikiwa walimchezesha Lufunga mwenye kadi na kesi iliamuriwa pia Azam bila shaka walilalamikiwa walimchezesha mchezaji mwenye kadi ndio maana nikasema kumekuwa na kesi zaidi ya mbili kwenye bandiko

Facts zipo real mkuu
 
Kila sekta nchi hii ni dili na usanii kwisha kazi.. Na hawa wa kwenye vilabu vya simba na yanga wangekuwapo toka miaka hiyo wala hivi vilabu visingekuwa na hata majengo yao wenyewe..
wanatamani wauze hata hayo majengo.
 
wanatamani wauze hata hayo majengo.
Ha ha ha yule Kassim Dewji wakati wa utawala wake aliingia mkataba wa pango na wafanyabiashara kwenye jengo la simba, mkataba wa miaka 30 akavuta mkwanja wake wa nguvu akaenda kununua maboti ya uvuvi na kufungua duka la michezo Jamhuri Street.. Wapangaji wanaendelea kulipa pango kiduchu mpaka karibia na 2025 huko..
 
Duuuh mkuu sikuijua hii
 
Mbaya zaidi unakuta naye aliingia mkataba wa awali bila kuwaconsult "wahusika".
 
Duuuh mkuu sikuijua hii
Mkuu hili lilileta sana mvutano.. Lakini mwisho wa siku hawa walioingia nao wakatafuta chaka lao vile vile.. Unakumbuka hela za Okwi zililipwa kwenye akaunti ya kiongozi binafsi badala ya akaunti ya klabu..? Wakasingizia sababu ni TRA.. Sasa kuna hela zilitoka kwenye hizo za Okwi zikalipwa akaunti ngeni Hong Kong huko..

Umeona sasa wanavyopokezana ulaji hawa.. Mishahara ya wachezaji ilikuwa inalipwa na TBL, Vodacom wanatoa hela, hela za viingilio, hela za mauzo ya jezi na bidhaa nyingine za vilabu.. Bado unasikia wafadhali wanatoa hela za usajili mambo mengine..

Tunahitaji miujiza pekee itutoe hapa tulipo..
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe ameachia ngazi.

Habari za uhakika zimeeleza kuwa Hans Poppe ameandika barua ya kuachia ngazi kwa madai kuwa anaona mambo yanaendeshwa ndivyo sivyo.

Chanzo chetu cha kuaminika kinaeleza kuwa "Hans Poppe ameachia ngazi kwa kuwa hakufurahishwa na mlolongo ulivyokuwa hadi Simba kuingia mkataba wa SportPesa,” kilieleza chanzo.

"Hans Poppe ameandika barua kujiuzulu kwenye kamati ya utendaji, maana yake anaondoka moja kwa moja katika nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya usajili.

"Kilichomchukiza, anasema kuna kundi lililoongozwa na Rais Evans Aveva na makamu Geofrey Nyange Kaburu, lilifanya mambo kimya kimya na Hans Poppe amesema hata Mo Dewji aliyeisaidia Simba mishahara naye hakushirikishwa hata kiungwana tu, hivyo amepinga hilo."

Chanzo: Muungwana
 
Back
Top Bottom