Mkapa apanda kizimbani Kisutu

Inaonekana hii picha ameitoa kwenye website ya Mwananchi. Lakini huko hawajaandika kwamba hii picha wameichukua mahakamani. Wameandika tu ni picha ya Mkapa.
 
Picha nimetuma kwa mods watuwekee. Nimepiga za kutosha.

Wamemaliza wataendelea na mashahidi wengine... Wako nje watu wanampongeza Mkapa
 
tuzifuatilie hatua za huyu jamaa kwa umakini sana, haya ni maandalizi yake ya kugombea Urais
 
Inaonekana hii picha ameitoa kwenye website ya Mwananchi. Lakini huko hawajaandika kwamba hii picha wameichukua mahakamani. Wameandika tu ni picha ya Mkapa.
members wengine hawaoni kama ni issue kwa jinsi wanavyopoteza credibility yao hapa jamvini. Si ajabu mwishowe wakaja kuambiwa kuwa 'wanasubiria matokeo yao ya form iv!

asante sana mkuu n00b kwa kutujuza
https://www.jamiiforums.com/members/n00b.html

 
Inawezekana hizo siri anazoficha Mkapa ndio ushahidi muhimu wa aidha kumtia hatiani au laa Mahalu, sasa kama zitafichwa kuna umuhimu gani wa yeye Mkapa kuja mahakamani ? na anatarajia mahakama iote ?
 
Marando jembe yaani kafanya mpaka Mkapa kasimama kizimbani
 
EPA ataenda nini ? mbona kaanza kuwatetea jamaa zake? JK watch out closely..........huyu kafungua mlango wa kuweza kushitakiwa ama kutakiwa kutoa ushahidi mwsho wa siku kilafisadi atasema wewe ndio shahidi ,tukianzia na Richmond.
 
Hao mawakili wa serikali vipi? kwenye cross examination wameuliza maswali gani haswa au wamemchekea tu? Swali la kwanza na la muhimu kutest credility yake walitakiwa wamuulize kwanini alifanya biashara ikulu!

Infact, walitakiwa wamuulize ANBEN ilikuwa kampuni yake na ilikuwa inafanya biashara gani, na 1st registered office ilikuwa wapi? Kisha waswitch waulize maswali ya mgodi wa Kiwira. Akishaanza kujiumauma ndio waulize maswali ya jengo la Italy!

The sky is the limit!
 
  • Thanks
Reactions: ral
Mkapa:
Nilitoa maelekezo ya kununua jengo kama India, Us na Uingereza.
Sikuuliza kwanini ilikua akaunti 2 tofauti.
Siwezi kusema siri nyingine maana zinaweza kuleta matatizo ya Kidiplomasia na Italy. Thanks God Italy hawakuwahi kulalamika!


Kwa akili yangu finyu ni kwamba unapotoa ushahidi mahakamani unatakiwa kusema ukweli bila kuficha kitu. Na ndio maana unaapa kwa kutumia kitabu kitakatifu kuwa utasema ukweli.

Sasa kama utaficha baadhi ya maneno eti ni siri, hapo kiapo ulichoapa ni sawa na bure. Ushahidi wake hautoshelezi kabisa.

ARUDIE TENA KUTOA USHAHIDI, FISADI MKUBWA HUYU!!!!.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Huyu hakupaswa kupanda Mahakamani kutoa ushahidi bali alipaswa kupanda Mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi na kufanya biashara akiwa Ikulu.

Usiwe na wasiwasi mkuu. Huyu Mkapa kesha anza kuchukua mazoezi ya kwenda mahakamani, maana tukichukua tu nchi huyu jamaa lazima akaozee Segerea
 
Back
Top Bottom