Aisee unauliza jibu?huyo alikuwa jambazi!...motor vehicle inspector ndo mwenya haki ya kukagua leseni yako!..kama kweli alikuwa askari angekuambia umpe kadi ya gari na kitambulisho chako aangalie majina ili kujiridhisha hilo gari hujaliiba hapo coco, alafu cha kushangaza hao askari wanakaa na wateja maeneo ya hapo coco wakati pembeni tu hapo kwa pinda watu wanakabwa saa moja usiku,aisee mungu wako mkubwa!Habari zenu wakuu, Natumai mnaendelea vizuri na shughuli za kila siku kwa maendeleo ya taifa letu la Tanganyika.
Ilikua siku ya jumamosi tarehe 12/07/2014.
Mida kati ya saa mbili na saa tatu usiku, baada ya kupata chakula nikaamua mimi na mwenzangu(rafiki wa kike) twende fukwe za coco kupunga upepo na kubadilisha mazingira, Tulipofika(upande wa sinema) hatukutaka kushuka kwenye gari bali tulibaki ndani ya gari huku tulibadilishana mawazo na pia kupiga picha kwa kutumia simu zetu, kuna wakati ilibidi tutoke nje ili kupata madhali nzuri ya kupigia picha, Tulikaa kwa muda wa kama dakika 40 kisha tukaamua kuondoka.
KASHESHE LAANZA.
Nilipowasha tu injini ya gari yangu kuna bwana aliekua amevalia mavazi meusi na koti refu jeusi alikuja kwa mwendo wa haraka kuelekea upande wangu(dereva) akitokea upande wa sinema(big screen) ile ambayo hupenda kutumia kuoneshea mpira, alipofika kwangu jambo la kwanza alinisalimia, nilipomjibu alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa polisi, Nikamjibu "Nashukuru kukufahamu"(huku nikimtazama machoni).
Baada ya kumjibu vile kwa namna fulani nahisi nilimpunguza kasi, Akakosa maneno ya kuongea, Akaanza kuulizia leseni yangu, nikamtolea leseni orijino lakini zilikua mbili(moja iliyoisha muda wake na mpya) hapo ndio vuguvugu likaanza.
VUGUVUGU;
Aliniuliza kwa nini namiliki leseni mbili kwa jina moja nikamjibu kuwa moja imeisha muda wake, akataka azishike zote nikamgomea, ila nikamuonesha nikiwa nimezishika na hapo tukapishana, akanitukana tusi moja kubwa sana tena nikiwa na rafiki yangu wa kike, hapo hasira zikanipanda nikamuambia mimi siwezi kukupa chochote, Akanijibu ni lazima nimpe, akapiga hatua moja nyuma akatoa bastola(ra) kiunoni akabadilisha kidude cha kuwekea risasi akaweka kingine,akaikoki akaniwekea kichwani kisha akaniambia nimpe leseni, kwa ubishi wangu nikagoma, akahesabu mpaka tatu kisha akavuta lakini sikusikia paaaah! Wala nini japo mwili mzima ulishalowa jasho, nikapata kiburi huku nikitetemeka nikaendelea kubisha kwa nguvu zote, naye akanisogelea kwa ukaribu zaidi na kisha akashika bastola vizuri tena, kwa mara ya pili nikapatwa na uoga nikamkabidhi leseni zote, akaziangalia kisha akanirudishia na kuondoka zake, na mimi kwa kiburi huku nikitetemeka nilimjibu hovyo huku nikiondoka.
Mpaka sasa siamini kama yule alikua ni askari ama ni tapeli.
ANGALIZO;
Tuwe makini sana tunapotembelea maeneo yale.
Jeshi la polisi inabidi waangaze pale kwani matapeli pia wapo na kama yule jamaa alikua ni askari, ni kwa nini aliamua kutumia nguvu na lugha ya matusi katika mazingira rahisi kiasi kile??
MCHANA MWEMA.
hivi kila mwenye gari ana bastola??!! coco beach kuna kitisho gani cha kusema huwezi kwenda huko na gari bila bastola??!!
Yaelekea mkuu wewe ni mpishi mzuri sana, ndio maana hutaki kuamini. Hiyo ishu ni ukweli kwa asilimia mia, na imenitokea mimi mwenyew jumamosi
Jeshi lenu kwani wewe ni mwanamgambo wa Al-Shabab au Hamas?
Tanzania kuna majeshi yafuatayo na yote ni mali ya umma:
Jeshi la Polisi
Jeshi la Kujenga Taifa
Jeshi la Wananchi
Jeshi la Zimamoto
Jeshi la Uhamiaji
Enewei inawezekana wewe ni Mkurya...
Sehemu yangu ya sita ya ufahamu inanipa alert km hii ni habari ya kutunga au ilioongezwa chumvi isiyotumia upeo wa akili na iliyolenga kutuhabarishanulivyo kidume wa ovyo. Hakuna polisi wala jambazi anayeweza kuigiza kufikia kiwango hiki. Sare za polisi zinajulikana na wakati wa usiku huwa ni wengi. Jambazi anajua wenye gari huwa wamebeba pistol hivyo sidhani km wanaweza kufanya huo mchezo.
Habari zenu wakuu, Natumai mnaendelea vizuri na shughuli za kila siku kwa maendeleo ya taifa letu la Tanganyika.
Ilikua siku ya jumamosi tarehe 12/07/2014.
Mida kati ya saa mbili na saa tatu usiku, baada ya kupata chakula nikaamua mimi na mwenzangu(rafiki wa kike) twende fukwe za coco kupunga upepo na kubadilisha mazingira, Tulipofika(upande wa sinema) hatukutaka kushuka kwenye gari bali tulibaki ndani ya gari huku tulibadilishana mawazo na pia kupiga picha kwa kutumia simu zetu, kuna wakati ilibidi tutoke nje ili kupata madhali nzuri ya kupigia picha, Tulikaa kwa muda wa kama dakika 40 kisha tukaamua kuondoka.
KASHESHE LAANZA.
Nilipowasha tu injini ya gari yangu kuna bwana aliekua amevalia mavazi meusi na koti refu jeusi alikuja kwa mwendo wa haraka kuelekea upande wangu(dereva) akitokea upande wa sinema(big screen) ile ambayo hupenda kutumia kuoneshea mpira, alipofika kwangu jambo la kwanza alinisalimia, nilipomjibu alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa polisi, Nikamjibu "Nashukuru kukufahamu"(huku nikimtazama machoni).
Baada ya kumjibu vile kwa namna fulani nahisi nilimpunguza kasi, Akakosa maneno ya kuongea, Akaanza kuulizia leseni yangu, nikamtolea leseni orijino lakini zilikua mbili(moja iliyoisha muda wake na mpya) hapo ndio vuguvugu likaanza.
VUGUVUGU;
Aliniuliza kwa nini namiliki leseni mbili kwa jina moja nikamjibu kuwa moja imeisha muda wake, akataka azishike zote nikamgomea, ila nikamuonesha nikiwa nimezishika na hapo tukapishana, akanitukana tusi moja kubwa sana tena nikiwa na rafiki yangu wa kike, hapo hasira zikanipanda nikamuambia mimi siwezi kukupa chochote, Akanijibu ni lazima nimpe, akapiga hatua moja nyuma akatoa bastola(ra) kiunoni akabadilisha kidude cha kuwekea risasi akaweka kingine,akaikoki akaniwekea kichwani kisha akaniambia nimpe leseni, kwa ubishi wangu nikagoma, akahesabu mpaka tatu kisha akavuta lakini sikusikia paaaah! Wala nini japo mwili mzima ulishalowa jasho, nikapata kiburi huku nikitetemeka nikaendelea kubisha kwa nguvu zote, naye akanisogelea kwa ukaribu zaidi na kisha akashika bastola vizuri tena, kwa mara ya pili nikapatwa na uoga nikamkabidhi leseni zote, akaziangalia kisha akanirudishia na kuondoka zake, na mimi kwa kiburi huku nikitetemeka nilimjibu hovyo huku nikiondoka.
Mpaka sasa siamini kama yule alikua ni askari ama ni tapeli.
ANGALIZO;
Tuwe makini sana tunapotembelea maeneo yale.
Jeshi la polisi inabidi waangaze pale kwani matapeli pia wapo na kama yule jamaa alikua ni askari, ni kwa nini aliamua kutumia nguvu na lugha ya matusi katika mazingira rahisi kiasi kile??
MCHANA MWEMA.
ndugu majambazi pia husoma alama za nyakati polisi hawezi uliza leseni usiku wana maswali yao kwa muda huo, hiyo ilikuwa ni mis-target kiukweli alikuwa na nia mbaya ila kuna mazingira yalisitisha azma yake.
mkuu sijasema jambazi nimesema raia mwenye nia mbaya kwani hata watoto, vibaka, vidokozi na wengineo sikuhizi wana bastola kwa akili nyepesi jambazi coco beach afuate nini?
Cooking up a Story vilaza mupo wengi
J.W.T.Z= Jeshi la Wakurya Tangu Zamani.
Jambazi aulize driving licence ya nini? labda alikuwa ni kichaa aliyetoroka hospitali.
Uache kufanya ngono kwenye gari...nisamehe kama nimetafsiri vibaya hii story yako..siku nyingine wale vijana wa Shigongo watawapiga picha itakuwa aibu!