Mkapa denounces culture of aid dependency

jaxonwaziri

JF-Expert Member
Feb 17, 2010
375
195
23jfqzd.jpg


Jana kwa wale waliobahatika kumsikiliza Rais mstaafu wa awamu ya Tatu ndugu Ben Mkapa, watakubaliana nami kuwa huyu jamaa amekomaa kimtazamo na namna anavyowakilisha hoja zake na kilichounda hoja yake ni cha maana ambacho kila mmoja wetu anahitajika kukifikiria.

Ben alikuwa anawaasa watu kwenye mkutano unaoendelea hapo Mlimani City kuwa kuna baadhi ya watu/viongozi wa africa (na ni wengi sio wachache) wanaodhani kuna nchi humu duniani zipo kwa ajili ya kuiendeleza Africa, na wala sio Africa yenye wajibu wa kujitambua na kujiendeleza kwa juhudi zake..

Kwa mtazamo wangu mkapa alisema jambo sahihi ambalo kila mwana wa Africa, kiongozi na mwananchi wa kawaida kila mtu kwa nafasi yake anatakiwa alitilie maanani. Kwamba hatuwezi kuwategemea watu fulani waje tu kuja kutuletea maendeleo, tufike mahali tuamue kuwa maendeleo yetu yatakuja kwa juhudi zetu na kwa kufanya kazi kwetu kwa bidii na kwa kufanya maamuzi sahihi.

Mfano mzuri nchi hii, kila hotuba ya kila kiongozi siku hizi ina - kiji uchafu cha '..tunaomba wahisani...' yaani imefikia hatua kujenga barabara, shule, hospitali, miundo mbinu ya maji na mengine mengi tunahitaji wahisani, lakini kununua BMWs, V8s na posjo za vikao tunaweza kwa hela zetu, na isitoshe bado tunaendelea kuwapa wtu misamahaa ya kodi kwa kisingizio cha kuimarisha uwekezaji tena katika resources ambazo sio za kudumu kama madini ambayo huwa yanaisha baada ya kipindi fulani.
Tunahitaji mabadiliko, kuanzia kufikiri kwetu na hatimae kuenenda kwetu.

Mungu ibariki Tanzania na Watu wake, Tujalie kuwa na watu wenye mawazo sahihi juu ya hatima ya watanzania wote wa sasa na wa baadaye. AMEN

Kutoka Daily News:

Mkapa denounces culture of aid dependency


By FINNIGAN WA SIMBEYE,
6th May 2010


FORMER President Benjamin Mkapa today denounced a growing culture of over dependence on external aid among Africans, saying the practice was counterproductive.

Mr Mkapa who was Tanzania president from 1995 to 2005, said the majority of the people on the continent feel that development always needed foreign aid.

"Most of us think that it is other people's responsibility to help us develop ... I find it difficult to understand this culture of over dependence," Mr Mkapa told a well attended news conference as three Commissioners of Africa Commission updated the press on implementation of its recommendations.

Mr Mkapa said in the Commission's report which was sanctioned by former British Prime Minister, Tony Blair, they recommended for aid to be increased but implementation has not been encouraging.

He, however, said despite their aid increment recommendation in the report, it's not mandatory that the developed countries should provide the suggested amount which many African leaders have been calling for.

"People must understand that the responsibility to develop Africa is our own and nobody else," said Tanzania's Third Phase President who is credited with having established credible institutions and policies for economic growth.

Mr Mkapa heaped praise on Ethiopian Prime Minister, Meles Zenawi for his commitment to develop his country with very little foreign aid.

During Mkapa's 10-year administration, government revenue collection skyrocketed from less than 30bn/- in 2005 to more than 100bn/- when he retired. His administration also tamed inflation from double digit (18pc) to single digit of 5 per cent when he left office.

United Nations Human Settlement Development (UN Habitat) Executive Director, Prof Anna Tibaijuka said in the Africa Commission final report, there was a chapter on culture.

Without going into details, Prof Tibaijuka said the Commission's report singled out two major problems facing the continent which include HIV/AIDS and rapid urbanization.

She said the government's latest initiative to rejuvenate the agriculture sector through 'Kilimo Kwanza' would help address the problem of poverty in rural areas and force people to move from urban centres to the countryside.

Prime Minister Zenawi who is also one of the Commissioners, said he was happy to serve on the Commission whose final report's recommendations are currently being implemented.

"I can say that progress that we have seen in Africa recently is because of implementation of the Commission's report," Mr Zenawi noted.

Formed in 2004 to find out the reasons for Africa's underdevelopment, the Commission submitted its final report to Mr Blair in March, 2005.
 
Wapo wengi sana viongozi wa style hiyo. Huo mtindo wao unashuka mpaka ngazi za chini huku kwny halmashauri zetu n.k. Hata kwny mambo yaliyo ndani ya uwezo wao lazima wapeleke vilio vyao serikali kuu ilhali nao wana ngazi za kimaamuzi zitambulikazo kikatiba na vyanzo anuai vya mapato, lakini hawaishi kulilia nyonyo ya Mama (serikali kuu)
 
Ben kakumbuka shuka kumeshakucha!!!

Si huyu huyu mteule wa Mwalimu?

Aliyoyafanya wakati wa utawala wake sote tunayajua.Yeye aliuza almost kila kitu kwa kuwakaribisha "wawekezaji" , wengi wao wakiwa feki.

Suala la kuwakaribisha wachimbaji wanaotuibia kutwa kucha tunalifahamu fika. Net Group Solutions je? Na ufisadi wao nani alilazimishia?

Ni jambo la kisikitisha Ben anakumbuka Ujamaa na Kujitegemea sasa hivi anapoona mambo akiwa nje ya uongozi.

Anachokiona sasa ndo alichokuwa akiaambiwa mara zote, na yeye akijibu kuwa Watanazania "wavivu wa kufikiri".

Hivi na viongozi wavivu wa kuwasikiliza wananchi wao tuwafanyeje?

Yanayotokea sasa hata nchini kwetu Tanzania , muasisi wake ni Ben William Mkapa. Hatushangai sana kwa yanayotokea ingawaje yanatusikitisha.
 
Umenena Lole, natumai hata huyu tulienae akitoka atakua na mtazamo huo huo.
 
Jaxowaziri na Lelo, nawashukuruni. Jaxowaziri anasema Mkapa alisema kitu sahihi na amekomaa kimtazamo, Lelo kakumbuka shuka kumeshakucha. Nakubaliana nanyi wote maana ukiona unaweza kukosoa, ukifanya unashindwa kujikosoa.
 
"People must understand that the responsibility to develop Africa is our own and nobody else," said Tanzania's Third Phase President who is credited with having established credible institutions and policies for economic growth. Mr Mkapa heaped praise on Ethiopian Prime Minister, Meles Zenawi for his commitment to develop his country with very little foreign aid. During Mkapa's 10-year administration, government revenue collection skyrocketed from less than 30bn/- in 2005 to more than 100bn/- when he retired. His administration also tamed inflation from double digit (18pc) to single digit of 5 per cent when he left office.
This is the reason why am saying, despite the rumours that Mkapa had his own dirty deallings, I respect BEN MKAPA.
I urge bwana JK to invite Ben Mkapa in his close advisory ring. That way we, (Tanzanians) will survive the next 5yrs bwana JK is rumoured to rule after this year's general election
 
Imani bila matendo imekufa, Ben ndiye aliyeleta Mkukuta, Minitaiga2020, Mkurabita n.k. ambayo yote ni mipango ya kusaidiwasaidiwa tu!
 
Ben namkubali kama kiongozi anayeweza kusimamia jambo analoliamini na kuwajibika kwa makosa yake. Sio mtuu wa kulialia na kuonewaa huruma kila wakati eti anadanganywa au alidanganywaa..Kiongozii ni kuonyesha njia na kuwajibika kwa makosaa yake..

Katika international paltform Ben yuko juu sana kutokana na uwezo wake wa kuchambua mambo na kutoa mawazoo imara ya kusonga. Utawala wake unayo mapungufu yake ila yale aliyowezaa kuyasimamia vema (uchumi, miundombinu, elimu, afya,nk) ni ishara ya independent thinking ilivyo muhimu katika kusimamia maono ya uongoziii.. Bravo Ben u always make us proud!!!!
 
Ben namkubali kama kiongozi anayeweza kusimamia jambo analoliamini na kuwajibika kwa makosa yake. Sio mtuu wa kulialia na kuonewaa huruma kila wakati eti anadanganywa au alidanganywaa..

Mbona hapa analia kuwa alidanganywa/tulidanganywa:

"We privatized everything the state had. Everything was bought by foreign capital because we had no national capital to compete. The foreign companies almost always closed local businesses, which were not competitive, transforming them into distributors of foreign products and driving up unemployment. The experts of the World Bank and the IMF predicted that this would happen, but they told us: Now the influx of foreign investment will lead to the creation of new, competitive and technologically current businesses that will provide the foundations for a lasting, modern development. None of this happened for us" - Ben

Chanzo: http://businessmirror.com.ph/home/opinion/14843-the-sudden-demise-of-neoliberal-economics.html
 
Huwa namkubali sana Ben. Anauwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuisimamia! Hata ukiangalia maamuzi yake kipind cha utawala wake, alikuwa na nia ya dhati ila execution yake ndo pengine ilikuwa problem! anyway, the guy is brilliant!
 
Ben kakumbuka shuka kumeshakucha!!!

Si huyu huyu mteule wa Mwalimu?

Aliyoyafanya wakati wa utawala wake sote tunayajua.Yeye aliuza almost kila kitu kwa kuwakaribisha "wawekezaji" , wengi wao wakiwa feki.

Suala la kuwakaribisha wachimbaji wanaotuibia kutwa kucha tunalifahamu fika. Net Group Solutions je? Na ufisadi wao nani alilazimishia?

Ni jambo la kisikitisha Ben anakumbuka Ujamaa na Kujitegemea sasa hivi anapoona mambo akiwa nje ya uongozi.

Anachokiona sasa ndo alichokuwa akiaambiwa mara zote, na yeye akijibu kuwa Watanazania "wavivu wa kufikiri".

Hivi na viongozi wavivu wa kuwasikiliza wananchi wao tuwafanyeje?

Yanayotokea sasa hata nchini kwetu Tanzania , muasisi wake ni Ben William Mkapa. Hatushangai sana kwa yanayotokea ingawaje yanatusikitisha.

kuna tofauti kubwa kati ya uwekezaji na misaada
 
Ben alifanya kazi nzuri ya kuweka mazingira ya uwekezaji. Uwekezaji ndani ya nchi hata uwe wa mtaji mdogo kiasi gani una positive impact kwa njia moja au nyingine. Shida ya kwetu ni wale watunga sera na watekelezaji ndiyo hawapo makini kabisa.
 
Kusema kweli Kikwete alisikitisha pale aliposema eti nchi maskini kama Tanzania haziwezi kujitoa zilipo na kuwa nchi tajiri zinawajibu wa kuzisaidia nchi maskini. Ukweli ni kuwa nchi maskini hazioneshi kufanya chochote. Mojawapo ya maswali aliyoulizwa kikwete ni ikiwa nchi maskini zinafanya juhudi za kutosha kujitoa pale zilipo. Mtazamo wa wataalam wengi ilikuwa serikali maskini nyingi za Afrika hazifanyi juhudi za kutosha. Majibu ya Kikwete yalikuwa ni ya kisiasa tu na kusema ukweli hakujibu lolote la maana.

Hapa mkapa inaonekana ametoa veiled statement ya kupingana na Kikwete na kumpasha kuwa kutegemea misaada hakukumsaidia yeye na hakutamsaidia Kikwete wala rais yeyote wa Africa. Na hizo foreign direct investiment zilizoahidiwa na Benki ya Dunia haziji vile vile. Zile kidogo zinazokuja zinakuja kwenye maeneo predictable sana kwa mfano kwenye madini, mafuta na mawasiliano. Hakuna FDI inayokuja kwenye Kilimo wala processing industries. Tena zinakuja baada ya kupewa vivutio vya kupindukia. Vivutio vinavyofanya biashara hizo zisiwe sustainable kwa sababu siku vivutio hivyo vikiondolewa biashara hizo zitafungwa.

Njia pekeee iliyobaki ni kwa nchi zenyewe kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali. Hili ni gumu sana ukizingatia serikali nyingi ni hohe hahe, fisadi na zisizo na ufanisi. Kwa hiyo kitu cha kwanza muhimu ni kuleta mabadiriko makubwa ndani ya serikali yatakayoleta ufanisi. Mojawapo ya vitu vinavyolalamikiwa na hao wenye FDI ni milolongo ya taratibu zisizoeleweka, kudaiwa rushwa, ucheleweshaji wa makusudi kwa nia ya kushawishi rushwa, n.k. Mambo yote haya yako ndani ya uwezo wa waafrika wenyewe kuyatatua.

Misaada haitaondoa rushwa na red tape. Misaada haitaleta ufanisi katika serikali zisizo na ufanisi. Sana sana misaada inafanya nchi nyingi maskini ziendelee kuwa vile zilivyo (maintain status quo). Misaada inasababisha kusiwe na incentive ya kufanya reformation na kuleta ufanisi. Misaada inawafanya viongozi wengi wasiwe wabunifu na kuangalia njia mbadala za kutafuta mapato ya serikali ndani ya mipaka yao. Kwa kifupi misaada mingi haiwezi kumtoa Matonya barabarani, sana sana itafanya akina matonya wawe wengi zaidi bara barani.

Huo ndo ukweli na pengine Mkapa ameuona akiwa nje ya madaraka. Pengine hata Kikwete atagundua hilo akishatoka madarakani kama Mwinyi alivyojua kuwa azimio la Arusha lilikuwa zuri baada ya kutoka madarakani.

Kutotegemea misaada kunampa changamoto kiongozi. Si viongozi wengi wa nchi maskini kama Tanzania walio tayari kwa changamoto kama hizo. Kitu chepesi kwao ni kukubali kupokea misaada na masharti yanayoambatana nayo. Hata hivyo kitu hicho kimeshatuthibitishia kuwa hakina faida ya muda mrefu.
 
Ninahisi JK huwa hasomi maoni haya, natamani angekuwa japo anapita pita huku kuchukua ushauri wa bure maana naona wale jamaa zake wanamdanganya kwa mengi maana wanaona anadanganyika. Kuna wakati huwa najiuliza: Hivi huwa anafanya kazi kweli pale magogoni ama huwa anajipumzisha tu! mbona baba wa taifa alikuwa anasoma, anaandika na anazunguka huku na huko? Ndugu yetu vp, naona vyeo vya kutunukiwa tu, mara Dokta.
Halafu, kama anawahutubia hata wasomi wa nchi za watu, mbona sijawahi kusikia anathubutu kuhutubia katika chuo kikuu chochote nchini,(labda alishajaribu UDOM), vipi kuhusu pale Nkurumah? Mzumbe?
 
He said it was dejecting that more than 50 years since most of African countries attained independence, they have continued to looking for aid as a way of emancipation.

"We chased away colonialists knowing that they will not give us independence. How come then that now we are returning to hem asking for aid?" he posed, adding: "We need to accept that change is our responsibility. Extraordinary dependence is not only a shock, it is disgraceful…we should get on our feet and think for ourselves."

Katika hii 50 years, miaka 10 si alikuwa madarakani huyu? mbona simwelewi huyu Baba jamani?? Je miaka yake ofisini ni msingi upi ameweka wa kuliezesha taifa lake kuondokana na utegemezi? Naomba kusaidiwa jamani.

The citizen
 
Uwekezaji wekeza, wekezwa wawekezeji, duh Ben nimemsikia sijui ndio ile majibu ya akina Sumaye kuwa hawakuelewa kwanini hatuendelei mpka walipoenda Havard inawezekana sasa Ben naye baada ya kukaa nje ya wanja sasa aweza ona vema fursa za kufunga magoli na anashangaa kwanini mastriker wanavutavuta miguu!!
 
MM hapo umenena! ni sawa na Padre au Mchungaji kukumbuka maji ya baraka akishakuwa kafunga ibada na kanzu kaweka kando!
 
Jaxonwaziri,
Aliyosema Mkapa ni maneno yaliyosemwa na viongozi wengine toka mwaka 1960..Hata kina Bob Marley waimbaji wimbo ni huo huo tu. Infact, Mkapa ni mmoja wa Viongozi waliopinga msemo huo kwa vitendo vyao.
Mkuu watu wapo wengi sana aina ya Mkapa wanaosoma Biblia na kuitangaza kwa nguu zote hali matendo yao ni kinyume cha mafundisho ya Biblia..Sasa sielewi kama hawa watu wana akili sana au?
 
"One thing is clear. Globalisation is driven by the pursuit of profit, by being competitive, and by the interplay of power relations - power to determine the framework and rules of the game; power of technology to cut costs and increase the speed of production and delivery; political and military power to pursue national goals unilaterally if necessary; and power to influence others. The way I see it, the game is very well underway, and we have been dealt a card. It is a bad card, to be sure. Yet, we must play. How smartly we play the card we have, and how effectively we demand a fair game, is what will determine whether we remain relevant to, and benefit from, the unprecedented integrative forces that shape our world, or whether we will entrench our irrelevance and impoverishment" – The then President Mkapa's ‘Statement at the Launching of the National Dialogue on the Social Dimension of Globalisation, 19 August 2002'

Huyo ndio alikuwa Mkapa enzi zake. Bingwa wa kuutetea utandawazi. Kipenzi cha Wafadhili na Wawekezaji.
 
Back
Top Bottom