William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amesema, hakuna Mtanzania anayeweza kudiriki kumzomea kwa kuwa rekodi ya utendaji wake kitaifa na kimataifa inaendelea kumlinda. Mkapa amelakiwa kwa kishindo katika ziara ya siku moja wilayani Kilolo mkoani Iringa.
mimi niko ‘busy' sana na shughuli za kimataifa baada ya kumaliza utumishi wangu serikalini," amesema Mkapa.
Mkapa amesema, baada ya kumaliza urais wake amekuwa akijihusisha na shughuli mbalimbali za kimataifa zinazomfanya awe safarini muda mwingi akishughulikia uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na nchi nyingine;
CHANZO: Habari Leo
Ngalikihinja,BEING BETTER DOES NOT TAKE AWAY YOUR PROBLEMS.............. yale ya kiwira anatakiwa ajizomee mwenyewe............. uzuri ni kuwa nafsi za binadamu huwa zina kawaida ya kujishitaki pindi mtu anapofanya visivyo..............
Jamani nimesoma maoni yote ya watu humu, kwa kusema kweli na pia tuache unafiki, Mkapa alifanya kazi kubwa sana ambayo huwezi kulinganisha. Mimi namkubali sana jamaa, ukianzia kuinua mapato ya serekali, hazina ya fedha za kigeni BOT, ubinafsishaji ambao umeongeza ajira, barabara, Uwanja mkuu wa Taifa, Daraja kubwa la Rufiji, utendaji kazi masaa mengi ofisini na safari chache za nje, alipambana na mfumuko wa bei (mkate haba Dar ulikua TShs 150,sasa zaidi ya 700, Unga wa sembe ulikua Tshs 250, sasa 900, Daladala ilikua 150 kwa 50 kwa muda mrefu. Amepunguza madeni ya nje
Tumwache apumzike jamaa alifanya kazi kubwa Sana, ila hamna mtu ambaye ni Mungu au Malaika asiye na makosa. Kama swala ni kufanya biashara je ni wangapi wanafanya kwa kupitia migongo ya ndugu zao? Si afadhali huyu alifanya mwenyewe? Mimi nakwambia Tanzania ni kubwa sana, kwa hiyo alifanya mambo mazuri sana jamaa.
Unajua performance ya mtu inabidi uipime kwa kulinganisha na tulikotoka, Mkapa alipokea nchi ikiwa katika hali mbaya sana, vijana walikua hawataki shule, serekali ilikua haina hela, shule ilikua haithaminiki, hospitali dawa kulikua hamna, yeye alipambana kufa na kupona. Vyote tunavyojivunia sasa vimetoka kwenye uongozi wake.
Swala hapa ni kuchambua kwa upeo wa mpana wa kiuchumi na sio kuleta siasa, unayesema mkapa hakufanya kitu je ni nani aliyefanya? Hamna aliyemsafi 100%
Wanaoamini biblia, Yesu aliletewa mwanamke moja mzinzi na watu wengi. Ila kwa sheria ya kiyahudi ilimpasa kupigwa mawe hadi kufa. Yesu akawaambia makutano, kwa yeyote anayejiona hana dhambi yeyote awe wa kwanza kumpiga jiwe, Yesu akainama chini akawa anachora kwa kidole chini, hapo alikua anandika amri za Mungu. Aliponyanyua kichwa hakumkuta mtu hata mmoja, na akamwamuru yule mama aende zake na asirudie tena dhambi. Kwa mfano huu, anayejiona hana dhami yeyote awe wa kwanza kumyooshea mkapa kidole.
Amefanya makubwa sana, tumwache apumzike
Huyu anajizomea mwenyewe. Kamwe tusingemsikia hata siku moja Mwalimu anauliza swali la kipumbavu kama hili. Anajishuku sana, muungano bado miezi miwili I hope sherehe za Kitaifa zitakuwa Dar na yeye aamue kuingizana pale uwanja wa Taifa bila kujifichaficha watu wampe haki yake.
Hakuna aliyemzomea....
Hakuna aliyemuuliza kama alijigawia Kiwira
Hakuna aliyemuuliza kama yeye sasa ana mali kiasi gani....hakuna!
..iweje sasa, si huku ndiko wanakukaribisha huku? angalia tu mavazi ya waliohudhuria huo mkutano... ni watu wa kutoa sauti za kuzomea hao, au??
gublack,Ndugu wanaogopa
Hukumsikia Lowasa, miongoni mwao hakuna msafi hata moja, kikubwa nani atadhubutu kuanza kumfunga paka kengele????? ukianza kuwapeka mahakamani hutawamaliza, naamini wanaambiana wewe bwana ukingia nilinde mie nilimlinda aliyenitangulia, Hatujawa na huo uthubutu hata kidogo ndugu yangu
Huyu anajizomea mwenyewe. Kamwe tusingemsikia hata siku moja Mwalimu anauliza swali la kipumbavu kama hili. Anajishuku sana, muungano bado miezi miwili I hope sherehe za Kitaifa zitakuwa Dar na yeye aamue kuingizana pale uwanja wa Taifa bila kujifichaficha watu wampe haki yake.
gublack,
Nashauri tujaribu, aliekuwa Rais wa marekani Richard Nixon alisema:"Tray and fail, but never fail to tray" (Jaribu ushindwe, lakini usishindwe/usiache kujaribu)
Mwalimu JK Nyerere mara nyingi alikuwa akikumbusha: Tumeonewa kiasi cha kutosha
Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha na
Tumepuuzwa kiasi cha kutosha.
Na Unyonge wetu ndio uliotufanya Tuonewe, Tunyanyaswe na Tupuuzwe. Na akatutaka tulete Mapinduzi ya kujitoa katika hali hizo. Naamini Mwalimu alikuwa Akiwalenga Wakoloni Weupe/Wageni.
Leo hii tuna WAKOLONI WEUSI, ndugu zetu, kakazetu, dadazetu, Damu yetu wenyewe inatutia MASHAKANI utathubutu kusema Afadhali ya Mkoloni. Hivyo ndhani wakati umefika:
Tujadili njia za kuyageuza maneno yetu kuwa vitendo:
Nimeyasema haya katika thread nyingine naona niyarudie hapa kuna umuhimu wa Walk the Walk badala ya Talk the Talk! Naona wakati umefika kwa JF kuwa na "ACTION GROUP" ili kujaribu kukabiliana na baadhi matatizo yanyosababishwa na viongozi wetu kwa vitendo. Kwa wale mliotanguli kujiunga na kuchangia mawazo kila uchao mniwie radhi in advance ikiwa ninakosea, lakini tumekuwa wazungumzaji na watoa lawama, au Wafagiliaji wa kambi A na Wapondaji wa Kambi B, Wakati ukweli wa mambo ni kuwa Kambi zote hizo zimeoza zinakwenda kwa amri ya Mungu tu.
Matatizo ya UFISADI,RUSHWA,UBADHIRIFU WA MALI ZA TAIFA,UONGOZI MBAYA/MBOVU,UTUMIAJI MBAYA WA MADARAKA na mengine mengi ni baadhi ya mambo ambayo "ACTION GROUP" Ingeweza kukabiliana nayo Kwa kutumia Vyombo na Taasisi za ndani na nje ya Nchi. Ili maswala kama hayo yasipotee na kuishia hewani "ACTION GROUP" Ichukuwe hatua za kuyafikisha katika taasisi za nchi zinazohusika na ikiwa zitakataa kuyapokea au zitapuuza basi yapelekwe katika taasisi za kimataifa. Ni jambo litakalohitaji Wakati na Moyo mkuu wa kujitolea na bila shaka fedha za uendeshaji pia zitahitajika, ningependa kusikia hoja zenu:
MZEE MWANAKIJIJI, REV KISHOKA, BUBU ATAKA KUSEMA, FIELDMASHER, ELNINO, MWIBA, GAME THEORY, COMPANERO, JUJUMAN, LOLE GWAKISA MARIA ROZA, HALISI, STEVE DII, JULIUS, BINTI MARINGO, NGALA, FIRST LADY na wote ambao majina yenu sikuweza kuyataja kwa leo.
Ndugu wanaogopa
Hukumsikia Lowasa, miongoni mwao hakuna msafi hata moja, kikubwa nani atadhubutu kuanza kumfunga paka kengele????? ukianza kuwapeka mahakamani hutawamaliza, naamini wanaambiana wewe bwana ukingia nilinde mie nilimlinda aliyenitangulia, Hatujawa na huo uthubutu hata kidogo ndugu yangu
Aisifuye mvua imemnyea, maslahi mbele.Wabongo bwana, yaani humu ndani wanoonekana wanampinga Mkapa kwa mkumbo tu wa kwa sababu watu wana sema hivi wako kibaaao!! Acheni ujanja wa kuvizia mtu hadi astaafu ndiyo muanze kusema, kwanza Rais gani duniani ambaye hakuwahi kukosea kwa makosa kama hayo ya kawaida tu?? Kumbe alikuwa sahihi kusema baadhi ya TZ ni wavivu wa kufikiri.
Hebu jiulizeni kashfa aliyopata mtoto wa Koffi Anan kwa ile kashfa ya mafuta mbona Anan hakuandamwaaaa, kwani mnafikiri yule angepata nafasi ya kufanya yale bila baba yake kuwa katibu wa UN!?
Ben, Ben, Ben, mnawonea tu mzee wa watu mwacheni apumzike!! kama mna uchunga kweli komaeni na huyu alienunua Madaraka kwa kuhonga waandishi n.k au mnasubiri astaafu pia!!??