Mkapa: Najuta

Mkapa: Najuta

Lakini pamoja na ubabe wake Jamaa alikua very logical, watanzania walikosa hoja. Ukichukulia watu walitoka katika mikono ya 'hewala si utumwa'.
Nakumbuka enzi za mtangulizi wake zile kesi za balozi wa nyumba kumi au za serikali ya mtaa zilikua zikisikiliziwa Ikulu chini ya mtangulizi huyo...ilikua ni hadi kesi za wana ndoa au majirani kununiana kwa visa vya eti huyu katoka ghorofani kwake kuja kurusha takataka kwenye ngazi za mlangoni kwetu, maana miaka ile uchafu ndiyo ilikua habari ya mjini.
Nakiri sijawahi kusoma comment ya uongo kama hii! Hivi huamini kuwa uongo ni dhambi na utahukumiwa juu ya uongo??
 
Alikuwa na lundo la washauri nguli wa masuala mbalimbali. Alikuwa na mawaziri, wabunge, RC's & DC's et al.
Kwanin aombe msamaha yeye? Ina maana hakufuata alichokuwa anashauriwa?
 
Sipendeleagi kusema haya but nimelazimika kuyasema walau kidogo; tokea nchi imepata Uhuru Magufuli ni rais 5 kukaa Ikulu na anafanya kua rais 3 Mkristo.

Hawa 4 (Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete) ni 2 tu ndio nimewahi kuwasikia kwa masikio yangu na kuwasoma wakiomba msamaha mahali walipokosea, tena wote wameomba msamaha zaidi ya mara 1 na wamefanya hivyo hadharani; ni Nyerere na Mkapa.

Sijui ni kwasababu ya malezi ya dini zao kwamba lazima mtu atubie makosa na maovu yao au ni unyenyekevu (ambao nao still umekaa kimalazi ya Kikristo zaidi).

Sina kumbukumbu kama nimwahi kumsikia Mwinyi na Kikwete kuomba msamaha (Mwenye kumbukumbu anikumbushe).

Swali ninalo jiuliza, hivi hawa wengine ni kwasababu ya malezi ya kidini au misimamo ya dini zao au imetokea tu kama coincidence? Mwenye uelewa tafadhari.
 
haya buana ngoja tumsubiri HB wa msoga kama na yeye ataomba radhi,maana ule mchakato wa katiba ulikula pesa nyingi sana.
 
Shetani akizeeka anakuwa malaika .... kumbuka kauli hii toka mmoja wa wale alokuwa nao kwenye uongozi
"Ndege ya rais lazima inunuliwe hata kama wananchi watakula nyasi"
 
Sipendeleagi kusema haya but nimelazimika kuyasema walau kidogo; tokea nchi imepata Uhuru Magufuli ni rais 5 kukaa Ikulu na anafanya kua rais 3 Mkristo. Hawa 4 (Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete) ni 2 tu ndio nimewahi kuwasikia kwa masikio yangu na kuwasoma wakiomba msamaha mahali walipokosea, tena wote wameomba msamaha zaidi ya mara 1 na wamefanya hivyo hadharani; ni Nyerere na Mkapa. Sijui ni kwasababu ya malezi ya dini zao kwamba lazima mtu atubie makosa na maovu yao au ni unyenyekevu (ambao nao still umekaa kimalazi ya Kikristo zaidi). Sina kumbukumbu kama nimwahi kumsikia Mwinyi na Kikwete kuomba msamaha (Mwenye kumbukumbu anikumbushe). Swali ninalo jiuliza, hivi hawa wengine ni kwasababu ya malezi ya kidini au misimamo ya dini zao au imetokea tu kama coincidence? Mwenye uelewa tafadhari.

Ni coincidence tu mkuu. Hakuna dini isiyofundisha kuomba msamaha au kufanya toba baada ya kukosea
 
mini-620x308.jpg

Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania

Mkapa: Najuta
Posted by: Wolfram Mwalongo 16 hours

RAIS Mstaafu, Benjamin Mkapa haachi kujuta kutokana na baadhi ya yale aliyoyatenda kwenye utawala wake, anaomba Watanzania wamsamehe, anaandika Wolfram Mwalongo.

Kinachomfanya kujuta ni hatua ya utawala wake kukabidhi ‘injini ya uchumi’ wa taifa hili kwa wawekezaji chini ya ‘sera ya ubinafsishaji.’ Mkapa alikabidhi mashirika ya umma mikononi mwa wawekezaji bila kuwa na mkakati wa kusimamia ili sera yake iwe na tija kwa taifa.

Rais Mkapa alihudumia nchi hii kama rais kuanzia mwaka 1995 hadi 2005. Alipokea madaraka hayo kutoka kwa Rais Ali Hassan Mwingi aliyehudumia nchi kuanzia 1985 mpaka 1995, aliyeanza kuhudumia taifa hili kwenye ngazi hiyo ni Mwalimu Julius K. Nyerere tangu Uhuru 1961.

Akiwa kwenye Tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofayika kwenye Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana Mkapa amekiri kwamba, hatua ya kuleta sera ya ubinafsishaji bila kuweka chombo maalum cha kudhibiti kumesababisha hasara.

Si mara ya kwanza kiongozi huyo mstaafu kusema maneno hayo hasa anapozungumzia maswala mazito katika utawala wake.

“Kukosekana kuundwa mfumo mzuri wa udhibiti kumesababisha kuwepo kwa watu waliotumia fursa hiyo kwa maendeleo yao binafsi na si kwa Taifa.

“Kwenye uongozi wangu kitu ambacho mpaka sasa ninajuitia ni kuanzisha sera ya ubinafsishaji na kushindwa kuweka mfumo au chombo cha kuudhibiti,”amesema Mkapa.

Mara kadhaa wachumi wa kitaifa wamekuwa wakikosoa utawala wa Mkapa kwa kuita wawekezaji na kuwapa ‘mali’ za taifa katika misingi mibovu ya uangalizi wake na kusababisha kuteketea kwa mali hizo. Miongoni mwayo ni viwanda, mashirika ya umma pamoja na Benki.

Mkapa kwenye tamasha hilo amesema “kuhusu ubinafsishaji huo ndio kitu naweza kukiri nilikosea na ninachoweza kuwaomba Watanzania msamaha.”

Mashiriki mengi ya umma pamoja na viwanda vilivyokabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nje vilikufa na wengine kutumia mali hizo za taifa katika kujipatia mikopo na kufanya mambo mengine nje ya malengo yaliyokusudiwa.

Hata hivyo, Mkapa amesema “nilifanya kosa lakini hatuwezi kusema ubinafsishaji haufai kwa sababu ulisaidia kuleta mabadiliko na na kuongeza uzalishaji katika mashirika yaliyokuwa yameshindwa kuendeshwa na serikali.”

Ametoa mfano kwamba, “wakati mimi naingia madarakani viwanda vya sukari vya Mtibwa, Kagera, na Kilombero vilikuwa vikizalisha tani 120,000 hadi 130,000 lakini wakati naondoka niliacha vinazalisha tani 300,000.

“Mtibwa ilikuwa imeishakufa kabisa, lakini tuliweza kukirudisha na baada ya mimi kuondoka vimeendelea kuzalisha lakini inashangaza kuona miaka 17 wameshindwa kuongeza uzalishaji.”

Hata hivyo Mpaka alirudisha lawama kwa Watanzania kwamba, wana hulka ya kuzungumzia zaidi watu kuliko kuzungumzia sera na kuziboresha ili ziwe na tija kwa taifa.

Kwenye hotaba yake Mpaka amesema kuwa, Mwalimu Nyerere alishughulishwa katika kutafuta maendeleo ya Watanzania na kwamba, hakupinga ubinafsishaji kwenye taifa hili.

“Mwalimu Nyerere alikubali dhana ya ujasiriamali, uwekezaji, ushindani, ubunifu, ufanisi na utengenezaji wa faida vitu ambavyo viko sambamba na Ubepari,” amesema Mkapa na kuongeza;

“Vitu alikuwa anavitaka Mwalimu ni baadhi ya mambo mabaya ya Ubepari ikiwemo unyonyaji na mgawanyo wa faida usio sawa na ndio maana akaweka Azimio la Arusha akilenga kuwa na jamii ya usawa isiyo na unyonyaji.”

Akizungumzia ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) amesema, Mwalimu Nyerere aliona faida za ubinafsishaji na kwamba, aliona umuhimu wa kuibinafsisha benki hiyo.

“Kuhusu NBC Mwalimu si kwamba alikuwa anapinga kuibinafsisha bali ni namna ambavyo inaweza kuwanufaisha wananchi baada ya kuibinafsisha,” amesema Mkapa.
Naumbuka aliiuza nbc kwa bei ya kukata tamaaa na sijui ni kitu gani kilimpata huyo achimwene
 
Tunaweza kudhani kaomba msamaha katika hali ya kawaida ya majuto ya kibinadamu, tunaweza kudhani kwamba kaamua kuwa muungwana na kufanya kitubio ili abaki na amani LAKINI katika picha pana ni salamu kwa Jakaya ni salamu za kutaka naye ajitokeze na kukiri pale alipokosea....halafu?
Ni salamu pia kwa Magufuri kwamba a jifunze kutokana na makosa ya watangulizi wake na kikubwa ASIKILIZE maoni ya wengine ASIKILIZE wananchi wanataka nini kwakuwa huko tuendako hakutakuwa na nafasi ya kuomba msamaha ukiwa jukwaani umevaa suti unasikilizwa bila kuhojiwa huku ukipigiwa makofi..!
Umeelezea vema mkuu, lkn kwa mfumo wetu huu tulio nao wa watawala kwenda kwenda kwenye majukwaa na huku wamezungukwa mitutu huo ujasiri wa kuwahoji na kuwataka waeleze nini wametufanyia tunaweza kuupata wapi?
 
Nakumbuka alikuwa mbishi ka nini eti Leo ndo anaomba msamaha basi tutarajie na jk kuomba msamaha baada ya miaka kadhaa mbele.
Hakuna cha kuomba msamaha huyo ni muongo mbona hajaomba msamaha kwa watanzania alio waita malofa?hivi huo msamaha anawaomba hao hao malofa au kuna watanzania welevu wamezaliwa?
 
kaka! hata tusipomsamehe tutamfanya nini sisi wananchi wa kawaida? acha tu nafsi yake imsute imuhukumu, katunyonya sana wanyonge na jasho letu linamuelemea hajui atalipeleka wapi naye umri wa kufa unakaribia, si alidhani dunia ndo kila kitu akasahau kujiwekea hazina ya faraja mbinguni!
Mkuu binadamu wengi wanajisahu sana, hawa watawala wakiona wamezungukwa na walinzi na mitutu na magari ya delaya wanadhani hakuna hukumu ya mungu
 
Tunaweza kudhani kaomba msamaha katika hali ya kawaida ya majuto ya kibinadamu, tunaweza kudhani kwamba kaamua kuwa muungwana na kufanya kitubio ili abaki na amani LAKINI katika picha pana ni salamu kwa Jakaya ni salamu za kutaka naye ajitokeze na kukiri pale alipokosea....halafu?
Ni salamu pia kwa Magufuri kwamba a jifunze kutokana na makosa ya watangulizi wake na kikubwa ASIKILIZE maoni ya wengine ASIKILIZE wananchi wanataka nini kwakuwa huko tuendako hakutakuwa na nafasi ya kuomba msamaha ukiwa jukwaani umevaa suti unasikilizwa bila kuhojiwa huku ukipigiwa makofi..!

Wewe umenena
 
MH. MKAPA: Wasomi WAACHE KULALAMIKA NA KUJIKITA KWENYE TAFITI ZAIDI.
Raisi mastaafu Mh. Benjamini William Mkapa amewataka wasomi kuacha tabia ya kulalamika na badala yake wajikite zaidi kwenye tafiti zikakazo saidia nchi. Pamoja na hayo mh. Mkapa pia ametolea ufafanuzi mada mbalimbali ikiwemo swala la ubinafsishaji na katiba.
 
Kuomba msamaha sio kitu kibaya bali ni njia mojawapo ya kujutia kosa ingawa wakati mwingine msamaha unaweza kuwa wa kinafiki tu.
 
Kuomba msamaha sio kitu kibaya bali ni njia mojawapo ya kujutia kosa ingawa wakati mwingine msamaha unaweza kuwa wa kinafiki tu.
Hata muomba msamaha inaweza kuwa mnafiki pia
 
Back
Top Bottom