Mama: Mwanangu hebu mpigie simu babako mwambie chakula tayari.
Mtoto: Sawa mama.
Mtoto: Mama simpati.
Mama: Basi subiri kama baada ya dakika 5 halafu mpigie tena inawezekana ni mambo ya network hayo.
(Baada ya dakika 5)
Mtoto: Mama mimi baba simpati, simu yenyewe anayepokea ni Mwanamke.
Mama: haaa!! sawa mwanangu niachie mimi suala Hilo, wewe nenda kale.
(Baada ya dakika 30 Baba akabisha Hodi..
Akakaribishwa na bonge la kibao hajakaa vizuri sufuria mara mwiko ikawa balaa, Mume yuko katika hali ya mshangao.. akazidiwa)
Majirani wakaja kuamulia ugomvi, Kufika Mume yuko chini ya sofa Hoi bin Taabani.
Mama: Pu-mba-vu zako wewe kunifanyia Mimi??? hivi ukaenda kwa malaya zako kuniachia mimi nyumba?
Mwanangu hebu waambie majirani yule Mwanamke Alipopokea alisemaje?
Mtoto: Alisema, SAMAHANI MTEJA WA NAMBARI ULIOPIGA, HAPATIKANI KWA SASA!!!
Hahahahah....
Ingekua wewe ni huyo Baba ungemfanyaje Mkeo???