#COVID19 Mkataba wa EU na AstraZeneca kumalizika Juni, EU imeanza maongezi na Pfzer

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na Soko la Ndani, Thierry Breton amesema umoja huo haujarefusha mkataba wa kuendelea na chanjo ya Covid-19 ya ubia wa makampuni ya Kiingereza na Kisweden ya AstraZeneca.

Breton ameiambia televisheni ya Ufaransa "France International" kwamba hawajarefusha mkataba baada ya mwezi ujao wa sita na kwamba bado wapo katika hali ya kutafakari kuhusu hatua hiyo.

Chanjo hiyo imehusishwa na athari ndogo za kuganda kwa damu, na hasa kwa wanawake wenye umri mdogo, na kusababisha baadhi ya mataifa kuweka masharti ya kutumiwa kwa watu wenye umri mkubwa.

Awali Jumamosi, Kamisheni ya Umoja wa Uklaya iliingia makubaliano na mzalishaji wa chanjo nyingine ya Covid-19 kampuni ya BioNTech/Pfizer ya ununuzi wa dozi ya nyongeza ya zaidi ya dola bilioni 1.8 hadi 2023.

DW Swahili
 
Aisee, kumbendio mana walikuwa wanamchukia Magu, dozi ya nyongeza tu dola Bll 1.8 !!. In Tsh..you talking about trions of miney.
Kweli vita ya kibiashara nimbaya sana kama alivyokuwa akisema mwenyewe.

Hapa bongo naskia kipimotu ni karibia dola 100.
 
Back
Top Bottom