Mkapa: Najuta

Mkapa: Najuta

Alikuwa jeuri na mbabe sana huyu... msamaha empty tu utasaidia nn...? I don't accept...!! NBC asidanganye watu, MWALIMU ALIPINGA sana sana... na watu wengi wasomi walipinga.. ila yeye alibinafsisha nakuwapa makaburu rafiki zake..!! Kama ana uchungu na nchi hii AKAUZE HOTEL YA KIMATAIFA ILE PALE DURBAN South Africa aliyojengewa na matajiri kama asante... na siku ya ufunguzi wa hotel hiyo ya KIFAHARI, alimwalika Mh. Nelson Mandela na ALIKATAA NA KUMUONA HAFAI, sbb MANDELA ALIJUA NI RUSHWA HIYO na kumwambia pamoja umehongwa na nchi yenu maskini na umepewa asante na matajiri si basi UNGEJENGA HATA KWENU TZ watu wako wapate ajira..!!

Huyu nae ni walewale..!!
 
Ashatu......................Kwa miaka yote ijayo halafu anatuomba msamaha.Kama anajuta amefanya nini kuhusu hilo.Bado juzi kati kaita watu malofa . simuelewi.
 
Ndiyo madhara ya mropokaji (mwandishi wa habari) kuwa rais. Mkapa na JK ni marais useless kuwahi kutokea hapa Tanzania. Mimi wala simsamehe kwani alipokuwa rais huyu mropokaji alikuwa hataki ushauri, alikalia wizi tu. Huyu naye inabidi afunguliwe mashitaka haraka sana.

Afunguliwe mashtaka kwa katiba ipi....!???
 
Huyu nae atuache Watanzania,atatuomba msamaha kwa mangapi?
Unafiki tu.

Alikuwa wapi miaka yote hiyo?

Anataka kututumia Watanzania kama jukwaa la kumfikishia madongo aliyemkabidhi kijiti miaka hiyo.
 
Y
Hivi Mkapa anaweza kutuhakikishia kwamba Mwalimu aliukubali ubinafsishwaji wa NBC?
Huyu jamaa ni muongo, na ndiyo maana kila kukicha nafsi inamhukumu kwa matendo aliyoyafanya akiwa Rais.
Yani hapa ndio kaniacha hoi-afu bado anasema anajuta kosa kwa kuendelea kisema uongo
 
Mkapa ni mtu aliyetumia IQ ndogo ya Watanzania kutawala nchi na kutuingiza matatani
 
Lakini pamoja na ubabe wake Jamaa alikua very logical, watanzania walikosa hoja. Ukichukulia watu walitoka katika mikono ya 'hewala si utumwa'.
Nakumbuka enzi za mtangulizi wake zile kesi za balozi wa nyumba kumi au za serikali ya mtaa zilikua zikisikiliziwa Ikulu chini ya mtangulizi huyo...ilikua ni hadi kesi za wana ndoa au majirani kununiana kwa visa vya eti huyu katoka ghorofani kwake kuja kurusha takataka kwenye ngazi za mlangoni kwetu, maana miaka ile uchafu ndiyo ilikua habari ya mjini.

Sio kwamba watanzania walikosa hoja sema ktk kipindi hicho watanzania walikuwa mbumbumbu alitumia uwezo mdog po wa kifikira wa watanzania kutatawala atakavyo
 
mini-620x308.jpg

Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania

Mkapa: Najuta
Posted by: Wolfram Mwalongo 16 hours

RAIS Mstaafu, Benjamin Mkapa haachi kujuta kutokana na baadhi ya yale aliyoyatenda kwenye utawala wake, anaomba Watanzania wamsamehe, anaandika Wolfram Mwalongo.

Kinachomfanya kujuta ni hatua ya utawala wake kukabidhi ‘injini ya uchumi’ wa taifa hili kwa wawekezaji chini ya ‘sera ya ubinafsishaji.’ Mkapa alikabidhi mashirika ya umma mikononi mwa wawekezaji bila kuwa na mkakati wa kusimamia ili sera yake iwe na tija kwa taifa.

Rais Mkapa alihudumia nchi hii kama rais kuanzia mwaka 1995 hadi 2005. Alipokea madaraka hayo kutoka kwa Rais Ali Hassan Mwingi aliyehudumia nchi kuanzia 1985 mpaka 1995, aliyeanza kuhudumia taifa hili kwenye ngazi hiyo ni Mwalimu Julius K. Nyerere tangu Uhuru 1961.

Akiwa kwenye Tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofayika kwenye Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana Mkapa amekiri kwamba, hatua ya kuleta sera ya ubinafsishaji bila kuweka chombo maalum cha kudhibiti kumesababisha hasara.

Si mara ya kwanza kiongozi huyo mstaafu kusema maneno hayo hasa anapozungumzia maswala mazito katika utawala wake.

“Kukosekana kuundwa mfumo mzuri wa udhibiti kumesababisha kuwepo kwa watu waliotumia fursa hiyo kwa maendeleo yao binafsi na si kwa Taifa.

“Kwenye uongozi wangu kitu ambacho mpaka sasa ninajuitia ni kuanzisha sera ya ubinafsishaji na kushindwa kuweka mfumo au chombo cha kuudhibiti,”amesema Mkapa.

Mara kadhaa wachumi wa kitaifa wamekuwa wakikosoa utawala wa Mkapa kwa kuita wawekezaji na kuwapa ‘mali’ za taifa katika misingi mibovu ya uangalizi wake na kusababisha kuteketea kwa mali hizo. Miongoni mwayo ni viwanda, mashirika ya umma pamoja na Benki.

Mkapa kwenye tamasha hilo amesema “kuhusu ubinafsishaji huo ndio kitu naweza kukiri nilikosea na ninachoweza kuwaomba Watanzania msamaha.”

Mashiriki mengi ya umma pamoja na viwanda vilivyokabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nje vilikufa na wengine kutumia mali hizo za taifa katika kujipatia mikopo na kufanya mambo mengine nje ya malengo yaliyokusudiwa.

Hata hivyo, Mkapa amesema “nilifanya kosa lakini hatuwezi kusema ubinafsishaji haufai kwa sababu ulisaidia kuleta mabadiliko na na kuongeza uzalishaji katika mashirika yaliyokuwa yameshindwa kuendeshwa na serikali.”

Ametoa mfano kwamba, “wakati mimi naingia madarakani viwanda vya sukari vya Mtibwa, Kagera, na Kilombero vilikuwa vikizalisha tani 120,000 hadi 130,000 lakini wakati naondoka niliacha vinazalisha tani 300,000.

“Mtibwa ilikuwa imeishakufa kabisa, lakini tuliweza kukirudisha na baada ya mimi kuondoka vimeendelea kuzalisha lakini inashangaza kuona miaka 17 wameshindwa kuongeza uzalishaji.”

Hata hivyo Mpaka alirudisha lawama kwa Watanzania kwamba, wana hulka ya kuzungumzia zaidi watu kuliko kuzungumzia sera na kuziboresha ili ziwe na tija kwa taifa.

Kwenye hotaba yake Mpaka amesema kuwa, Mwalimu Nyerere alishughulishwa katika kutafuta maendeleo ya Watanzania na kwamba, hakupinga ubinafsishaji kwenye taifa hili.

“Mwalimu Nyerere alikubali dhana ya ujasiriamali, uwekezaji, ushindani, ubunifu, ufanisi na utengenezaji wa faida vitu ambavyo viko sambamba na Ubepari,” amesema Mkapa na kuongeza;

“Vitu alikuwa anavitaka Mwalimu ni baadhi ya mambo mabaya ya Ubepari ikiwemo unyonyaji na mgawanyo wa faida usio sawa na ndio maana akaweka Azimio la Arusha akilenga kuwa na jamii ya usawa isiyo na unyonyaji.”

Akizungumzia ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) amesema, Mwalimu Nyerere aliona faida za ubinafsishaji na kwamba, aliona umuhimu wa kuibinafsisha benki hiyo.

“Kuhusu NBC Mwalimu si kwamba alikuwa anapinga kuibinafsisha bali ni namna ambavyo inaweza kuwanufaisha wananchi baada ya kuibinafsisha,” amesema Mkapa.

1. Watu wengi waliathirika na ubunafsishaji wa baadhi ya mashirika ya umma kwa mfn pale TRC idadi kubwa walipoteza ajira.

Mkapa anajua mateso ya kukosa ajira?

2. Sekta za reli na bandari zimekufa au kuzorota na kuathiri uchumi wa nchi vibaya sana. Je Mkapa anajua hasara ya jambo hili?

3. Uamuzi wake wa kubinafsisha mashirika hayo ulihusu pia uuzaji wa ardhi (viwanja) na nyumba za wafanyakazi wa mashirika hayo!

Mkapa anasema nini kuhusu makosa haya na atafanya mini ili nyumba na ardhi hizo zirudishwe ili mashirika hayo yasiathirike kiuendeshaji kwa kukosa nyumba za wafanyakazi na maeneo ya ardhi ambayo yangetumika kwa mahitaji mengine?

4. Hivi kubinafsisha Kongolo Quarry ya TAZARA na Tura Quarry ya TRC ili mashirika haya yanunue mawe yaani kokoto kwa mwekezaji; kwa akili ya kawaida tu, na hili Mkapa anaona lilikuwa jambo la busara?

Kwa mtazamo makini, huwezi kukwepa uwezekano wa 'vimelea' vya ufisadi kwenye zoezi zima la ubinafsishaji wa sekta hizi; kiasi kwamba haitoshi kwa Mkapa kusema tu kuwa anakubali makosa. Labda aseme mwenyewe atawajibika vipi kwa madhambi haya?

Hawezi kusema anakiri makosa halafu anakuwa mkali na kukemea wanaofuatilia mambo haya kwamba 'wasiwe walalamikaji' au wasiwajadili watu binafsi nk. nk.; Ukiwa Rais wa nchi lazima tukujadili we we binafsi kwasababu Ikulu ni mahali PATAKATIFU. Sio sehemu ya kwenda kujaribu au kubahatisha mambo yako kwa gharama ya uhai wa taifa zima!
Halafu ukiulizwa Katiba mpya ilikwama vipi unakwepa swali! Lakini wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ulionekana unapanda majukwaani kuwatetea wana CCM wenzako waliozima harakati za katiba mpya!

Niseme tu, jamani! Nahisi kwamba Mkapa hajutii makosa yake wala hana muda na vitu kama Demokrasia ya vyama vingi, Utawala Bora au Ukweli na Uwazi aliouhubiri enzi zake. Bali kwake ni lazima CCM yake iendelee kutwawala, na kwa gharama yoyote.

Ndiyo maana nadiriki kusema Mkapa hawezi kusema kitu kuhusu mgogoro wa Zanzibar. Kwake kilichofanyika huko ni demokrasia. Tena nadhani akiulizwa jambo kuhusu hilo atakuwa mkali kweli kweli!
Mimi namsamehe.
 
mini-620x308.jpg

Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania

Mkapa: Najuta
Posted by: Wolfram Mwalongo 16 hours

RAIS Mstaafu, Benjamin Mkapa haachi kujuta kutokana na baadhi ya yale aliyoyatenda kwenye utawala wake, anaomba Watanzania wamsamehe, anaandika Wolfram Mwalongo.

Kinachomfanya kujuta ni hatua ya utawala wake kukabidhi ‘injini ya uchumi’ wa taifa hili kwa wawekezaji chini ya ‘sera ya ubinafsishaji.’ Mkapa alikabidhi mashirika ya umma mikononi mwa wawekezaji bila kuwa na mkakati wa kusimamia ili sera yake iwe na tija kwa taifa.

Rais Mkapa alihudumia nchi hii kama rais kuanzia mwaka 1995 hadi 2005. Alipokea madaraka hayo kutoka kwa Rais Ali Hassan Mwingi aliyehudumia nchi kuanzia 1985 mpaka 1995, aliyeanza kuhudumia taifa hili kwenye ngazi hiyo ni Mwalimu Julius K. Nyerere tangu Uhuru 1961.

Akiwa kwenye Tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofayika kwenye Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana Mkapa amekiri kwamba, hatua ya kuleta sera ya ubinafsishaji bila kuweka chombo maalum cha kudhibiti kumesababisha hasara.

Si mara ya kwanza kiongozi huyo mstaafu kusema maneno hayo hasa anapozungumzia maswala mazito katika utawala wake.

“Kukosekana kuundwa mfumo mzuri wa udhibiti kumesababisha kuwepo kwa watu waliotumia fursa hiyo kwa maendeleo yao binafsi na si kwa Taifa.

“Kwenye uongozi wangu kitu ambacho mpaka sasa ninajuitia ni kuanzisha sera ya ubinafsishaji na kushindwa kuweka mfumo au chombo cha kuudhibiti,”amesema Mkapa.

Mara kadhaa wachumi wa kitaifa wamekuwa wakikosoa utawala wa Mkapa kwa kuita wawekezaji na kuwapa ‘mali’ za taifa katika misingi mibovu ya uangalizi wake na kusababisha kuteketea kwa mali hizo. Miongoni mwayo ni viwanda, mashirika ya umma pamoja na Benki.

Mkapa kwenye tamasha hilo amesema “kuhusu ubinafsishaji huo ndio kitu naweza kukiri nilikosea na ninachoweza kuwaomba Watanzania msamaha.”

Mashiriki mengi ya umma pamoja na viwanda vilivyokabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nje vilikufa na wengine kutumia mali hizo za taifa katika kujipatia mikopo na kufanya mambo mengine nje ya malengo yaliyokusudiwa.

Hata hivyo, Mkapa amesema “nilifanya kosa lakini hatuwezi kusema ubinafsishaji haufai kwa sababu ulisaidia kuleta mabadiliko na na kuongeza uzalishaji katika mashirika yaliyokuwa yameshindwa kuendeshwa na serikali.”

Ametoa mfano kwamba, “wakati mimi naingia madarakani viwanda vya sukari vya Mtibwa, Kagera, na Kilombero vilikuwa vikizalisha tani 120,000 hadi 130,000 lakini wakati naondoka niliacha vinazalisha tani 300,000.

“Mtibwa ilikuwa imeishakufa kabisa, lakini tuliweza kukirudisha na baada ya mimi kuondoka vimeendelea kuzalisha lakini inashangaza kuona miaka 17 wameshindwa kuongeza uzalishaji.”

Hata hivyo Mpaka alirudisha lawama kwa Watanzania kwamba, wana hulka ya kuzungumzia zaidi watu kuliko kuzungumzia sera na kuziboresha ili ziwe na tija kwa taifa.

Kwenye hotaba yake Mpaka amesema kuwa, Mwalimu Nyerere alishughulishwa katika kutafuta maendeleo ya Watanzania na kwamba, hakupinga ubinafsishaji kwenye taifa hili.

“Mwalimu Nyerere alikubali dhana ya ujasiriamali, uwekezaji, ushindani, ubunifu, ufanisi na utengenezaji wa faida vitu ambavyo viko sambamba na Ubepari,” amesema Mkapa na kuongeza;

“Vitu alikuwa anavitaka Mwalimu ni baadhi ya mambo mabaya ya Ubepari ikiwemo unyonyaji na mgawanyo wa faida usio sawa na ndio maana akaweka Azimio la Arusha akilenga kuwa na jamii ya usawa isiyo na unyonyaji.”

Akizungumzia ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) amesema, Mwalimu Nyerere aliona faida za ubinafsishaji na kwamba, aliona umuhimu wa kuibinafsisha benki hiyo.

“Kuhusu NBC Mwalimu si kwamba alikuwa anapinga kuibinafsisha bali ni namna ambavyo inaweza kuwanufaisha wananchi baada ya kuibinafsisha,” amesema Mkapa.

Jamani tunahitaji katiba mpya...Huyu Mkapa si wa kutuomba msamaha wala kuongea hadharani kwani ilibidi akamatwe kitambo kwa kuifilisi nchi na wizi alioufanya yeye na mkewe kipindi akiwa rais. Eti leo anatuomba msamaha? Huyu anatusanifu tu, inabidi akamatwe haraka sana.
 
Huyu nae atuache Watanzania,atatuomba msamaha kwa mangapi?
Unafiki tu.
Alikuwa wapi miaka yote hiyo?
Anataka kututumia Watanzania kama jukwaa la kumfikishia madongo aliyemkabidhi kijiti miaka hiyo.
Kijiti akamuachia Vasco Da Gama.... the discoverer of new lands overseas....

masikini...

Mi nasema MAGUFULI aongeze tu udictator.. maradufu.
 
crocodile tears... Machozi ya mamba ni ya unafiki sio kwamba anakuonea huruma kama haujui mamba anapootea mnyama au mtu na kumkamata pale anapokuwa anamtafuna huwa anatafuna mpaka anatokwa na machozi lakini ndo anafurahia utamu hivyo, ni sawa na hawa vigogo waliojilimbikizia mali za watanzania alafu wanajifanya kutuonea huruma mambo yanavyozidi kuwa magumu
 
Tubadili katiba watu kama hawa wakaozee jela tu...huwezi kuisababishia nchi hasara halafu eti uombe msamaha kirahisirahisi
 
NBC inaniuma mpaka leo.......na mkapa asitudanganye eti hata mwalimu alitaka NBC iuzwe....wakati nyerere mpaka anakufa analalamikia kuhusu nbc.....tunamuomba awe mkweli........mwalimu mpaka aliuliza kuwa "can nbc open a branch in new york"?...
Katika utawala wake alibinafsisha ziwa Victoria kwa miaka 99 kitu ambacho kimewafanya wananchi kuishi ka maskini kwenye nchi yao wakati Mungu aliwapa ziwa liwakomboe. Leo wanaishia kuogelea tu na kupiga picha basi lakini kuhusu kitoweo haipo tena, wanakula mabaki tu na mifupa. Katika hili kamwe siwezi kumsahau mkapa
 
Nani wa kumfunga paka kengele? mswada upelekwa bungeni wa rais mstaafu kushitakiwa akiwe ameboronga, je?nan hataupeleka huo mswada???
 
mini-620x308.jpg

Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania

Mkapa: Najuta
Posted by: Wolfram Mwalongo 16 hours

RAIS Mstaafu, Benjamin Mkapa haachi kujuta kutokana na baadhi ya yale aliyoyatenda kwenye utawala wake, anaomba Watanzania wamsamehe, anaandika Wolfram Mwalongo.

Kinachomfanya kujuta ni hatua ya utawala wake kukabidhi ‘injini ya uchumi’ wa taifa hili kwa wawekezaji chini ya ‘sera ya ubinafsishaji.’ Mkapa alikabidhi mashirika ya umma mikononi mwa wawekezaji bila kuwa na mkakati wa kusimamia ili sera yake iwe na tija kwa taifa.

Rais Mkapa alihudumia nchi hii kama rais kuanzia mwaka 1995 hadi 2005. Alipokea madaraka hayo kutoka kwa Rais Ali Hassan Mwingi aliyehudumia nchi kuanzia 1985 mpaka 1995, aliyeanza kuhudumia taifa hili kwenye ngazi hiyo ni Mwalimu Julius K. Nyerere tangu Uhuru 1961.

Akiwa kwenye Tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofayika kwenye Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana Mkapa amekiri kwamba, hatua ya kuleta sera ya ubinafsishaji bila kuweka chombo maalum cha kudhibiti kumesababisha hasara.

Si mara ya kwanza kiongozi huyo mstaafu kusema maneno hayo hasa anapozungumzia maswala mazito katika utawala wake.

“Kukosekana kuundwa mfumo mzuri wa udhibiti kumesababisha kuwepo kwa watu waliotumia fursa hiyo kwa maendeleo yao binafsi na si kwa Taifa.

“Kwenye uongozi wangu kitu ambacho mpaka sasa ninajuitia ni kuanzisha sera ya ubinafsishaji na kushindwa kuweka mfumo au chombo cha kuudhibiti,”amesema Mkapa.

Mara kadhaa wachumi wa kitaifa wamekuwa wakikosoa utawala wa Mkapa kwa kuita wawekezaji na kuwapa ‘mali’ za taifa katika misingi mibovu ya uangalizi wake na kusababisha kuteketea kwa mali hizo. Miongoni mwayo ni viwanda, mashirika ya umma pamoja na Benki.

Mkapa kwenye tamasha hilo amesema “kuhusu ubinafsishaji huo ndio kitu naweza kukiri nilikosea na ninachoweza kuwaomba Watanzania msamaha.”

Mashiriki mengi ya umma pamoja na viwanda vilivyokabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nje vilikufa na wengine kutumia mali hizo za taifa katika kujipatia mikopo na kufanya mambo mengine nje ya malengo yaliyokusudiwa.

Hata hivyo, Mkapa amesema “nilifanya kosa lakini hatuwezi kusema ubinafsishaji haufai kwa sababu ulisaidia kuleta mabadiliko na na kuongeza uzalishaji katika mashirika yaliyokuwa yameshindwa kuendeshwa na serikali.”

Ametoa mfano kwamba, “wakati mimi naingia madarakani viwanda vya sukari vya Mtibwa, Kagera, na Kilombero vilikuwa vikizalisha tani 120,000 hadi 130,000 lakini wakati naondoka niliacha vinazalisha tani 300,000.

“Mtibwa ilikuwa imeishakufa kabisa, lakini tuliweza kukirudisha na baada ya mimi kuondoka vimeendelea kuzalisha lakini inashangaza kuona miaka 17 wameshindwa kuongeza uzalishaji.”

Hata hivyo Mpaka alirudisha lawama kwa Watanzania kwamba, wana hulka ya kuzungumzia zaidi watu kuliko kuzungumzia sera na kuziboresha ili ziwe na tija kwa taifa.

Kwenye hotaba yake Mpaka amesema kuwa, Mwalimu Nyerere alishughulishwa katika kutafuta maendeleo ya Watanzania na kwamba, hakupinga ubinafsishaji kwenye taifa hili.

“Mwalimu Nyerere alikubali dhana ya ujasiriamali, uwekezaji, ushindani, ubunifu, ufanisi na utengenezaji wa faida vitu ambavyo viko sambamba na Ubepari,” amesema Mkapa na kuongeza;

“Vitu alikuwa anavitaka Mwalimu ni baadhi ya mambo mabaya ya Ubepari ikiwemo unyonyaji na mgawanyo wa faida usio sawa na ndio maana akaweka Azimio la Arusha akilenga kuwa na jamii ya usawa isiyo na unyonyaji.”

Akizungumzia ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) amesema, Mwalimu Nyerere aliona faida za ubinafsishaji na kwamba, aliona umuhimu wa kuibinafsisha benki hiyo.

“Kuhusu NBC Mwalimu si kwamba alikuwa anapinga kuibinafsisha bali ni namna ambavyo inaweza kuwanufaisha wananchi baada ya kuibinafsisha,” amesema Mkapa.
Wengi hawatomsamehe
 
Na inaniuma kwa mauaji yaliyotokea Mwembechai na Zanzibar wakati wa Utawala wake kwa kweli inauma sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mimi namkumbuka tu Mkapa kama kiongozi aliyekosa mbinu za kuinua uchumi na kupata fedha za kuendesha nchi, jambo lililosababisha aamue kuuza nyumba 8000 na kuuza mashirika zaidi ya 360 kwa bei chee ili apate pesa za kuendesha nchi.
Namkumbuka sana kwa huu usanii na ukosefu wa mipango wa kuinua uchumi hata kwa kukodisha au kupangisha zile nyumba za umma zilizouzwa kwa bei ya kodi ya kupangisha kwa mwaka mmoja tu.

Watanzania inabidi tumsamehe tu mana sisi ndio tuliamua wenyewe kumpa nchi na katiba inayomfanya aiendeshe nchi kama mali yake binafsi.
Aliitendea haki katiba yake na kuwafanya wananchi waisome namba.
Mpaka leo bado tunaendelea kuwapa watu wale wale madaraka kwa kutumia katiba ile ile yenye mambo yale yale chini ya chama kile kile na idadi kubwa ya wabunge wa chama kile kile.

Wakiwa madarakani wanazungukwa na wapambe wengi wa kuwakingia kifua ili wasikosolewe lakini wanapoondoka ndipo tunaanza kuwaomba waje kuomba msamaha kwa mambo ambayo walikua wameshaonywa na kuambiwa kuwa wanakosea wakakaidi.
 
Back
Top Bottom