Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,853
- 30,197
PICHA YA ABDALLAH KASSIM HANGA AKIBARIZI MSASANI BEACH KWENYE NYUMBA YA OSCAR KAMBONA
Hakuna kitabu kilichoeleza historia ya Hanga na Oscar Kambona kwa siku chache Hanga lipokuwa anakaa nyumbani kwa Kambona London kama kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.’’
Hanga alikuwa anatokea Conakry Guinea anarudi Tanzania akafikia nyumbani kwa Kambona.
Kambona akamsihi Hanga asirudi Tanzania abakie hapo hapo Uingereza kwani taarifa zake alizokuwanazo Kambona hazikuwa nzuri.
Hanga hakukubali ushauri wa Kambona akashikilia lazima arudi.
Kambona kwa kutaka Hanga abadilishe mawazo yake akawaita vijana wawili kutoka Zanzibar waliokuwa pale London waje wamsaidie katika kumshawishi ‘’mzee’’ wao abakie London.
Katika vijana hawa alikuwa Ahmed Rajab.
Kambona hakufanikiwa juu ya juhudi hizi alizofanya.
Qadar ya Allah ilikuwa imekwishapita Hanga alikuwa ameandikiwa kuuliwa Zanzibar.
Hilo ndilo lililokuja kuwa.
Haikuwa Kambona peke yake aliyemuonya.
Endelea kusoma.
Kuna mtu alinisikia Radio Kheri nafanya kipindi kuhusu historia ya Zanzibar na nikamweleza Hanga.
Huyu bwana akanitafuta ili anieleze mengi kuhusu Hanga kwani wakijuana vizuri Zanzibar toka udogo wao.
Tulikutana na akanieleza kisa cha Hanga kinachofanana na yale yaliyotokea London nyumbani kwa Kambona.
Huyu bwana anasema kuwa kulikuwa na vijana kiasi waliokimbilia Dar es Salaam baada ya mapinduzi kutafuta kazi na kuanza maisha mapya.
Yeye alikuwa mmoja wa hawa vijana wa Kizanzibari na alipata kazi katika kampuni moja ya ndege.
Ikawa kila ndege yake ikitua Dar es Salaam yeye anakuwa uwanjani kuipokea.
Anasema siku moja alikuwa uwanja wa ndege kupokea ndege yake akamuona mke wa Hanga, Bimkubwa pale uwanjani.
Akamfuata kumsalimia na kumuuliza mbona yuko pale.
Bimkubwa akajibu, ‘’Kassim anakuja leo nimekuja kumpokea.’’
‘’Mimi nilishtuka sana kwa kuwa sisi vijana kutoka Zanzibar tuliokuwa Dar es Salaam tulikuwa kila siku tunakutana na kupashana habari zinazotoka Zanzibar na taarifa kuhusu Hanga zilikuwa zinatisha.
Huu ulikuwa wakati watu wanakamatwa na kupelekwa jela utasikia fulani kakamatwa jana usiku, fulani inahofiwa kauliwa na taarifa nyingi mfano wa hizo zilizokuwa zinatisha sana.''
Mpashaji wangu anasema yeye aliingia hadi ndani ya ndege kumlaki Hanga.
Akamuomba wale chakula pamoja pale uwanjani yeye na mkewe Bimkubwa kisha ndiyo wende zao.
Alimpatia nafasi Hanga na kumtahadharisha kuwa wala asitoke pale uwanja wa ndege kwenda nyumbani bali abakie pale pale na arudi London na ndege ile ile na kimya kimya.
Mpashaji wangu akanieleza kwa masikitiko makubwa kuwa Hanga alimkatalia.
Wakaagana Hanga akaondoka na mkewe.
Yaliyomfika Hanga yanafahamika.
Kalamu ya Allah ilkikuwa imeshaandika kalamu imenyanyuliwa na wino umekauka.
Picha hiyo hapo chini inamuonyesha Hanga akiwa Msasani Beach alipokuwa anakaa kwenye nyumba ya Oscar Kambona.
Ilikuwa bila shaka kutoka nyumba hii ndipo alipochukuliwa kupelekwa Ukonga Prison nakutoka hapo akarejeshwa Zanzibar.