Mkataba mwingine feki-wanafunzi wa tz msumbiji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkataba mwingine feki-wanafunzi wa tz msumbiji

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Nahami, Sep 8, 2011.

1. N

Nahami New Member

#1
Sep 8, 2011
Joined: Sep 8, 2011
Messages: 3
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Inasikitisha kuona hapa tz mwanafunzi ananyimwa mkopo wakati serikali hiyohiyo inamgharamia mwanafunzi mmoja TSh 20,525,000/= kwa mwaka hapo nchini msumbiji. Kwa habari za kuaminika nilizozipata zinasema kuwa wanafunzi hao wa kitanzania ni 29 waliopelekwa chini ya mpango wakubadilishana wanafunzi yaani Tanzania-Mozambique students Exchange Program (TAMOSE). Inasemekana makubaliano kt ya tz na msumbiji yalikuwa wanafunzi 50 kwa 50 ila tz ikapeleka 29 wakati wao waliletwa 50. Kitu ambacho kinatia wasiwasi ni kwamba fedha hizo ambazo wanalipiwa ni mkopo! Tena kwa mwaka wa lugha tuu, Je? Wakianza masomo rasmi baada ya lugha itagharimu kiasi gani? Inavyoonekana hapo kuna ufisadi au mkataba wa kizembe na wakitapeli kwani haiwezekani serikali ikubali kuendelea kumlipia mwanafunzi mmoja zaidi ya milioni 20 kwa mwaka wakati ingetosha kuwalipia wanafunzi kadhaa hapa tz. WADAU wanaofahamu mikataba naomba wafuatilie ijulikane kama kuna nini hapo sababu kwa mtaji huu tz tunanyonywa.

2. Gajungi

Gajungi Senior Member

#2
Sep 9, 2011
Joined: Sep 4, 2011
Messages: 195
Likes Received: 5
Trophy Points: 35
Kuna mawili:Hizo info si za uhakika au kuna ufisadi mkubwa sana. Nina taarifa za wanafunzi watz cuba na Algeria hawajafikia hapo, kwa hiyo hilo ni swala sensitive liangaliwe kwa ukaribu sana.

3. S

Shimba New Member

#3
Sep 9, 2011
Joined: Sep 7, 2011
Messages: 4
Likes Received: 0
Trophy Points: 0

Nilipoona kichwa cha habari hii kwanza wala sikushtuka kwani mikataba yetu mingi haina tija. Pia nilimtumia email mdau mmoja ambaye alienda huko maputo juzi kwenye michezo hii ya All African Games inayoendelea pengine anaweza kupata info zozote toka huko kama wanafunzi hao wanasoma jijini maputo ilabado analifanyia kazi na aliahidi leo atanipa jibu. Ninachofahamu kawaida nikwamba kama ni exchange program basi wanahudumiwa na nchi waliyopo nasiyo tanzania. Ilakama ni nchi yetu basi hainahaja kuendelea na mkataba wa kuumizana namnahiyo. Labda kama ingekuwa wanasoma USA hapo ingeniingia akilini. Wanafunzi wanaosoma nje hukopeshwa na bodi USD 450 hadi 800 kwa mwezi mfano algeria na urusi ambazo hataukizidisha kwa 1575 haifiki hiyo mil 20. Sijui hapo inakuwaje ila ninachohisi kuna watendaji aidha huko wanakosoma au hapa bongo wanahusika kujinufaisha na hiyo program laasihivyo basi tayari wangeshavunja mkataba.

4. S

Shimba New Member

#4
Sep 9, 2011
Joined: Sep 7, 2011
Messages: 4
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Nimeambiwa wanafunzi hao walishukia hotelini ambapo ndiko wanakoishi hadi hivi sasa ingawaje wameshaanza masomo. Hawaishi katika hostel za vyuo ndiyomaana wanalipiwa gharama kubwa hivyo na serikali yetu kupitia bodi tena bila ridha yao. Kuna mwanafunzi mmoja wa msumbiji anaesoma hapo UD chini ya huo mpango amenitonya kwani anafahamiana na baadhi ya hao wanafunzi. Hapa napatwa na shaka na mmiliki wa hiyo hotel ni m bongo au wa huko.

5. n

ngulube New Member

#5
Sep 11, 2011
Joined: Sep 9, 2011
Messages: 4
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
wawarudishe kama wale wa ukraine kama wamekosa vyuo vya kuwapeleka kuliko kuwapangishia hoteli. Sidhani kama mtanzania tena mwanafunzi wa kawaida anaweza kumudu gharama za kuishi hotelini hata mwezi mmoja. Labda kama hawapewi hizo pesa mikononi kwani wangesha acha chuo kitambo ikizingatiwa south africa vyuo ni nafuu na walipo hata kwa miguu panazamika. @ Milioni 20!! Labda mdau kazidisha sifuri. Kama kweli wanalipiwa pesa hizo basi siyo mkopo kwani hazilipiki.

6. Abdulhalim

Abdulhalim JF-Expert Member

#6
Sep 11, 2011
Joined: Jul 20, 2007
Messages: 16,472
Likes Received: 126
Trophy Points: 160
Exchange students ni special case na kama fani wanazosomea ni nyeti hamna hatari yeyote. Tatizo linaeza kuwa upatikanaji na mchujo wa wanafunzi wenye kuna uwazi kiasi gani, otherwise hamna hatari.

7. Bujibuji

Bujibuji JF-Expert Member

#7
Sep 11, 2011
Joined: Feb 4, 2009
Messages: 35,336
Likes Received: 22,188
Trophy Points: 280

saa hizi mahitaji yetu makubwa ni umeme. Naamini huko Nchumbiji wanasomea namna ya kujaza mabwawa kwa nguvu zisizo onekana.

8. Abdulhalim

Abdulhalim JF-Expert Member

#8
Sep 11, 2011
Joined: Jul 20, 2007
Messages: 16,472
Likes Received: 126
Trophy Points: 160
Kwa kifupi exchange students ni kama ambassadors kwa taifa huko waendapo, na priveleges zao ni tafauti. Cha msingi ni kuondoa subjectivities kwene utoaji wa hizo nafasi, maana najua mara nyingi ni mambo ya chini ya kapeti na vijimemo.

9. Perry

Perry JF-Expert Member

#9
Sep 11, 2011
Joined: Feb 24, 2011
Messages: 10,029
Likes Received: 861
Trophy Points: 280
Acha vijana wafaidi bana..

10. S

Shimba New Member

#10
Sep 11, 2011
Joined: Sep 7, 2011
Messages: 4
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Nilizozipata za uhakika kutoka huko nikwamba walienda huko badala yakushukia vyuoni wakawekwa hotelini kwa madai kuwa nafasi za vyuoni zimejaa. Walikopeshwa na bodi dola 250 kwa mwezi kwaajili ya chakula na malazi ila gharama zikaongezeka kwa dola 650 baada ya kuwekwa hotelini nakuwa dola 900 kwa mwezi kila mmoja. Wakatimba ubalozini kushinikiza serikali iwaongezee pesa bila mafanikio. Bill kutumwa tz serikali ikadai italishughulikia ila nimkopo wao. Wakakubali ila sasa yapata miezi mi 3 hawajalipiwa pesa hizo wakaandamana tena ubalozi kudai waondolewe wanapoishi wapelekwe chuoni kwani gharama nikubwa na pesa ya kujikimu mahitaji ya chuo wamenyimwa kwani serikali imeamua kuendelea kulipia wanapoishi wakati vyuoni ni kama dola 10 tuu kwa siku.

11. Perry

Perry JF-Expert Member

#11
Sep 11, 2011
Joined: Feb 24, 2011
Messages: 10,029
Likes Received: 861
Trophy Points: 280

ni bora m2 upigikie kwenu kuliko kwenye nchi ya ugenini.

12. n

ngulube New Member

#12
Sep 11, 2011
Joined: Sep 9, 2011
Messages: 4
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Kama mkataba unasema wanafunzi waishi hotelini wakati wakisoma basi na wakwao wawekwe hapo Kempiski hotel wajilipie kama watamudu. Waache kuwatesa vijana wa watu kwani wataishia kukatwa mikopo hiyo hadi wastaafu na watoto waendelee kulipa. Kama msumbiji ilikuwa haina sehemu ya kuwaweka kwanini waliingia mkataba? Au serikali haioni kama mkataba unanyonya upande wetu? Bongo wanafunzi wanapewa sh 7,500 kwa siku na bodi tena kwa mbinde na wakati huohuo inawalipia wanaosoma nje dola 30 kwa siku sawa na sh 45,000 tena kwa kuwalazimisha waishi hotelini!

Loading...