Mkataba wa Lemere

MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
623
595
Mkataba wa Lemera

Gazeti la Mwanahalisi la tar. 11 Feb. mwaka 2009, katika Makuu yake yenye kichwa cha habari, Mkataba wa Kuuza Kongo lilijikiu katika anga za Virunga. likiclcza kile kiilichoitwa Vita vya Kongo kwamba ilikuwa ni utekelezaji wa Makubaliano ya Lemera y. mwaka I996, yenye shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa kuliko yoyote ilc Afrika Mashariki na Kati. Makubaliano yalifanywa kati y. Laurent Desire Kabila, akiwa kiongozi wa chama cha Kuikombo. Kongo, kutoka utawala wa dikteta wa Mobutu Sese Seko, kwa upande mmoja na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda na Mashariki mwa Kongo. Makubaliano hayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini na hujulikana kwa jina hilo, ukitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyamanda wa kabila la Kitutsi. Taarifa zinaonesha makubaliano yaliandaliwa mapema mjini Kigali, na pale Lemera yalikuwa yanazinduliwa 111 Ilikubaliwa wakati huo kwamba hiyo ndiyo ingekuwa asante au zawadi kwa Rwanda, kwa kuikomboa Kongo.

Laurent Desire Kabila alikuwa tayari amechoka. KW! takriban miaka 20 alikuwa akipambana na utawala wa Mobutu Sese Seko. Alikuwa amchkia hatua ya kutamauka na kutulia mikononi mwa mamlaka za ujasusi jijini Dar es Salaam. Mwaka 1996,ij Kigali, Rwanda, kulikuwa kimeundwa kikundi cha wapiganaji waliojiita Wapinzani wa Dikiteta Mobutu. Hawa waliku“ Wakongomani na Wanyarwanda kutoka Rwanda na wengini waliokuwa wakiishi Mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Kongo Katika kundi hilo alikuwemo Mkongomani, Jenerali Andre Kind Ngando, askari mtaalamu “ kusomea.

Anadaiwa kupata mafunzo nchini Cuba, Ujerumani na Bulgaria. Alikuwa akiongoza Wakongomani wapatao 600 katika kikundi hicho. Wakati kikundi hicho kinataka kuanza vita, kilitaka kuwa na msemaji. Mungu akupe nini! Kikundi hicho kilikwenda Tanzania kuomba ushauri wa Mwl. Julius Nyerere, ambapo kwa ushauri wa TISS, Mwalimu aliwapa Laurent Desire Kabila kuwa msemaji wa wapiganaji.

Mwanzoni mwa vita vya kumg’oa mzandiki, dikteta bedui, Mobutu, kikundi hiki kilijulikana kama cha Wanyamulenge. Dunia nzima ikaambiwa na kuaminishwa kuwa hayo yalikuwa maasi ya Wanyamulenge. Wanyamulenge ni watu wanaodaiwa kutoka kwenye vilima vya Mulenge vilivyoko wilaya ya Uvira katika mkoa wa Kivu Kusini.

Makabila ya asili ya hapo ni Wavira na Wafuliro. Wanaojiita Wanyamulenge ni Wanyarwanda. Vita vilianza kwa propaganda kuu kwamba serikali ya Mobutu haitambui Wanyamulenge ambao walidai ni raia wa Kongo ambapo serikali ya Kongo iliwanyanyasa na inawanyima uraia. Haya yalikuwa madai makubwa sana yaliyovuta hisia kali na huruma kwa wapiganaji. Wapinzani, chini ya Jenerali Andre Kisasi Ngando, na msemaji mkuu wao Laurent Kabila waliteka, kama mchezo, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma. Wakavuka Ziwa Kivu na kuingia Kivu Kusini.

Ilikuwa baada ya kukamata mji wa Bukavu, makao makuu ya Kivu Kusini na sehemu nyingi za mkoa huo, wapiganaji wa Kinyarwanda waliingiza pendekezo la rais ajaye wa Kongo, kutoka Kivu Kaskazini na Kusini kwa Rwanda. Lakini kabla suala hilo nyeti kupewa uzito unaostahili, wapiganaji wa Kinyarwanda, baada ya kuteka Bukavu, wanadaiwa kuanza kupora mali, magari, vifaa vya rlyumbani, dawa katika maduka, hatua ambayo ilielezwa kuwa Uhamishaji wa mali za wakazi wa Bukavu na maeneo mengine.

Alikuwa Jenerali Ngando anayeripotiwa kupinga uporaji “Siomithilika, jambo ambalo lilimletea uhasama kwa baadhi ya Wapiganaji. Kuona hivyo, Laurent Kabila akamsaliti Jenerali gando. Ngando anasemekana kuuawa siku chache baada ya kutofautiana na wapiganaji juu ya uporaji. Inaelezwa kuwa alimiminiwa risasi na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto katika mbuga ya wanyama ya Virunga.

Kabila aliulizwa mara nyingi juu ya Ngando. Alikuwa majibu tofauti. Akiwa bado msituni alisema Jenerali Ngando amekamatwa na majeshi ya serikali na mara ametekwa wanamgambo wa Mai Mai. Baadaye Kabila ' alisema Ngando alijeruhiwa na kupelekwa Ujerumani kwa matibabu. Na wakati akiwa rais, aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kuwa Ngand0 alikuwa askari kama askari“ wengine na kwamba alikufa kwenye mapambano. Ilikuwa baada ya kifo cha Jenerali Ngando ndipo Kabila aliingizwa kwenye makubaliano ya kumega Kongo. Kwanza, kikundi cha wapiganaji kiligeuzwa kuwa chama cha AFDL (Alliance de front Democratique pour la Liberation du Congo). Kabila akapanda cheo na kuwa kiongozi wa chama cha ukombozi wa Kongo kutoka kuwa msemaji tu wa wapiganaji.

Baada ya kuundwa kwa AFDL, jina la Wanyamulengc likatoweka kabisa. Wapiganaji wakaitwa waasi wa Kongo. Taarifa zinasema kabla wapiganaji kutoka Bukavu na kuanza safari iliyomfikisha Kabila madarakani, waliingia katika mkataba ambao ndio umekuja kuitwa Makubaliano ya Lemera. Viongozi wakuu wa wakati huo wa baadhi ya nchi walipata nakala ya makubaliano hayo ya kumega Kongo.

Miongoni mwa nchi hizo ni Tanzania, Namibia, Uganda, Burundi, Zambia, Ethiopia, Eritrea, Zimbabwe,“ Angola. Namibia, Sudan na baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani: Makubaliano ni pamoja na kufanya fnikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini kutawaliwa na Wanyarwanda wa Kitutsi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Uganda, Na kwamba utawala huo ambao ungefanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Kabila, ungetekelezwa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 1998.

Chini ya mpango huo, raia wa Kongo, wakazi wa Kivu Kaskazini wangehamishiwa Kivu Kusini kwa aratibu na kwa utulivu huku makazi yao yakichukuliwa na wavamizi. Hatua ya kwanza isingekuwa ngumu kwani Rwanda ingedai kuwa inapambana na wanamgambo wa Kihutu walioitwa Interhamwe ambao itaelezwa kuwa wanatishia amani nchini Rwanda.

Hivyo ndivyo imekuwa ikifanywa hadi hivi sasa. Makubaliano yalieleza kuwa kuchukuliwa kwa miji ya Goma na Butembo mkoani Kivu Kaskazini, sharti iwe hatua ya kwanza kwa kuwa hayo ndiyo maeneo yenye upinzani mkubwa. Kufanikiwa kwa awamu ya pili, kungetegemea mafanikio ya awamu ya kwanza, kama makubaliano yanavyodaiwa kueleza.

Wafuatiliaji wa mahusiano ya Rwanda na Kongo wanasema ingawa mpango huo ulishindikana kutekelezwa kuanzia mwaka 1998, kuingia kwa majeshi ya Rwanda nchini humo hivi sasa, ni utekelezaji wa hatua ya kwanza ya Makubaliano ya Lemera, na isitoshe tayari miji ya Goma na Butembo iko chini ya kile kinachoitwa Majeshi ya Ushirikiano ya Rwanda na Kongo.

Kwa mujibu wa masimulizi juu ya makubaliano hayo, awamu ya pili ingekuwa kujaza wakazi wa Kaskazini katika Kivu Kusini na kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wazawa wangeenguliwa, kukosa uongozi na hivyo kunyimwa sauti. Hatua nyingine ilikuwa kuanzisha benki ya kusaidia wavamizi katika Kivu mbili, kujenga makazi yapatayo laki 600,000 elfu na kujiimarisha katika nchi ya kigeniKongo. Inaaminika kuwa Kabila alikubaliana na masharti ya makubaliano kwa kuwa lengo lake lilikuwa moja tu, Kuingia ikulu ya Kinshasa kwa msaada wowote kutoka kwa yeyote awe Mungu au shetani. Ilikuwa baada ya makubaliano hayo, Kabila alisonga mbele na hatimaye kushinda na kuingia Ikulu ya Kinshasa akiwa na wapiganaji wa Rwanda, akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Rwanda, J ames Kabarebe.

Baada ya kuingia ikulu, Kabila aliwasiliana na Mwl. Nyerere mjini Dar es Salaam chini ya uratibu wa TISS, ambako chaguo la Tanzania lilikuwa nikuzuia uuzwaji huo wa ardhi ya Kongo. Mashauriano yaliyochukua sura dhahiri ya nguvu ya Tanzania katika ujasusi, yalimpa nguvu Kabila na alipowarejclca wabia "K aliwagcuka dhahiri shahiri.

Ilikuwa baada ya miaka miwili ya urais, alitangaza, tena kwa j . kuwa wageni wote waondoke nchini. Aliongeza kwa kufaa,,“ kwamba Wanyarwanda warudi kwao na kusema anawashukum k“ kazi waliyofanya.

TISS ilikuwa tayari imesoma mwelekeo wa makubaliano yale na kuona kuwa yanatoa mwanya kwa kile kilichoitwa Nchi ya Ahadi ya Watutsi kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Somalia, Ethiopia, Eritrea na Tanzania. Ilikuwa iwavyo, Kabila atangaze, akiwa rais, kuwa Kivu mbili zote ni makazi ya Watutsi ili hau wananchi wa Kongo watakaobaki humo, wawe wanafahamu kwamba siyo kwao.

Kabila alinukuliwa akisema kuwa hayo (Makubaliano ya Lemera) ni makubaliano ya porini na kwamba yeye hakuwa na madaraka ya kuuza nchi. Alisema hakatai kuwepo mkataba, lakini akataka hilo [ipelekwe kwa wananchi kupitia bunge ili wananchi wenyewe waamue. Kilichomshangaza zaidi Kabila, baada ya kutangaza kuwa Wanyarwanda warudi kwao, ni kwamba aliyekuwa wa kwanza kuondoka na kukimbilia Afrika Kusini, alikuwa waziri' wake wa mambo ya nje aliyeitwa Bizima Karaba (Bizimana Karahamuheto).

Katika mshangao na labda kejeli, Kabila alisema, “Kumbe nchi ilikuwa imevamiwa! Hata waziri wangu wa mambo ya nje“ alikuwa Mnyarwanda?" Hiyo ilifuatiwa na kufukuzwa kwa James Kabarebe aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Kongo na kurudi Rwanda na kuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda. Hatua hizi na nyingine, ndio’ zilisababisha kutotekelezwa kwa Makubaliano ya Lemera. Pengine wachunguzi na wafuatiliaji wa mahusiano ya nchi hizi mbli wanasema, makubaliano yameandikwa na yapo; hayajafutika Kilichofanyika ni ukaidi wa kimadaraka wa Kabila kama ilivyo kwaMarais wengine wa Afrika wa kutotaka kutimiza ahadi yake akuingia ikulu. Kabila alikuwa amesoma kitabu cha Raphael

Ntibazokiza kilichoeleza mahusiano ya Watutsi na wabantu, kiitwacho Plan de la Colonisation Tutsi au Kivu et Region Centrale d9 I ’Afrique. Yaani, Mpango_ wa ukoloni wa Kitusi katika Kivu na eneo la Afrika ya Kati.

Raphael anaandika, “(. . .) Mhutu ameumbwa kufanyia kazi watu wengine. Hawezi hata kujaribu kupata uongozi. Chukua nafasi zote za mikoa na wilaya na atakayekuwa mtawala ahakikishe kuwa anaalinda maslahi yetu (...). Baadaye watakapokuja kustuka; watakuwa wamechelewa (...) " Licha ya Raphael, mmoja wa waliokuwa watu wa karibu wa Kabila alinukuliwa akisema kuwa hakuna kitu kilichomsononesha Kabila kama kauli ifuatayo ndani ya kitabu Cha Raphael iliyosema: “Tutumie ukarimu wao. Tujinyenyekeze kwao kama sisi ni watumishi wao. Tukiishachukua nafasi zao tuwatelekeze na “kuwalipa ujira wa nyani’ ili kudhihirisha kuwa hawana uwezo."

Kabila aliuawa kabla hajamaliza kunyukana na Rwanda. Aliuawa na mmoja wa watoto wake, yaani vijana wadogo waliokuwa watu wa karibu sana na waliomlinda tangu akiwa msituni. Kuna maelezo tatanishi juu ya kifo cha Kabila. Wapo wanaodai aliyemuua alitumwa na waliokuwa wakitaka atekeleze makubaliano ya Lemera, lakini, wakati huo huo, wapo wengine wanadai ni karata za nchi za Magharibi. Kwa kuwa Jonas Savimbi aliuawa katika mwaka moja tu baada ya kifo cha Kabila, inadaiwa kulikuwa na mkono usioonekana wa mataifa makubwa, ukitaka kuingia Kongo na hivyo kuomba msaada wa kuondoshwa kwa Kabila huku mkkono huo usionekana kuwezesha kukamatwa na kuuawa kwa Savimbi. Siasa hizi halijafafanuliwa.

Kuingia kwa Joseph Kabila, anayedaiwa kuwa mtoto wa kufikia wa Laurent Kabila, kulionekana kuleta mgeuko mwingine kuelekea kule ambako baba yake alikataa. Kwani kile kinachoitwa Makubaliano kati ya Serikali ya Rwanda na ya Kongo kinaonekana Wazi kuwa utekelezaji wa mpango wa awali ambao Laurent Kabila alikataa. Aidha, kukamatwa kwa Jenerali Laurent Nkundabatware Ila kuhifadhiwa nchini Rwanda kulielezwa kuwa ni sura kamili ya kilichokuwa kikihisiwa cha kuheshimu kazi ya maandalizi aliyokuwa akifanya nchini Kongo.

Yapo madai ya muhimu yanayoelekea kidole kwa Nkundabatware kuwa ni Mnyarwanda kutoka Rwanda_ Lakini, Rwanda walisema ni Mkongomani. Jambo la msingi ni kwamba Nkundabatwe hakuwa na jeshi lolote nchini Kongo_ Aliongoza majeshi ya Rwanda hadi hapo ilipoonekana kuwa mazingira yamekuwa mazuri kwa Rwanda kuingia Kongo kwa kisingizio cha kufukuza Interhamwe na kuweka usalama mpakani. Kwa kuthibitisha hili, mpiganaji wa kundi la M23 mjini Goma, Mutereba Rwakibela alinukuliwa akisema, “Hata akipelekwa Kongo leo hii, Kabila atamlinda J enerali Nkundabatware, labda kama wakuu wa Kongo na Rwanda watakuwa wamegundua kuwa amewasaliti.” Aliyekuwa Waziri Oflsi ya Rais (Siasa) nchini Uganda, Moses Byaruhanga, alisema nchi yake inaunga mkono Shirikisho la Kivu na Kisangani na kwamba wanasubiri kuona serikali ya Kinshasa inalionaje suala hilo.

Katika medani za kijasusi, kumekuwa na taarifa za kukamilisha kumegwa kwa mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kutoka Jamhuri ya Kongo na kuzifanya Muungano wa Jamhuri ya Kivu. Kauli ya msemaji wa ikulu Uganda iliongeza uwezekano wa kuimega Kongo pale inapohusisha jimbo jingine la Kisangani ambako kwa nyakati. tofauti majeshi ya Uganda yanadai kuwinda waasi wa Lord's Resistance Army (LRA). Kiongozi wa LRA, Joseph Kony alikuwa akipambana na majeshi ya serikali ya Yoweri Museveni kwa zaidi ya miaka 30.

Uganda sasa ilidai kuwa Kongo inatumika kama kichaka cha waasi hao. Kauli ya Uganda haipishani na mipango inayodaiwa kufanywa na Rwanda ingawa Rwanda, kupitia balozi wake mjini Dar es Salaam, iliwahi kukaririwa ikisema haina mpango wowote wa kuigawa Kongo. Jumuiya ya Kimataifa ilitekwa kwa propaganda za Interhamwe, Wanyamulenge, waasi wa LRA na kumbukumbu za mauaji ya kimbari.

Katikati ya majilio hayo mapya ya Joseph Kabila, Paul Kagame na Yoweri Mseveni kujaribu kutekeleza Mkataba wa Lemera, mwaka 2015, nguvu ya Ujasusi ya Tanzania imeingilia kati, kwa mwavuli wa Umoja wa Mataifa, imepeleka kikosi hatari kiitwacho koboko au Blackm mba cha makomandoo nchini Kongo kuzima jaribio hilo linaloratibiwa na washirika hao kwa mgongo wa kundi la uasi la M23. Ni vita kamili inayoungwa mkono na Afrika Kusini na ushindi unapatika kwa Kongo kubaki salama chini ya mkono wa TISS na MI. Maslahi ya Tanzania katika hili yanabaki kuwa ni Usalama katika eneo la maziwa makuu. Lakini nyuma ya pazia la ujasusi eneo la maziwa makuu linapita kwenye kipindi kigumu.

Idara ya ujasusi nchini Rwanda (NISS) inatumia kila njia kudhibiti wanaoitwa wahaim' mathalani mauaji ya aliyekuwa mkuu wa ujasusi, Patrick Karegeya. Vyombo vya Utangazaji (Habari) vya mataifa viliandika habari nyingi sana kuelezea mauaji hayo lakini ukweli unabaki kuwa, Apollo Gafaranga ndiye aliyetekeleza mauaji ya Patrick Karegeya huko Johanesburg. Huyu Apollo Gafaranga ni mmoja wa wafanyibiashara wakubwa hapo Rwanda akiwa na Jumba la Sinema la Kifahari maeneo ya Nyamirambo ambapo sasa ni maarufu kwa jina la Cine star cinema. Ujenzi wa kituo hicho (au jumba hilo) uligharimu dola milion moja, na siku ya ufunguzi mwaka 2009, aliyefungua ni Rais Paul Kagame mwenyewe.

Nyuma ya pazia, Apollo Gafaranga alikuwa amefunzwa ujasusi na pia akiwa na ya hali ya juu ya uuaji. Wakati Patrick Karegeya akiwa Mkuu wa Ujasusi miaka hiyo, Appolo Gafaranga alikuwa ni mmoja wa mawakala (infomer) wake. Baadaya Patrick Karegeya kumuasi Kagame na kukimbia kwenda uhamishoni nchini Afrika Kusini, huko Rwanda kuna kikundi kiliundwa haraka na rais Kagame kilichojulika kama Escadran dela Mort, ambapo Apollo Gafaranga alikuwa mmoja wa kikundi hiko. Lengo kuu la

kikundi hiki, limekitwa juu ya kuwatafuta wale wote walio kinyume na utawala wa Rwanda na kuwamaliza (yaani kuwafuta kwenye nyuso za ulimwengu).

Baada ya kuingizwa katika kikundi hiki, Appolo Gafaranga alipewa mafunzo ya hali ya juu ya namna ya kutekeleza mauaji bih kujulikana ambapo lengo kuu ni kumuua. Karegeya. Mafunzo yalipokamilika na biashara hiyo kuwa imefunguliwa kama geresha machoni pa watu wa kawaida, mwaka 2010, Appolo Gafaranga alianza urafiki na Patrick Karegeya huku akijifanya kuwa ni mmon wa watu waliokuwa wakiupinga utawalawa wa Kagame nchini Rwanda. Appolo Gafaranga alianza kumtembelea Bw. Patrick Karegeya huko Afrika Kusini na pia alishiriki kwa ukamilifu katika mikutano ya chama cha RNC, chama ambacho mpaka leo kinapanga kuuangusha utawala wa Kagame huko Rwanda.

Mara zote aliposafiri kwenda Afrika Kusini kwa Patrick Karegeya, Appolo Gafaranga alikuwa hatokei moja kwa moja nchini Rwanda na isitoshe mara zote, alikuwa akitumia pasipoti na nyaraka zingine za bandia kwenda Afrika Kusini. Desemba, mwaka 2012, ni (huyuhuyu) Appolo Gafaranga alimri Bw. Patrick Karegeya kuacha kutumia walinzi aliokuwa amepewa na serikali ya Afrika Kusini chini ya mwavuli kuwa wanaweza kununulika na akauawa, na ndipo. Patrick Karegeya alikubaliana na ushauri huo (ulio na uasi uliojificha) na kwenda katika mamlaka za Afrika Kusini na kutoa ombi lake hilo akisema sasa yuko makini na kila safari anayofanya ndani ya nchi hiyo kwavyo hahitaji walinzi. Na bila kusita, mamlakl ya Afrika Kusini iliwaondoa walinzi wake.

Miezi sita baadae, Apollo Gafaranga alimpigia simu Patrick Karegeya na kumwambia kuwa serikali ya Rwanda inamtishia uhai wake na tayari imefunga biashara zake. Hivyo akamuomba Patric“ Karegeya amtengenezee mazingira ili nae akimbilie huko Afrika ya Kusini na kuanza biashara huko. Muda wote huo, Patrick Karegeya hakujua kuwa huyo aliyekuwa naye (Appolo Gafaranga) ana mpango mwingine kabisa tangu mwanzo wa urafiki wao. Patrick Karegeya alianza maandalizi ya kumuandalia makazi mkimbizi mwenziye, Appolo Gafaranga.

Tarehe 28 Disemba, Appolo Garafaranga aliwasiliana tena na rafikiye (mlengwa wa kifO) Patrick Karegeya na kumwambia kuwa amtafutie chumba katika Hoteli, na kwamba safari hii asingependa kufikia nyumbani kwake, kwa. Patrick Karegeya, ili asije akahamisha usalama wake maana naye anafuatiliwa kwa karibu na serikali ya Rwanda. Kwa hiyo, angependa kufikia hotelini ambako atakuwa salama zaidi.

Patrick Karegeya alikodi chumba namba 905 katika Hoteli ya Sandton, Johanesburg na tarehe 29 mwezi huohuo,. Appolo Gafaranga akafika Afrika Kusini na kupokelewa na Bw. Patrick Karegeya kwenye uwanja wa Oliver Tambo na kuelekea moja kwa moja hotelini, ambako waliachania hapo kwa makubaliano kwamba wakutane tarehe 31 ili kuendelea na mipango yao ya namna ya kuiangusha serikali ya Kagame lakini pia namna anavyoweza kuanzisha makazi yake na biashara zake hapo Afrika Kusini.

Kama walivyoahidiana, ilipofika tarehe 31 mwezi huohuo, wa Disemba, Patrick Karegeya akaenda moja kwa moja Hotelini aliko mshirika na rafiki wake, Appolo Gafaranga. Alipofika na kuingia ndani, Patrick Karegeya alifunga mlango na kuweka alama pale mlangoni iliyoonesha, Do not disturb.

Wakati Patrick Karégeya anaiangia ndani ya chumba cha Hoteli ile, mle ndani ya chumba palikuwa na jumla ya watu watatu, maana yake kuna wawili waliongezeka ambapo wote hawa, wanatoka kwenye kikosi kazi cha Escadron dela Mort. Hawa wawili walikuwa wamejificha bafuni wakati Patrick Karegeya akiingia. Walimuua kwa kumpiga risasi Bw. Patrick Regeya na walipohakikisha amekufa (yaani roho na kiwiliwili Vimeachana) wakaubeba mwili na kuuweka kitandani kisha Wakaufunika shuka kuanzia, shingoni hadi kisiginoni. Na hapo Patrick Karegeya historia ya uhai wake ikawa imefutikia hapo duniani. Baada ya mauaji hayo ya kijasusi, Escadron dela mort waliondoka pasipo kujulikana na kutokomea nje ya Afrika Kusini wakipitia Musumbiji na Tanzania.
 
Kumbe vijana wetu wa TISS wako vizuri kiasi hicho?

Tuwape hongera kwa maono,mpango,na kazi nzuri wanazofanya kwa ukombozi wa ara letu la Afrika.
 
Nakumbuka pia kuna mwanajeshi nazani wa Rwanda au Burundi kama sio Kongo alikamatiwa Airport DSM akijaribu kukimbia.
 
Kumbe vijana wetu wa TISS wako vizuri kiasi hicho?

Tuwape hongera kwa maono,mpango, na kazi nzuri wanazofanya kwa ukombozi wa ara letu la Afrika.
Kipindi hicho bashite alikuwa hana nguvu yoyote ndani ya dstv
 
Back
Top Bottom