Ben kakumbuka shuka kumeshakucha!!!
Si huyu huyu mteule wa Mwalimu?
Aliyoyafanya wakati wa utawala wake sote tunayajua.Yeye aliuza almost kila kitu kwa kuwakaribisha "wawekezaji" , wengi wao wakiwa feki.
Suala la kuwakaribisha wachimbaji wanaotuibia kutwa kucha tunalifahamu fika. Net Group Solutions je? Na ufisadi wao nani alilazimishia?
Ni jambo la kisikitisha Ben anakumbuka Ujamaa na Kujitegemea sasa hivi anapoona mambo akiwa nje ya uongozi.
Anachokiona sasa ndo alichokuwa akiaambiwa mara zote, na yeye akijibu kuwa Watanazania "wavivu wa kufikiri".
Hivi na viongozi wavivu wa kuwasikiliza wananchi wao tuwafanyeje?
Yanayotokea sasa hata nchini kwetu Tanzania , muasisi wake ni Ben William Mkapa. Hatushangai sana kwa yanayotokea ingawaje yanatusikitisha.
Tatizo kubwa tulilonalo ni kwamba wengi wetu huangalia nani kasema nini na hapo kumjibu yule aliyesema bila kuangalia ukweli ya yale aliyoyasema!! Mimi binafsi nakubaliana kabisa na hoja kuwa nchi za Africa haziwezi kuendelea kwa kutegemea misaada toka kwa wajomba wa ughaibuni!! Hiyo ndio hoja ya msingi aliyoiongelea Ben; kama Ben hakuliona hilo alipokuwa Rais, inawezekana kuwa sasa ambapo yuko nje ndio amepata mwanga wa kutafakali kwa kina mambo ambayo yalimpita alipokuwa kiongozi!! Mpirani pia , watazamaji wanafulsa nzuri zaidi kugundua makosa ya team kuliko wale wanaocheza na hasa captain wao!!