Hii ni moja ya speech ya ki.pu.mba.vu na kilo.fa zaidi toka kwa kiongozi kuliko upu.mbavu na ulo.fa aliouna kwa watu waliompa heshima ya kuwa kiongozi wa nchi.Ubinafsishaji anaojaribu kuujutia hapa ndiyo uliompa fursa ya kufanya biashara akiwa ikulu.
Kupitia Sera ya ubinafsishaji aliyoisimamia mwenyewe,aliweza kufungua kampuni ya ANBEN na kujimilikisha kinyume na sheria za nchi mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira.Leo hii anapojaribu kutoa kilio cha machozi ya mamba,anapaswa alisemee hili,akiri hadharani kuwa aliitumia ofisi ya Umma kujinufaisha binafsi.
Ni katika uongozi wake rais wa sasa alisimamia uuzwaji wa nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa huku baadhi ya nyumba hizo zikitolewa kwa "vidosho" wa wanene.
Pamoja na kukiri kushindwa kwake,uongozi wake uliacha majeraha mengi ambayo hayatasahaulika milele.Ni katika uongozi wake Taifa lilishuhudia mauwaji ya wapemba waliouliwa kikatili na majeshi yetu yaliyoapa kuilinda mipaka ya nchi yetu,lakini kwa mara ya kwanza badala ya kuilinda mipaka yetu,yaliwageukia Watanzania na kuwafyeka mithiri ya kuku alaye mayai yake.Kwa Mara ya kwanza nchi yetu ilizalisha wakimbizi baada ya kukimbilia nchi jirani ya Kenya kuukimbia mkono wa chuma na vifaru vya majeshi yetu vilivyokuwa vikiwaswaga kwa amri ya Mkuu wa nchi.
Huu waweza kuwa uchochezi kwa Tafsiri ya Policcm,lakini haya ninayoyaandika si uchochezi bali ni ukweli mchungu ambao viongozi wetu wanatamani waufute katika kumbukumbu za vichwa vyetu lakini hawawezi kwa sababu hawana mamlaka ya kutawala na kuzitiisha akili na dhamiri zetu,wataishia kutawala viwiliwili vyetu tu lakini si ufahamu wetu.
Viwiliwili wanaweza kuvitawala hata kwa taarifa za intelejensia feki ya policcm inayowapa kibali cha kuswaga watu kwa mabomu na Maji ya kuwasha.Unafiki wa watawala wetu na wapambe wao ukijaribu kuuweka katika viwango vya kidunia,waweza kuwa ni unafiki wa kiwango cha PhD.Mtu anakurupuka bungeni mithiri ya msukule na kuiomba serikali ijenge uwanja wa kumbukumbu ya push-ups na bado waziri mwenye dhamana badala ya kukemea upuuzi huo,anamuunga mkono kwa kuahidi kufikiri namna ya kujenga kumbukumbu hiyo.Kati ya push-ups na mauwaji ya Wazanzibar yaliyosimamiwa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ni kipi kilipaswa kujengewa kumbukumbu?Wazanzibar waliouliwa makumi kwa makumi mwaka 2001,maadhimisho yake hadi leo hupigwa marufuku na jeshi la police kana kwamba waliouliwa Zanzibar walikuwa ni magaidi,lakini kutokana na mparaganyiko wa maono ya kiutawala,watu wanaomba kumbukumbu za push-ups na serikali inaridhia,je hoja za aina hii haziwezi kuwa kigezo cha kulifanya Taifa letu kuandikwa kwenye Vitabu vya maajabu ya Dunia kama Taifa la watu wa.pumba.vu zaidi Duniani?
Hii ni nchi ya ajabu sana ambayo ukijipa muda wa kuitafakari unaweza kuishia korokoroni kwa kuitwa mchochezi kwa kuwa tu unajaribu kusema ukweli ambao viongozi wetu hawapendi kuusikia.Mungu tusaidie kupata viongozi wenye hofu ya kweli kuliko hawa wa kumbukumbu za push-ups.Amen.