Natumai hao ndugu na majamaa ndo wapo humu ndani kumpigia chapuo ni kama wanalipa fadhila kwa neema waliyoipata kutoka kwake!!..nahisi kabisaa naniii ....atakuwa mmoja wapoHalafu anajifanya yuko busy wakati ameweza kuhudhuria vikao vingi vinavyomuhusu vya chama chao, lakini hajawahi hata siku moja kuhudhuria sherehe za 9 December, Mapinduzi au Muungano tangu atoke madarakani. Naona huupanga ubusy wake uangukie sherehe hizo.
Wewe endelea kuwa busy tu lakini ujuwe hata kama Watanzania hatutakuzomea ukweli tunaujua kwamba wewe ni mwizi na kuna ushahidi wa kutosha kuhusu hili na ulitumia muda mwingi wa madaraka yako kujitajirisha wewe, familia yako na ndugu na jamaa. Watanzania ni wastaarabu hivyo usijipige kifua kwa vile hujazomewa ukadhani tunafurahia utendaji wako ulipokuwa madarakani.
Mkuu umejibiwa mr clean kafanye mengi lakini kaboronga mengi.makaburu wa Africa kusini walimuuliza steve Biko kwamba je hakuna jema lolote ambalo weupe wameifanyia Africa kusini? Akajibu yapo lakini not worth commenting. umejibiwa pia baya moja ufunika mema yote. Research inaonyesha kwamba kukua kwa uchumi huo unaosema ukuendana na kupungua kwa umaskini wala utapiamulo Tanzania. kumbe basi pesa za kigeni zilitokana na tanzania kuuza resources zake kwa pei ya kutupa na siyo uzalishaji mali.Ukiangalia bei halisi ya resources za tanzania alizouza ulinganishe na hayo unayoona amefanya utakuta loss kubwa. Hao waliotangulia na waliofuata wangeuza au wakiuza resources za Tanzania kwa speed na bei ya mkapa taifa lingecolapse.Hataivyo mwanao akiwa wa kwanza darasani baada ya kupata alama 40% utajua darasa hili ni la wachovu huwezi ukamsifia ilihali unajua kafeli.Unajua nashangaa sana, unaposema mtu kafanya vibaya je unalinganisha na nini? Wengine mnaseama alizalisha na kuchukua vile vile, je wanaochukua bila kuzalisha hao tuwaitaje?
Ukitaka ujua uzuri na utendaji wa serekali zote za awamu nne, usimzungumzie tu Mkapa. Wewe toa data za awamu moja baada ya nyingine hapo ndipo tutaona kumbe Mkapa hakufanya kitu. Hili swala lakuongea tu bila ulinganishi ni aibu kwa wasomi. Ili kujua kama mtu amefanya vizuri unatakiwa uangalie vitu vifuatavyo
Umlinganieshe yeye na wenzake katika idara zote, kama haiwezekani uwe na standard za kulinganisha. Huwezi kusema ubatili. Pia jiulize wewe umelifanyia nini taifa lako?
Ili tuondoe ubishi, mnaosema mkapa aliboronga tuambieni ni nani aliyefanya vizuri na ni kwenye maendeo gani yenye tija
Mwacheni ampumzike
mikataba ya kihuni karibu yote ilisainiwa kipindi chake..........kila awamu ilikuwa na mazuri yake na mabaya ukianzia kwa mwl nyerere hadi kwa kikwete. Hayo madudu yaliyofanywa kwenye miaka ya mwisho ya ben na wasaidizi wake yasiwe nongwa. Kina mkono, bhoke na wengine walifaidika na utawala wa awamu ya kwanza.
Linga nisha yaliyofanyika katika awamu ya nne kwa miaka hii mitatu na halafu jaribu kufikiria hali itakuwaje mpaka tunapofika 2015.
Unakubali tulinganishe madudu yao?? Kuzomewa alikokutaja kunahusiana na nini?Kila awamu ilikuwa na mazuri yake na mabaya ukianzia kwa Mwl Nyerere hadi kwa Kikwete. Hayo madudu yaliyofanywa kwenye miaka ya mwisho ya Ben na wasaidizi wake yasiwe nongwa. Kina Mkono, Bhoke na wengine walifaidika na utawala wa awamu ya kwanza.
Linga nisha yaliyofanyika katika awamu ya nne kwa miaka hii mitatu na halafu jaribu kufikiria hali itakuwaje mpaka tunapofika 2015.
- Unaona si nilisema huko nyuma kwamba kuwazomea ni silaha nzito sana tuliyonayo wananchi, hawapendi kuzomewa wanapenda kutukuzwa tu, sasa dawa ni kuyazomea tu, si huyu anasema mwenyewe fears zake kwamba anaogopa kuzomewa, sasa zomea tuu mpaka lirudishe Kiwira,
- Halafu lituambie siri ya kufungua benki yake baada ya kuwa Rais wa 10 years only tena Tanzania wakati Mwalimu miaka 25 hakufngua hata kiosk cha soda!
Respect.
FMEs!
Alishawahi kuzomewa mbona?Sina commemnts.Ninachokijua watanzania tu waoga hatuna ubavu wa kumzomea kiongozi mkubwa kama yeye ila dhambi anazo tena za kutisha.
Mmeona mapokezi yangu, kuna mtu yeyote amenizomea? Sijifichi na wala sikimbii kuzomewa, mimi niko busy sana na shughuli za kimataifa baada ya kumaliza utumishi wangu serikalini, amesema Mkapa.
CHANZO: Habari Leo